Ishi Kulingana na Maneno ya Manabii
Kuwa na uwiano na madhumuni ya matakatifu ya mbinguni, tunamkubali nabii na kuchagua kuishi kilingana na maneno yake.
Baba Yetu wa Mbinguni anawapenda watoto wake wote na anatamani kwamba wajue na waelewe mpango Wake wa furaha. Kwa hivyo, huwaita manabii, wale ambao wamesimikwa na nguvu na mamlaka ya kutenda katika jina la Mungu kwa ajili ya wokovu wa watoto Wake. Ni wajumbe wa haki, mashahidi wa Yesu Kristo na nguvu isiyo na kikomo ya Upatanisho Wake. Wanashikilia funguo za ufalme wa Mungu duniani na wamepewa mamlaka ya kufanya ibada za kuokoa.
Katika Kanisa la kweli la Bwana, “hakuna mwingine ila mmoja tu duniani kwa wakati mmoja ambaye kwake yeye nguvu na funguo za ukuhani zitasimikwa.”1 Tunamkubali Rais Thomas S. Monson kama nabii, mwonaji, na mfunuaji. Anafunua neno la Bwana kutuongoza na kulisimamia Kanisa lote. Kama Rais J. Reuben Clark Jr. alivyoelezea, “Rais wa Kanisa … yeye peke yake ana haki ya kupokea funuo za Kanisa.”2
Kuhusu nabii anayeishi, Bwana ameamuru watu wa Kanisa Lake:
“Nawe utayaangalia maneno yake yote na amri ambazo atazitoa kwenu kadiri atakavyozipokea, mkitembea katika utakatifu mbele zangu;
“Kwani neno lake mtalipokea, kama vile linatoka kinywani mwangu, katika uvumilivu wote na imani yote.
“Kwani kwa kufanya mambo haya milango ya jahanamu haitawashinda.”3
Ili kuwiana na mpango mtukufu wa mbinguni, tunamkubali nabii na tunachagua kuishi kulingana na maneno yake.”
Pia tunawakubali washauri wa Rais Monson na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuaji. “Wana haki, nguvu, na mamlaka ya kutangaza mawazo na mapenzi ya [Bwana] … , kulingana na … Rais wa Kanisa.”4 Wanaongea katika jina la Kristo. Wanatoa unabii katika Jina la Kristo. Wanafanya mambo yote katika jina la Yesu Kristo. Katika maneno yao tunasikia sauti ya Bwana na tunahisi upendo wa Mwokozi. “Na lolote watakalolisema wakati wanaongozwa na Roho Mtakatifu litakuwa andiko … na ni uweza wa Mungu kwa wokovu.”5 Bwana mwenyewe ameongea, “Iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote in sawa.”6
Tunashukuru kwa kanisa “lililojengwa kwenye msingi wa manabii na mitume, Yesu Kristo mwenyewe akiwa ndio jiwe kuu la pembeni.”7 Nyumba ya Bwana ni nyumba ya utaratibu, na tusidanganyike kuhusu sehemu ya kutafuta majibu ya maswali yetu au hakuna haja ya kutokuwa na uhakika kuhusu sauti ipi tuifuate. Hatuhitaji “kutupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu.”8 Mungu anafunua maneno yake kupitia watumishi wake waliosimikwa, “kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe: hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na ufahamu wa Mwana wa Mungu.”9 Tunapochagua kuishi kulingana na maneno ya manabii, tuko kwenye njia ya agano ambayo inatuongoza kwenye ukamilifu wa milele.
Kutoka kwa mama asiye kuwa na mume anayepata shida kuishi nyakati za njaa, tunajifunza kile inamaanisha kumuunga mkono nabii. Bwana amemuagiza nabii Eliya aende Zarepati ambako angemkuta mjane ambaye Mungu alimwamuru kumkidhi. Eliya alipokuwa akikaribia kwenye mji, alimwona akikusanya kuni. Akamwita, “Niletee nami, nakuomba, maji kidogo katika chombo, ili niweze kunywa.”10
“Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, niletee nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako.
“Naye akasema, Kama Bwana Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.”
Eliya alijibu, “Usiogope, nenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza, mkate mdogo ukaniletee, kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.”11
Fikiria kwa dakika ugumu wa kile nabii alikuwa anakiomba kwa mama huyu mwenye njaa kukifanya. Bila shaka, Mungu mwenyewe angeweza kutoa chakula kwa watumishi Wake waaminifu. Lakini akitenda katika jina la Bwana, Eliya anatenda kama alivyoelekezwa, ambayo ilikuwa ni kumwomba mtoto mpendwa wa Mungu kujitolea kile alichokuwa nacho—kumsaidia nabii.
Lakini Eliya aliahidi pia baraka kwa ajili ya utiifu: “Kwa kuwa Bwana Mungu wa Israeli asema hivi, lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha.”12 Bwana alimpa mjane fursa ya kuchagua kuamini na kutii maneno ya nabii.
Katika dunia inayotishiwa na kukosekana kwa haki na njaa ya kiroho, tumeamriwa kumkubali nabii. Tunaposikiliza, kutetea, na kushikilia maneno ya kinabii, tunashuhudia kwamba tuna imani kujisalimisha kinyenyekevu kwa mapenzi yake, hekima, na wakati wa Bwana.
Tunaposikiliza neno la kinabii hata kama litaonekana kutokuwa ya mantiki, si wakati wake bora, ua ni gumu kulifanya. Kulingana na viwango vya dunia, kumfuata nabii kunaweza kuwa haitambuliki, siyo sahihi kisiasa, au kutokubalika kijamii. Lakini kumfuata nabii ni sahihi mara zote. “Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.” 13 “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe.”14
Bwana anawaheshimu na kuwapendelea wale ambao wanaotii mwongozo wa kinabii. Kwa mjane wa Zarefati utii kwa Eliya uliokoa maisha yake na mwishowe maisha ya mtoto wake wa kiume. Kama nabii alivyoahidi, “yeye, na mtoto wake na nyumba yake, walikula kwa siku nyingi…kulingana na maneno ya Bwana, yaliyonenwa na Eliya.”15
“Bwana atawalisha wale wanaomwamini.”16 Maneno ya manabii ni kama mana katika mioyo yetu. Tunapokula, tunabarikiwa, tunalindwa, na tunatunzwa kimwili na kiroho. Tunaposherekea maneno yao, tunajifunza jinsi ya kuja kwa Kristo na kuishi.
Mzee Bruce R. McConkie aliandika kwamba, kupitia manabii, “Bwana hufunua kweli za wokovu; … wokovu ambao umo ndani ya Kristo; na anatambua … njia inayotuelekeza kwenye uzima wa milele. … Katika kila wakati Bwana anawapa watu wake mwelekeo wanaouhitaji katika wakati wa shida na hatari. Na hakika siku za mbeleni kutakuwa na nyakati hakuna chochote bali hekima ya Mungu, ishukayo kutoka mbinguni na kutoka katika vinywa vya manabii, itaweza kuokoa watu wake.”17
Kwangu mimi, maneno ya manabii yaliyofundishwa na mwalimu wangu wa Laurel yalinipa uelewa wa jinsi gani agano la mahusiano ya ndoa linatakiwa kuwa. Maneno ya manabii yalinipa imani na tumaini kwamba ningeweza kujitayarisha na kupata nyumba yenye furaha. Kujifunza maneno ya manabii kila mara, yote ya kale na ya sasa, yalinisaidia wakati wa nyakati nguvu na mara nyingi miaka inayochosha ya kuwapata, kuwafundisha, na kuwalea watoto saba. Maneno ya manabii katika maandiko na yanavyofundishwa katika majukwaa ni maneno ya kufariji, upendo, nguvu, na furaha nzuri inayotugusa sote.
Tunapoyatii maneno ya manabii, tunajenga nyumba zetu na maisha yetu kwenye msingi wa kweli wa milele. “mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, … kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, ndio, mishale yake kimbungani, wakati mvua yake ya mawe na dhoruba kali itapigaa juu yenu, hautakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye … taabu na msiba usioisha.”18
Tuna chaguo. Tunaweza kuchagua kupuuza, kubeza, kutotilia maanani, au kukaidi maneno ya Kristo yaliyonenwa na watumishi wake waliosimikwa. Lakini Mwokozi ametufundisha kwamba wale wanaofanya hivyo wataondolewa kutoka kwenye watu wake wa ahadi.19
Tunaposoma na kujifunza maneno ya kinabii kwa maombi tukiwa na imani katika Kristo, na kusudi thabiti, Roho Mtakatifu atanena ukweli katika akili na mioyo yetu. Natumaini kwamba tutafungua masikio yetu na kusikia, mioyo yetu kuelewa, na akili zetu kwamba maajabu ya Mungu yaweze kufunguliwa katika uono wetu.20
Ninashuhudia kwamba Joseph Smith alikuwa, na ni nabii aliyeitwa na Mungu kurejesha injili ya Yesu Kristo na ukuhani Wake duniani. Na nashuhudia kwamba katika Rais Monson, tunaongozwa na nabii wa kweli wa Mungu leo. Na tuchague kusimama na manabii na kuishi kulingana na maneno mpaka tutakapounganika katika imani, kutakaswa katika Kristo, na kujazwa na ufahamu wa Mwana wa Mungu, katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.