Agano Jipya 2023
Machi 26. Ni kwa Jinsi Gani Wasichana na Wavulana Wanaweza Kufanya Kazi Pamoja ili Kusaidia Kujenga Ufalme wa Mungu? Mathayo 13; Luka 8; 13


“Machi 26. Ni kwa Jinsi Gani Wasichana na Wavulana Wanaweza Kufanya Kazi Pamoja ili Kusaidia Kujenga Ufalme wa Mungu? Mathayo 13; Luka 8; 13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Machi 26. Ni kwa Jinsi Gani Wasichana na Wavulana Wanaweza Kufanya Kazi Pamoja ili Kusaidia Kujenga Ufalme wa Mungu?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
mkutano wa baraza la kata.

Machi 26

Ni kwa Jinsi Gani Wasichana na Wavulana Wanaweza Kufanya Kazi Pamoja ili Kusaidia Kujenga Ufalme wa Mungu?

Mathayo 13; Luka 8; 13

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki urais wa darasa au wa akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni kwa jinsi gani ninaweza kupata furaha kwa kumfuata Yesu Kristo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Nani katika kata yetu au jamii yetu anahitaji msaada wetu? Tunawezaje kuwasaidia?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana kujiandaa kwa ajili ya huduma ya ummisionari?

  • Unganisha familia milele. Je! Tunaweza kuchangia vipi katika juhudi za kata za kazi ya historia ya familia na kazi ya hekaluni?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kukiwa na mfululizo wa mafumbo yanayopatikana katika Mathayo 13, Mwokozi alifundisha kweli muhimu kuhusu ufalme wa Mungu na ukuaji wake usio na kifani katika siku zetu. Katika mawili kati ya mafumbo haya, kitu kidogo na rahisi kinakuwa na matokeo ya kitu kikuu. Na ilikuwa ni matendo ya mwana au binti ya Mungu ambayo yalisaidia muujijza kutokea. Mbegu ndogo sana ya haradali ilikuwa kuwa mti mkubwa vya kutosha kwa ndege “kufanya makazi kwenye matawi” ambayo “aliyoitwaa mtu na akaipanda katika shamba lake” (Mathayo 13:31–32). Na kiasi kidogo cha chachu hufanya kiasi kikubwa cha kinyunya kufura wakati “chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga” (Mathayo 13:33). Ufalme wa Mungu katika siku zetu hutakua na kuenea kwa sababu Watakatifu Wake—ikijumuisha wasichana na wavulana—wanafanya kazi pamoja Naye kuujenga.

Katika nyongeza ya kusoma Mathayo 13 na Luka 813 wiki hii, fikiria kusoma ujumbe wa Rais M. Russell Ballard “Men and Women in the Work of the Lord” (New Era, Apr. 2014, 2–5) na ujumbe wa Rais Jean B. Bingham “Kuungana katika Kufanikisha Kazi ya Mungu” (Liahona, Mei 2020, 60–63).

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia vijana unaowafundisha kupiga taswira ya mafumbo katika Mathayo 13, fikiria kuonyesha picha ya mbegu ya haradali, chachu (kama iliki), lulu, na wavu wa kuvulia. Vijana wangeweza kupitia tena Mathayo 13:31–33, 45–48 na kushiriki kile kila moja ya mafumbo haya yanawafundisha kuhusu ufalme wa mbinguni. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia jumbe za mafumbo haya katika maisha yetu wenyewe? Je, tunafanya nini ili kumsaidia Bwana kuujenga ufalme Wake? Hapa kuna shughuli chache ambazo zinaweza kusaidia katika majadiliano.

  • Kabla ya mkutano, waalike washiriki wa darasa au akidi kujifunza kuhusu wanawake na wanaume ambao ni au walikuwa mfano mzuri katika kusaidia kuujenga ufalme wa Mungu. Watu hawa wangeweza kuwa kutoka kwenye maandiko, (ona “Nyenzo Saidizi”), kutoka kwenye historia ya Kanisa, au kutoka kwenye maisha yao wenyewe. Alika vijana kushiriki kile walichojifunza. Ni kwa njia gani watu hawa walimsaidia Bwana kujenga ufalme Wake? Ni jinsi gani tunaweza kufuata mifano yao?

  • Kama unawafundisha wavulana, waalike kuupitia tena ujumbe wa Rais Bonnie L. Oscarson “Wasichana katika Kazi” (Liahona, Mei 2018, 36–38) na watafute na kushiriki njia ambazo wasichana wanachangia katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Wasichana wangeweza kufanya upekuzi kama huo katika ujumbe wa Kaka Douglas D. Holmes “Kile Ambacho Kila Mwenye Ukuhani wa Haruni Anahitaji Kuelewa” (Liahona, Mei 2018, 50–53). Ni kwa jinsi gani majukumu ya wasichana na wavulana yanafanana? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya vyema pamoja tunapofanya kazi ya Mungu?

  • Ili kuwasaidia vijana kuelewa jinsi wanawake na wanaume wanafanya kazi pamoja katika kuujenga ufalme wa Mungu, ungeweza kuandika maswali ubaoni kama haya: Kwa nini Mungu anahitaji wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja kuujenga ufalme Wake? Ni kwa jinsi gani urais wa darasa na akidi unaweza kufanya kazi vyema pamoja? Vijana wangeweza kupitia tena sehemu za ujumbe wa Rais M. Russell Ballard “Wanaume na Wanawake katika Kazi ya Bwana” au ujumbe wa Rais Jean B. Bingham “Kuungana katika Kufanikisha Kazi ya Mungu,” hasa sehemu inayoanza na “Kwa hivyo hiyo inamaanisha nini kwako wewe na mimi?” Vijana wangeweza kushiriki majibu waliyopata kwa ajili ya maswali hayo.

  • Ili kuwasaida vijana kuelewa jinsi wanaweza kuujenga ufalme wa Mungu, fikiria kuonyesha video moja ua zaidi “We Are Strong Together,” “A Promise for the Lord’s Battalion,” na “Youth Responsibility in the Work of Salvation” (ChurchofJesusChrist.org). Je, tunafanya nini katika nyumba zetu, kata zetu, na jamii yetu ili kusaidia katika kazi ya Mungu? Fikiria kumuomba rais wa darasa au akidi kutoa maswala yaliyojadiliwa katika mikutano ya baraza la vijana ya kata ambayo inafaa kushirikiwa. Waalike washiriki wa darasa au akidi kushiriki umaizi kuhusu jinsi wangeweza kusaidia katika maswala haya.

Picha
msichana akilima

Mungu anawahitaji wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja katika kujenga ufalme wa Wake.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Wakati unapotoa mwaliko wa kuishi kanuni fulani, wasaidie wanafunzi kugundua baraka ambazo Mungu ameahidi kwa wale ambao wanaishi kanuni hiyo.

Chapisha