Agano Jipya 2023
Aprili 23. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Upendo Mkuu kwa Wale Wanaonizunguka? Mathayo 18; Luka 10


“Aprili 23. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Upendo Mkuu kwa Wale Wanaonizunguka? Mathayo 18; Luka 10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Aprili 23. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Upendo Mkuu kwa Wale Wanaonizunguka?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
Msamaria Mwema, na Annie Henrie Nader

Msamaria Mwema,

Aprili 23

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Upendo Mkuu kwa Wale Wanaonizunguka?

Mathayo 18; Luka 10

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja au mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni uzoefu gani wa karibuni uliotuleta karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Je, Kuna mtu amehamia kwenye kata yetu au kujiunga na Kanisa? Tunawezaje kuwasaidia wao wajisikie kukaribishwa?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, kuna shughuli zozote zinazokuja ambazo tunaweza kuwaalika marafiki zetu kuhudhuria?

  • Unganisha familia milele. Je, ni juhudi gani tunaweza kufanya kuandika historia yetu binafsi?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Baada ya Yesu kufundisha “mwanasheria” mmoja umuhimu wa amri mbili kuu—kumpenda Mungu na kumpenda jirani yetu—mwana sheria aliuliza, “Jirani yangu ni nani?” (ona Luka 10:25–29; Mathayo 22:35–40). Kwa kumjibu, Mwokozi alishiriki fumbo kuhusu Msamaria ambaye alihatarisha maisha yake kumtunza mtu Myahudi aliyejeruhiwa, alimchukua mtu yule kwenye hifadhi kumtunza, na alilipa gharama zote za kuuguzwa. Msamaria hakuzingatia tofauti kati yake na mtu yule ambaye alifikiriwa kuwa adui na watu wake, au kumhukumu au kupata sababu za kutomsaidia. Alimhudumia mtu aliye na mahitaji, licha usumbufu wa kibinafsi na dhabihu, kwa hiyo kuonyesha upendo kwa ajili ya mtu yule na kwa ajili ya Mungu. Unapotafakari mafundisho ya Mwokozi katika Luka 10:25–37, fikiria kuhusu kile hasa maana ya “mpende … jirani yako kama nafsi yako” (mstari wa 27).

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa kwamba wanapowahudumia wale wanaowazunguka, wanaonyesha upendo wao kwa Mungu? Ni nini kinawashawishi kuwapenda na kuwahudumia wengine? Unapojiandaa, unaweza kupitia tena ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Amri Kuu ya Pili” (Liahona, No. 2019, 96–100).

Jifunzeni Pamoja

Ili kuanza majadiliano kuhusu kuonyesha upendo mkuu kwa wale wanaotuzunguka, ungewaomba washiriki wa darasa au akidi kushiriki kile wamejifunza kuhusu kuwapenda wengine kutokana na fumbo la Msamaria mwema, linapatikana katika Luka 10:25–37. Je, tunajifunza nini kuhusu uhusiano kati ya amri kuu ya kwanza na ya pili kutoka katika 2 Wakorintho 10:27 na kauli ya Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo Saidizi”? Mawazo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuendeleza mjadala kuhusu kuonesha upendo kwa wale wanaotuzunguka.

  • Yesu Kristo ni mfano wetu mkuu wa kuonyesha upendo wa Mungu kwa kuwahudumia wengine, na washiriki wa darasa au akidi watapata mwongozo kwa kujifunza mfano Wake. Mwalike kila mtu kuwaza juu maisha ya duniani ya Yesu Kristo na kuchagua uzoefu kutoka kwa maisha Yake ambao unaonyesha upendo Wake mkuu kwa wengine. Muombe kila mtu kushiriki uzoefu waliouchagua, pamoja na kwa nini ni muhimu kwao. Waalike wale unaowafundisha kufikiria njia moja wangeweza kufuata mfano wa Mwokozi wa upendo. Wangeweza pia kushiriki mawazo yao kuhusu mtu wanayemjua ambaye anafuata mfano huu.

  • Shiriki na jadili na washiriki wa darasa au akidi kauli ya Rais Russell M. Nelson inayopatikana katika “Nyenzo Saidizi.” Waalike washiriki wa darasa au akidi kupitia tena ujumbe mmoja au zaidi wa mkutano mkuu iliyotajwa mtandaoni, wakitafuta mafundisho ambayo yanaweza kutuongoza katika juhudi zetu za kuwapenda wengine. Wangeweza kufokasi kwenye yafuatayo: mifano ya jinsi tunaweza kuhudumu kutoka katika “Amri ya Pili Kuu” na Rais Nelson; sehemu ya III, na VI katika ujumbe wa Rais Oaks “Kuwapenda Wengine na Kuishi na Tofauti”; na hadithi kuhusu sungura na ushauri kwa vijana kutoka katika “Mioyo Iliyofumwa Pamoja” na Mzee Gary E. Stevenson. Mngeweza pia kusoma pamoja Mosia 2:17 na Moroni 7:45–48. Ingeweza kusaidia kuandika mafundisho yaliyojadiliwa na vijana ubaoni. Kisha darasa au akidi ingeshauriana pamoja kuhusu njia mahsusi wanaweza kutumia vyema mafundisho haya kwenye mahusiano yao na wanafamilia, na marafiki, na ndani ya jamii yao, hata wakati watu wanaonekana vigumu kuwapenda.

  • Juhudi za washiriki wa darasa au akidi katika kazi ya wokovu na kuinuliwa zitakuwa na maana zaidi na furaha wakati wanahisi kushawishiwa na upendo. Ili kuwasidia wao kuona jinsi kila kipengele cha kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 1.2) kinahamasishwa na upendo, andika vipengele vinne ubaoni. Kisha waombe vijana kujadili jinsi gani kuwa na moyo uliojaa upendo kwa wengine kunaweza kubadili jinsi wanashiriki kila kipengele. Wanaweza kuwa na uzoefu kutoka katika maisha yao wenyewe au maisha ya wengine wangeweza kushiriki.

Picha
Wavulana na wasichana wakipamba keki

Rais Russell M. Nelson alifundisha, “Tunapompenda Mungu kwa mioyo yetu yote, Yeye hubadilisha mioyo yetu kwa ustawi wa wengine.”

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

  • Dallin H. Oaks, “Kuwapenda Wengine na Kuishi na Tofauti,” Liahona, Nov. 2014, 25–28

  • Gary E. Stevenson, “Mioyo Iliyofumwa Pamoja,” Liahona, Mei 2021, 19–23

  • A Good Samaritan,” “The Greatest Commandment” (video), ChurchofJesusChrist.org

  • Rais Dallin H. Oaks alifundisha: “Lakini ari yetu ya kutii amri hii ya pili lazima isitusababishe kusahau ya kwanza, kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote, roho na akili. … Lazima tujaribu kutii amri kuu zote mbili. Ili kufanya hivyo tunatembea mstari mwembamba sana kati ya sheria na upendo—kutii amri na kutembea njia ya agano, wakati tukiwapenda jirani zetu tukiwa njiani. Safari hii inatuhitaji kutafuta uvuvio wa kiungu juu ya nini cha kuunga mkono na cha kupinga na jinsi ya kupenda na kusikiliza kwa utiifu na kufundisha katika mchakato huo. Safari yetu inahitaji kwamba tusilegeze kamba juu ya amri bali tuoneshe kipimo kikamilifu cha uelewa na upendo” (“Amri Mbili Kuu,” Liahona, Nov. 2019, 73–75).

  • Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Watakatifu wa Siku za Mwisho … kwa dhati wanatafuta kuishi amri kuu ya kwanza na ya pili. Tunapompenda Mungu kwa mioyo yetu yote, Yeye hubadilisha mioyo yetu kwa ustawi wa wengine katika mzunguko mzuri, wa wema. … Kutoa msaada kwa wengine—kufanya bidii ya kuwajali wengine kama vile au zaidi ya sisi tunavyojijali—ni shangwe yetu. Hasa, naweza kuongeza, wakati ambapo si muafaka na wakati ambapo kufanya hivyo hututoa katika eneo letu la faraja Kuishi amri hiyo kuu ya Pili ni kiini cha kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo” (“Amri Mbili Kuu,” Liahona, Nov. 2019, 97, 100).

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Uzoefu wako binafsi wa kuishi injili utakuwezesha kutoa ushuhuda wa nguvu wa kanuni unazofundisha. Kwa sababu unaziishi kanuni hizo, Roho Mtakatifu anaweza kushuhudia ya kwamba yale unayoyafundisha ni ya kweli.

Chapisha