Agano Jipya 2023
Mei 28. Je, Ninaweza Kufanya Nini Sasa Kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi? Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21


“Mei 28. Je, Ninaweza Kufanya Nini Sasa Kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi? Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Mei 28. Je, Ninaweza Kufanya Nini Sasa Kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
Anakuja Tena Kuongoza na Kutawala, na Mary R.

Anakuja Tena Kuongoza na Kutawala, na Mary R.

Mei 28

Je, Ninaweza Kufanya Nini Sasa Kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi?

Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Tulijadili nini wakati uliopita, na ni mialiko gani au kazi gani zilitolewa? Tumefanya nini kushughulikia mialiko hiyo au kazi hizo?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Tunaweza kufanya nini au kusema nini ili kuwafikia wale wanaoweza kuwa wanahisi kuwa wapweke au wako mbali na Baba wa Mbinguni?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Yesu Kristo?

  • Unganisha familia milele. Ni mawazo gani tunaweza kushiriki mmoja na mwingine kuimarisha familia zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Ni kwa jinsi gani vijana wanahisi kuhusu kuishi katika siku za mwisho kabla ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo? Ni kweli kwamba hizi ni nyakati hatari, zilizo na dhiki, uovu na maangamizi. Lakini wakati Mwokozi alielezea siku zetu kwa wafuasi Wake karibia mwisho wa maisha Yake duniani, Yeye alitupatia tumaini. Ingawa tunatambua giza linalokuja, Yeye aliahidi kwamba nuru Yake “ingeufunika ulimwengu wote” atakaporudi tena (ona Joseph Smith—Mathayo 1:22–26; ona pia Mafundisho na Maagano 45:34–38).

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia vijana kuelewa vyema baraka na fursa za kuishi katika siku za mwisho? Je, ninaweza kufanya nini ili kuwatia motisha kujiandaa wao wenyewe na ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi? Kama nyongeza ya kujifunza vifungu vya maandiko vya wiki hii, fikiria kupitia tena nyenzo chache zilizoorodheshwa katika “Ujio wa Pili wa Yesu Kristo” katika Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org).

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia vijana kupitia tena kile walichosoma katika maandiko wiki hii, ungeweza kuandika vichwa hivi ubaoni: Unabii wa Huzuni and Matangazo ya Utukufu (ona Russell M. Nelson, “Kubiliana na Siku Zijazo kwa Imani,” Liahona, Nov. 2020, 73–76). Kisha kila mtu angeweza kupitia tena Joseph Smith—Mathayo 1:22–37 na kuorodhesha vitu vya “huzuni” na “utukufu” ambavyo vitatokea kabla Mwokozi kurudi tena. Kwa nini ni muhimu kwetu sisi kutambua matukio haya? Ili kuwasaida vijana kujifunza zaidi jinsi ya kujiandaa kwa ujio wa Mwokozi, fikiria shughuli zifuatazo au moja yako mwenyewe.

  • Maandiko katika “Nyenzo Saidizi” yanaweza kuwasaidia vijana kuelewa jinsi Baba wa Mbinguni anaandaa njia ya Ujio wa Pili wa Mwanawe. Fikiria kuandika matukio yaliyoelezewa katika maandiko ubaoni na kumwomba kila mtu kusoma mojawapo ya vifungu vya maandiko. Kila mtu angeweza kuoanisha kifungu na tukio ubaoni na kujadili kifungu hicho na darasa. Ni nini matukio haya yanapendekeza kuhusu wajibu wetu kuhusu kuandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi? Je, tumepata mwongozo kufanya nini kama darasa au akidi?

  • Rais Russell M. Nelson ameshauri: “Je, tunapaswa kushughulikia vipi unabii wenye huzuni na matamko matukufu juu ya siku zetu? Bwana alituambia jinsi ya kufanya hilo kwa hakikisho rahisi lakini la kushangaza: ‘Kama mmejitayarisha hamtaogopa’ [Mafundisho na Maagano]” (“Kabiliana na Siku Zijazo kwa Imani,” 74). Ili kuwasaidia vijana kuwa wamejiandaa zaidi kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi, fikiria kumuomba kila mmoja wao kusoma mojawapo ya kanuni tatu za maandalizi Rais Nelson alishiriki katika ujumbe wake. Waalike wao kushiriki kile wanachojifunza. Ni nini tuhamasisha kufanya kutenda juu ya ushauri wa Rais Nelson?

  • Hapo mwanzoni mwa ujumbe wake wenye kichwa “Kujiandaa kwa ajili ya Kurudi kwa Bwana,” Mzee D. Todd Christofferson alielezea vile ulimwengu utakuwa baada ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo (Liahona, Mei 2019, 81–84). Waalike vijana kupitia tena maelezo yake na kufananisha na vile ulimwengu ulivyo sasa. Wangeweza kujadili kile tunachoweza kufanya sasa ili kuwa tayari kuishi katika aina ya ulimwengu ambao Mzee Christofferson aliuelezea. ( aya nne za ujumbe wake kuanzia na “Kwanza, muhimu katika kurudi kwa Bwana” ingekuwa msaada.) Ni kwa jinsi gani Kanisa la Mwokozi linatusaidia sisi kujiandaa kwa ajili ya Ujio Wake wa Pili? Mzee Christofferson aliorodhesha njia tatu ambazo Kanisa ni la “kipekee na lililopewa nguvu na dhamana kukamilisha maandalizi muhimu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana.” Washiriki wa darasa wangeweza kutambua na kujadili vitu hivi.

Picha
msichana akijifunza

Kama tumejiandaa, hatutakuwa na haja ya kuogopa matukio yanayoelekea kwenye Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Wafundishe wanafunzi kwamba mara nyingine Roho atawafundisha vitu wakati wa majadiliano ya darasa ambavyo havikuzungumziwa kwa sauti.

Chapisha