“Mei 14. Ni kwa Jinsi Gani Bwana Huwasaidia Wanaume na Wanawake Kufanya Kazi kwa Pamoja katika Ndoa? Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Mei 14. Ni kwa Jinsi Gani Bwana Huwasaidia Wanaume na Wanawake Kufanya Kazi kwa Pamoja katika Ndoa?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Mei 14
Ni kwa Jinsi Gani Bwana Huwasaidia Wanaume na Wanawake Kufanya Kazi kwa Pamoja katika Ndoa?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Ni kwa jinsi gani kumgeukia Bwana hutusaidia kukabiliana changamoto zetu na majaribu yetu?
-
Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Nani tunamjua ambaye anahitaji maombi yetu na urafiki wetu?
-
Waalike wote kuipokea injili. Ni mipango gani ya kushiriki injili iliyojadiliwa katika mikutano ya baraza la vijana la kata? Ni kwa jinsi gani darasa letu au akidi yetu inaweza kushiriki?
-
Unganisha familia milele. Ni kwa jinsi kufanya kazi ya historia ya familia kunaweza kuimarisha mahusiano yetu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Kuanzia Adamu na Hawa, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wametafuta kuimairisha na kuwaunganisha wake na waume katika ndoa. Mwokozi alifundisha, “Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja” (Mathayo 19:5). Wakati huo huo, Shetani anafanya yote anayoweza kuvunja ndoa na kaungamiza familia. Washiriki wa darasa au akidi yako kuna uwezekano wanajua changamoto nyingi ambazo zinakumba ndoa siku hizi. Labda pia wanameshaona wake na waume wakifanya kazi pamoja na kutafuta msaada wa mbinguni ili kupata umoja. Tafakari jinsi uzoefu huu ungeweza kuwa kuwafundisha wao kuhusu kile kinachohitajika kupata umoja ndani ya ndoa. Ni kitu gani unachoweza kufanya kuwafundisha wao umuhimu wa kujiandaa sasa kwa ajili ya mahusiano ya ndoa ya wakati ujao?
Wiki iliyopita, washiriki wa darasa au akidi walipata fursa ya kusoma mafundisho ya Mwokozi juu ya ndoa katika Mathayo 19:4–6. Ili kujiandaa kufundisha, jifunze mistari hii, pamoja na ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Kwa Sifa za Wale Wanaokoa” (Liahona, Mei 2016, 77–80) au jumbe zingine zilizopendekezwa katika muhtasari huu.
Jifunzeni Pamoja
Ndoa inaweza kuwa haipo katika akili za vijana wengi. Hata hivyo, kitu muhimu sana kinachohitaji maandlizi ya makini. Labda ungeweza kuwaalika vijana kuwaza kwamba wanapiga magoti katika madhabahu hekaluni kufungwa na mfunganishaji anawashauri wajifunze Mathayo 19:4–6. Je, ni kweli gani tunazipata katika mistari hii ambazo zingeweza kuwasaidia wanandoa wapya? Ni kwa jinsi gani mume na mkewe wanakuwa “wamoja”? Ni kwa jinsi gani Mwokozi anasaidia? Shughuli kama hizi zinaweza kusaidia darasa au akidi kuelewa jinsi ya kupata umoja ndani ya ndoa.
-
Adamu na Hawa wanatoa mfano mzuri wa mume na mke wakifanya kazi kwa umoja. Ungeweza kuonyesha picha ya wao (ona Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], na, 5) na kuomba darasa au akidi kusoma Musa 5:1–12, wakitafuta njia ambazo kwazo Adamu na Hawa walifanya kazi kwa umoja. Je, walifanya nini ili kwamba Mungu aweze kubariki uhusiano wao? Ili kuwasaidia vijana kujifunza zaidi kuhusu umoja ndani ya ndoa, wangeweza kujifunza maandiko katika “Nyenzo Saidizi.”
-
Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha kwamba katika jamii nyingi siku hizi, “kila kitu kinaonekana cha kutupwa.” Lakini mtazamo huu lazima usitumike katika ndoa zetu na familia; badala yake tunapaswa “kuweka juhudi zetu bora katika kuzihifadhi na kuzirutubisha” (“Kwa Sifa za Wale Wanaookoa,” 77). Ili kuonyesha kipengele hiki, ungewaalika vijana kufikiria juu ya kitu fulani walichobadilisha karibuni ambacho kilikuwa kimevunjika, kuwa kuukuu, au kupitwa na wakati. Kwa nini ndoa ni tofauti na vyombo vya kubadilishwa kama hivi? Darasa au akidi ingeweza kisha kusoma sehemu ya ujumbe wa Rais Uchtdorf wenye kichwa “Kuokoa Ndoa Zetu” na kushiriki njia waume na wake wanaweza kufanya kazi pamoja na wakiwa na Mwokozi akiimarisha ndoa zao. Tunaweza kufanya nini sasa kujiandaa kwa ajili ya ndoa imara na zilizo na umoja?
-
Fikiria kuandika Umoja katika Ndoa ubaoni na kuwaalika vijana kushiriki orodha ya vitu wake na waume wanaweza kufanya ili kuwa wamoja. Kisha waombe wapekue “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist.org) kwa ajili ya mawazo wanayoweza kuongeza katika orodha zao. Ni sifa gani washiriki wa darasa lako au akidi yao wanaona katika kila mmoja au katika wanandoa wanawajua ambazo ni muhimu kwa ajili ya umoja katika ndoa? Kwa nini ni muhimu kukuza na kutumia kauni hizi katika mahusiano yetu sasa? Video katika “Nyenzo Saidizi” zinatoa baadhi ya mifano ya sifa hizi katika matendo.
-
Kama washiriki wa darasa lako au akidi yako wana maswali au shaka kuhusu talaka, fikiria kupitia tena pamoja sehemu ya ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Talaka” (Liahona, Mei 2007, 70–73).
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
1 Wakorintho 11:11; Mafundisho na Maagano 42:22; 49:1–17; Musa 3:18, 21–24 (Umuhimu wa umoja katika ndoa)
-
“Renaissance of Marriage,” “Let Us Be Men,” “Expressions of Love” (videos), ChurchofJesusChrist.org