“Aprili 9. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuimarisha Ushuhuda Wangu wa Ufufuko wa Yesu Kristo? Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Aprili 9. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuimarisha Ushuhuda Wangu wa Ufufuko wa Yesu Kristo?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Aprili 9
Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuimarisha Ushuhuda Wangu wa Ufufuko wa Yesu Kristo?
Pasaka
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki urais wa darasa au wa akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha, kwa nyongeza kwenye kushauriana kuhusu shughuli mahsusi ya darasa au shughuli za akidi, mnaweza kutaka kujadili misukumo na Dhima kutoka mkutano mkuu. Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia.
-
Ni dhima zipi au jumbe zipi zimejitokeza bayana kwetu? Ni nini kuliimarisha imani yetu katika Yesu Kristo?
-
Ni nini kiliimarisha shuhuda zetu juu ya manabii walio hai? Ni nini tulihisi kushawishika kufanya kwa sababu ya kile tulichojifunza au kuhisi?
-
Ni nini tunahitajika kufanya kama darasa au akidi ili kukumbuka na kutendea kazi ushauri tuliousikia katika mkutano mkuu?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Mitume wote wa kale na kisasa wanashuhudia kwamba Yesu Kristo yu hai! Aliteseka na kufa msalabani, Yeye alizikwa kaburini, na siku ya tatu Yeye alifufuka tena. Kwa sababu Yeye alishinda kifo, sisi sote tutafufuliwa. Ufufuko wa Mwokozi ulileta ahadi ya kutokufa na matumaini ya uzima wa milele. Ahadi hii iko katika moyo wa Pasaka.
Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tuna sababu ya kuamini kwamba Yesu Kristo alifufuka. Katika nyongeza ya ushahidi wa watu wa nyakati za Agano la Kale, tuna shuhuda za watu ambao waliishi nyakati za Kitabu cha Mormoni, Nabii Joseph Smith, na manabii na mitume wetu walio hai. Tunaweza pia kupata ushahidi binafsi wa Ufufuko kupitia Roho Mtakatifu. Ni kwa jinsi gani utawasaidia vijana kuimarisha shuhuda zao kwamba Yesu Kristo alifufuka? Unapojiandaa, fikiria kujifunza ujumbe wa Dada Reyna I. Aburto “Kaburi Halina Ushindi” (Liahona, Mei 2021, 85–86) na ujumbe wa Mzee S. Mark Palmer “Huzuni Yetu Itageuzwa kuwa Shangwe” (Liahona, Mei 2021, 88–89).
Jifunzeni Pamoja
Ungeweza kuanza kwa kujadili kuhusu Ufufuko wa Yesu Kristo kwa kuwaalika vijana kushiriki kile walichofanya wiki hii kusherekea Pasaka. Ungeweza kuwauliza kile walichojifunza au kufanya binafsi au pamoja na familia zao kuimarisha shuhuda zao za Ufufuko wa Mwokozi. Hapo chini kuna shughuli za kuwasaidia washiriki wa darasa lako au akidi yako kuimarisha shuhuda zao?
-
Jadilini pamoja kwa nini shuhuda ni muhimu katika maisha ya kila siku. Kisha tengeneza orodha ya ushahidi mwingi wa Ufufuko wa Yesu jinsi darasa lako au akidi yako inavyoweza kufikiria. Kila mtu angeweza kisha kuchagua maandiko kutoka katika yale yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo Saidizi” kujifunza kuhusu baadhi ya shuhuda hizi. Waalike washiriki wa darasa au akidi kushiriki kile walichojifunza. Wahimize wao pia kushiriki jinsi shuhuda hizi ziliimarisha shuhuda zao za Ufufuko wa Yesu Kristo.
-
Ni zipi baadhi ya hali ambapo ungeweza kushiriki shuhuda zao za Ufufuko wa Mwokozi. Kama mtu yeyote katika darasa au akidi amepata uzoefu wa kuzungumza mtu kuhusu Ufufuko wa Mwokozi, fikiria kumualika yeye kushiriki uzoefu huo. Wahimize washiriki wa darasa au akidi kufikiria kuhusu jinsi wangeweza kumsaidia mtu kuelewa Ufufuko wa Yesu Kristo na kupata ushuhuda ambao kwa sababu Yake sisi sote tunaweza kufufuliwa. Ni kweli gani muhimu kuhusu Ufufuko kwa watu wote ambazo zingekuwa muhimu kuwafundisha wengine? Washiriki wa darasa lako au akidi wangeweza kupata baadhi ya maswali katika maandiko katika “Nyenzo Saidizi.”
-
Wakati Mitume walimwambia Tomaso walikuwa wamemwona Mwokozi aliyefufuka, Tomaso alisema angeamini bila yeye kujionea kwa macho mwenyewe. Baadaye Yesu alimwambia Tomaso, “Heri wale wasioona, na wakasadiki.” Pitia tena uzoefu wa Tomaso, unaopatikana katika Yohana 20:24–29. Ni kwa jinsi gani umebarikiwa kwa kuamini katika Mwokozi bila kumuona Yeye? Ni kwa jinsi gani tunaimarisha imani yetu katika Yesu Kristo? Waalike washiriki wa darasa au akidi kupekua ujumbe mmoja ua mwingine kutoka kwa viongozi wa Kanisa katika “Nyenzo Saidizi” na kushiriki kwa nini wanashukuru kwa ajili ya Ufufuko wa Mwokozi. Ni kwa jinsi gani ufahamu wetu kwamba tutafufuliwa unaathiri jinsi tunavyofikiria kuhusu miili yetu na maamuzi tunayofanya?
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Luka 24:36–48; Yohana 20:11–29; 1 Wakorintho 15:3–8; 3 Nefi 11:1–15; Etheri 12:38–39; Mafundisho na Maagano 76:19–24 (Ushahidi wa Ufufuko)
-
2 Nefi 9:10–15; Mosia 16:8–11; Alma 11:42–45; Alma 40:23–25; Mafundisho na Maagano 93:33–34 (Maandiko ambayo yanafundisha kuhusu Ufufuko wa watu wote)
-
D. Todd Christofferson, “Ufufuko wa Yesu Kristo,” Liahona, Mei 2014, 111-14.
-
Gerrit W. Gong, “Hosana na Haleluya—Yesu Kristo Aliye Hai: Kiini cha Urejesho na Pasaka,” Liahona, Mei 2020, 52–55
-
Reyna I. Aburto, “Kaburi Halina Ushindi,” Liahona, Mei 2021, 85–86
-
S. Mark Palmer, “Huzuni Yetu Itageuzwa kuwa Shangwe,” Liahona, Mei 2021, 88–89
-
Video za Pasaka zinaweza kupatikana katika ChurchofJesusChrist.org/study/video/easter-videos.