2010–2019
Kuwapenda Wengine na Kuishi kwa Utofauti
Oktoba 2014


15:12

Kuwapenda Wengine na Kuishi kwa Utofauti

Kama wafuasi wa Kristo tunapaswa kuishi kwa imani na wengine ambao hawashiriki viwango vyetu au kukubali mafundisho ambayo ndiyo msingi wayo.

I.

Katika siku za kuhitimisha huduma yake hapa duniani, Yesu aliwapa wanafunzi wake kile alichoita “amri mpya” (Yohana 13:34). Alirudia mara tatu,ile amri ilikuwa rahisi lakini ngumu; “Mpendane, kama mimi nilivyowapenda nyinyi” (Yohana 15:12; ona pia mstari wa 17). Fundisho la kupendana limekuwa fundisho muhimu la huduma ya Mwokozi. Amri kuu ya pili ilikuwa “Mpende jirani yako kama nafsi yako” (Mathayo 22:39). Yesu hata hivyo alifundisha, “Wapendeni Maadui zenu” (Mathayo 5:44) Lakini amri ya kupenda wengine kama alivyo lipenda Kundi Lake ilikuwa kwa wafuasi Wake---na ni kwetu sisi---changamoto ambayo ilikuwa ya kipekee.” Kwa kweli, Rais Thomas S. Monson alitufundisha Aprili iliyopita. “Upendo ni sehemu muhimu sana ya injili, na Yesu Kristo ni Mfano wetu. Maisha Yake yalikuwa ni urithi wa upendo.”1

Kwa nini ni vigumu sana kuwa na upendo kama wa Kristo kwa mtu mwingine? Ni vigumu kwa sababu ni lazima tuishi miongoni mwa hao ambao hawashiriki imani yetu na maadili na wajibu wa agano. Katika sala Yake kuu kwa ajili ya wafuasi wake, aliyoitoa punde tu kabla ya Usulibio Wake, Yesu aliomba kwa ajili ya wafuasi Wake: “Nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia, kwa sababu wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu” (Yohana 17:14). Kisha, kwa Baba alimsihi, “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu” (mstari wa 15).

Tunatakiwa tuishi katika ulimwengu lakini tusiwe wa ulimwengu. Ni lazima tuishi katika ulimwengu kwa sababu, kama Yesu alivyofundisha katika fumbo, ufalme Wake ni “kama hamira,” ambayo kazi yake ni kuinua umati kwa athari zake (ona Luka 13:21; Mathayo 13:33; ona pia 1 Wakorintho 5:6–8). Wafuasi wake hawawezi kufanya hivyo kama tu watajihusisha tu pamoja na hao wanaoshiriki imani zao na desturi zao. Lakini Mwokozi pia alifundisha kwamba kama tunampenda, tutatii amri Zake (ona Yohana 14:15).

II.

Injili ina mafundisho mengi kuhusu kutii amri wakati tukiishi miongoni mwa watu wenye imani na desturi tofauti. Mafundisho kuhusu mabishano ni muhimu sana. Wakati Kristo aliyefufuka alipowaona Wanefi wakibishana juu ya jinsi ya ubatizo, Alitoa maelekezo ya wazi juu ya jinsi ibada hii inatakiwa ifanywe.Kisha alifundisha kanuni hii kubwa:

“Na hakutakuwa na ugomvi miongoni mwenu, kama vile ilivyo hapa sasa; wala hakutakuwa na ugomvi miongoni mwenu kuhusu nukta za mafundisho yangu, kama vile ilivyokuwa.

“Kwani amin, amin, nawaambia, yule ambaye ana roho ya ubishi siye wangu, lakini ni wa ibilisi, ambaye ni baba wa ubishi, na huchochea mioyo ya watu kubishana na hasira mmoja kwa mwingine.

“Tazama, hili ... ndilo fundisho langu, kwamba vitu kama hivi viondolewe mbali” (3 Nefi 11:28–30; mkazo umeongezwa).

Mwokozi hakuwekea kikomo onyo Lake dhidi ya ubishi kwa hao ambao hawakuwa wanatii amri kuhusu ubatizo. Alikataza ubishi kwa yeyote. Hata hao wanaotii amri wasichochee mioyo ya watu kubishana kwa hasira. “Baba wa ubishi” ni ibilisi; Mwokozi ni Mwana Mfalme wa Amani.

Hali kadhalika, Bibilia inafundisha kwamba “Wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu (Mithali 29:8). Mitume wa mwanzo walifundisha kwamba hatuna budi “Kufuata mambo ya amani” (Warumi 14:19) na “[sema] ukweli katika upendo” (Waefeso 4:15), “Kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu” (Yakobo 1:20). Katika ufunuo wa kisasa Bwana aliamuru kwamba habari njema ya injili ya urejesho lazima itangazwe “kuonya kila mtu kwa jirani yake, katika upole na unyenyekevu (M&M 38:41), “Na utafanya kwa unyenyekevu wote, … usitukane dhidi ya wenye kutukana” (M&M 19:30).

III.

Hata kama tunataka kuwa wapole na kuepuka ubishi, tusikubali kuhatarisha au kudhoofisha wajibu wetu kwa ukweli tunaoujua. Tusikubali kusalimisha msimamo wetu au maadili yetu. Injili ya Yesu Kristo na maagano tuliyofanya yametuweka kwenye wajibu usioepukika kama wapiganaji katika mapambano ya milele kati ya ukweli na makosa. Hakuna sehemu isiyopendelea upande wowote katika malumbano hayo.

Mwokozi alionyesha njia wakati maadui Zake walipomkabili na mwanamke ambaye “amefumaniwa alipokuwa akizini” (Yohana 8:4). Walipoaibika kwa unafiki wao, washitaki waliondoka nakumwachaYesu peke yake na mwanamke. Alimtendea kwa huruma kwa kukataa kumshutumu kwa wakati ule. Lakini pia kiuthabiti alimwelekeza “kutotenda dhambi tena” (Yohana 8:11). Upendo Wake mkarimu unahitajika, lakini mfuasi wa Kristo---kama vile alivyo Bwana---atakuwa imara katika ukweli.

IV.

Kama Mwokozi, wafuasi wake wakati mwingine wanakabiliwa na tabia ya dhambi, na leo wakati mwingine wanaitwa “walokole” au “watu wenye msimamo mkali.” Viwango vingi na desturi nyingi za kilimwengu zitoa changamoto kama hizo kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kawaida katika siku hizi ni wimbi lenye nguvu ambalo linahalalisha ndoa ya jinsia moja katika majimbo mengi katika Marekani, Kanada, na nchi nyingi katika ulimwengu. Pia tunaishi miongoni mwa baadhi ambao hawaamini katika ndoa kabisa. Baadhi hawaamini katika kupata watoto. Baadhi wanapinga vizuizi vyovyote juu ya ponografia au madawa ya hatari. Mfano mwingine---inayofahamika kwa waumini wengi---ni changamoto ya kuishi pamoja na mume au mwenzi asiyemuumini au mwanafamilia au kujihusisha na wafanyakazi wenzi wasioamini au wengine.

Katika sehemu zilizowekwa wakfu, kama mahekalu, nyumba za ibada, nyumba zetu wenyewe, hatuna budi kufundisha ukweli na amri kiuwazi na kikamilifu kama tunavyoelewa kutoka mpango wa wokovu uliofunuliwa katika injili ya urejesho. Haki yetu ya kufanya hivyo inalindwa na dhamana ya kikatiba ya uhuru wa kusema na dini, vile vile na faragha ambayo inaheshimiwa hata katika nchi zisizokuwa na dhamana ya katiba rasmi.

Katika umma, watu wa dini wanachosema na kufanya kinahusisha kufikiria mengine. Matumizi huru ya dini hutumia matumizi mengi ya umma, lakini yanapaswa kutii stahili ya lazima ili kupatia nafasi utekelezwaji wa mengine. Sheria zinaweza kuzuia tabia ambayo kwa kawaida inatambulika kama kosa au isiyokubalika, kama unyanyasaji wa kijinsia na vurugu au tabia ya kigaidi, hata kama imefanywa na mtu mwenye siasa kali katika jina la dini. Tabia za kusikitisha kidogo, hata kama hazikubaliki kwa baadhi ya waumini, kiurahisi inatakiwa kuvumiliwa kama imehalalishwa na kile nabii wa kitabu cha Mormoni alikiita “sauti ya watu” (Mosia 29:26).

Juu ya mada ya mahubiri kwa umma, tunatamani usikivu mkubwa sana kwa mafundisho ya injili kumpenda jirani yetu na kuepuka mabishano. Wafuasi wa Kristo wanatakiwa wawe mifano ya upole, tuwapende watu wote, tuwe wasikilizaji wazuri, na kuonyesha kujishughulisha kwa imani zao za kikweli. Ingawa tunaweza tusikubali, tusiwe wachokozi. Kauli zetu na mawasiliano juu ya mada zenye ubishani zisije zikasababisha ubishani, tuwe wenye busara wakati wa kuelezea na kufuatilia kauli zetu na katika kutumia ushawishi wetu. Kwa kufanya hivyo, tunaomba kwamba wengine wasichukizwe na imani za kweli za dini yetu na uhuru wa kutumia dini yetu. Tunawatia moyo wote kati yetu kutekeleza Sheria Muhimu ya Mwokozi. “Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo” (Mathayo 7:12).

Wakati misimamo yetu isiposhinda, hatuna budi kukubali matokeo yasiyofaa kwa mtazamo mzuri na tutende kiuungwana kwa maadui zetu. Bila kujali nini kinatokea, hatuna budi kuwa watu wenye urafiki juu ya wote, tukikataa mateso ya aina yeyote, ikijumuisha mateso kwa misingi ya kimbari, kimaadili, kidini, imani au kutoamini, na tofauti katika maelekezo ya mazingira ya kijinsia.

V.

Nimezungumza juu ya kanuni za kawaida. Sasa nitazungumza juu ya jinsi kanuni hizo zinavyotakiwa kutumika katika hali ya familia tofauti ambazo mafundisho ya Mwokozi yanatakiwa yafuatwe kwa uaminifu zaidi.

Naanza na kile watoto wetu wadogo wanajifunza wakati wanapocheza. Mara nyingi wasio-Wamormoni hapa Utah wamekuwa wameudhiwa na kutengwa na baadhi ya washiriki wetu ambao hawawaruhusu watoto wao kuwa marafiki wa watoto wa imani zingine. Kwa hakika tunaweza kuwafundisha watoto wetu weledi na matarajio ya tabia bila kuwafanya wajiweke mbali au kuonyesha kutoheshimu yeyote ambaye ni tofauti.

Walimu wengi katika Kanisa na shule wamesikitishwa kwa njia baadhi ya vijana, pamoja na vijana wa WSW, wanavyotendeana. Sheria ya kupendana hakika ni pamoja na upendo na kuheshimu dini zingine na pia kwa jamii tofauti, utamaduni, au ngazi za kiuchumi. Tunatoa changamoto kwa vijana wote kukwepa kushutumu, matusi au lugha na utendaji ambao kwa makusudi unawaumiza wengine. Hivi vyote vinakiuka amri ya Mwokozi ya kupendana.

Mwokozi alifundisha kwamba ubishi ni chombo cha ibilisi. Hiyo kwa hakika anafundisha dhidi ya baadhi ya desturi za lugha na utekelwezaji wa siasa. Kuishi na utofauti wa sera ni muhimu katika siasa, lakini utofauti wa sera hauhitaji kuhusisha mashabulizi kibinafsi ambayo yanazuia njia ya serikali na kuadhibu wahusika. Sisi sote lazima tuepuke mawasiliano ya chuki na kufanya ustaarabu kwa utofauti wa maoni.

Mazingira muhimu mno ya kupinga ubishi na kutekeleza heshima kwa utofauti upo katika nyumba zetu na mahusiano ya kifamilia. Tofauti haziepukiki---baadhi ya tofauti zitakuwa ndogo na baadhi zitakuwa kubwa. Kuhusu tofauti kubwa, chukuwa kwamba mwanafamilia ana mahusiano ya kinyumba. Hii inaleta athari mbili muhimu kwenye mgogoro---upendo wetu kwa mwanafamilia na ahadi yetu kwenye amri. Kufuatia mfano wa Mwokozi, tunaweza kuonyesha upendo wa huruma na bado tukawa imara katika ukweli kwa kupinga vitendo ambavyo vinaleta au vinaonekana kukubali kile tunachojua kuwa ni makosa.

Ninahitimishakwa mfano mwingine wa uhusiano wa kifamilia. Kwenye mkutano mkuu wa kigingi katika magharibi ya kati takribani miaka 10 iliyopita, nilikutana na dada ambaye aliniambia kwamba mumewe ambaye si mshiriki amekuwa akifuatana naye kanisani kwa miaka 12 lakini kamwe hajajiunga na Kanisa. Anatakiwa afanye nini? aliuliza. Nilimshauri aendelee kufanya mambo yote ya haki na avute subira na upole kwa mume wake.

Takribani mwezi mmoja baadaye aliniandikia kama ifuatavyo: “Vema, nilifikiri kwamba miaka 12 ilithibitisha jinsi nilivyokuwa na subira, lakini sikujua kama nilikuwa na huruma sana kuhusu hiyo. Kwa hivyo, nilitekeleza kwa bidii halisi zaidi ya mwezi mmoja,na akabatizwa.”

Ukarimu una nguvu,hususani katika mazingira ya familia. Barua yake iliendelea, “Najaribu hata kuwa na huruma zaidi sasa kwa sababu tunashugulikia kuunganishwa hekaluni mwaka huu!”

Miaka sita baadaye aliniandikia barua ingine: Mume wangu [ndiyo] aliitwa na kutengwa kuwa askofu [wa kata yetu].”2

VI.

Katika mahusiano mengi sana na mambo katika maisha, lazima tujumuike pamoja na watu ambao ni tofauti na sisi. Ambako uzima, nje ya tofauti hizi haitakiwi kukataliwa au kuachwa, lakini wafuasi wa Kristo wanatakiwa wajifunze kuishi kwa amani pamoja na wengine ambao hawashiriki maadili yao au kukubali mafundisho ambayo ndiyo msingi. Mpango wa wokovu wa Baba, ambao tunaujua kwa ufunuo wa kinabii, unatuweka katika mambo ya kidunia ambako tunatakiwa kutii amri zake. Hiyo ni pamoja na kuwapenda majirani zetu wa tamaduni na imani tofauti kwa njia ambayo Ametupenda sisi. Kama nabii wa Kitabu cha Mormoni alivyofundisha, lazima tusonge mbele tukiwa na upendo kwa Mungu na kwa watu wote” (2 Nefi 31:20).

Kama ugumu ulivyo kuishi katika machafuko yaliyotuzunguka, amri ya Mwokozi wetu kupendana kama anavyotupenda huenda ni changamoto yetu kubwa. Mimi naomba kwamba tuweze kuelewa hili na tutafute kuliishi katika mahusiano yetu yote na utendaji, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “Love—the Essence of the Gospel,” Ensign au Liahona, May 2014, 91.

  2. Barua kwa Dallin H. Oaks, Jan. 23, 2006, na Oct. 30, 2012.