2010–2019
Kutayarishwa kwa Njia Ambayo Kamwe Haijajulikana
Oktoba 2014


10:11

Kutayarishwa kwa Njia Ambayo Kamwe Haijajulikana

Na tujitayarishe kupokea maagizo ya kuokoa kwa ustahiki tone kwa tone na kuweka maagano husika kwa moyo mkunjufu.

Wakati binti yetu mdogo aliporudi nyumbani baada ya siku yake ya kwanza shuleni, nilimuuliza. “Mambo yameenda vipi?

Alijibu, “Vizuri.”

Asubuhi iliyofuata, hata hivyo, wakati nilipomwamsha aende shuleni alikunja mikono yake na kwa ukakamavu kusema, “Tayari nilikuwa nimeshaenda shuleni!” Kwa kweli nilikuwa sijamtayarisha au kumwelezea kwamba kuenda shule lilikuwa jambo la siku moja bali kwamba alitarajiwa kuenda shule siku tano kwa wiki kwa miaka mingi, mingi sana.

Tunapoangalia kanuni ya kujitayarisha, fikiria pamoja nami maandhari yafuatayo. Umekaa katika chumba cha selestia cha hekaluni na unawaona mabibi harusi na mabwana harusi wakikaribishwa ndani kwa utulivu wakitoka wanapongojea kuozwa kwa nyakati na milele yote. Bibi harusi anaingia katika chumba cha selestia, mkono kwa mkono na mpenzi wake. Amevalia vazi la kawaida lakini vazi maridadi la hekaluni na akiwa tuli, mwenye amani, tabasamu changamfu usoni mwake. Amejipamba vizuri siyo kuvuta nadhari sana. Anaketi chini, anatazama mazingira, na kisha ghafla anabubikwa na mhemko. Inaonekana kama machozi yake yanakuja kwa sababu ya staha na uchaji ambao yeye anao kwa yote mahali ambapo alipo na agizo takatifu linalomngojea na kipenzi cha moyo wake. Mwenendo wake unaonekana kusema, “Nina shukrani jinsi gani kuwa katika nyumba ya Bwana leo, tayari kuanza safari ya milele na mwenzi mpendwa wa milele” Anaonekana kuwa tayari kwa zaidi ya tukio tu.

Mjukuu wetu mpendwa wa kike majuzi aliniachia barua kwenye mto wangu ambayo sehemu yake inasema: “Kitu kimoja ambacho kimenigusa ninapoingia katika hekalu ni roho ya amani, upendo ambayo inadumu hapo. … Watu wanaweza kwenda hekaluni kupokea maongozi.” 1 Yeye yu sahihi. Tunaweza kupokea maongozi na ufunuo katika hekalu---na pia uwezo wa kukabiliana na dhiki za maisha. Kile anachojifunza kuhusu hekalu anashiriki kila mara katika kuchukua majina ya familia yake mwenyewe ili kufanya ubatizo na uthibitisho kitamtayarisha kwa maagizo ya hekalu ya ziada, maagano, na baraka, zote kwake mwenyewe na wale waliopo kwenye ule upande mwingine wa pazia.

Mzee Nelson  M. Nelson alifunza, “Kwa vile mahekalu yametayarishwa kwa watu, watu wanahitaji kujitayarisha wenyewe kwa ajili ya hekalu.”2

Ninaposoma tena kuhusu Kapteni Moroni katika Kitabu cha Mormoni, ninakumbushwa kwamba mojawapo wa mafanikio makuu ya Moroni ilikuwa ni matayarisho ya makini ya Wanefi kusimama imara dhidi ya jeshi lenye kutisha la Walamani. Aliwatayarisha watu wake vyema sana kwamba tunasoma: “Tazama, [Walamani] kwa mshangao wao mkuu, walikuwa [Wanefi] wamejitayarisha kwa ajili yao, kwa njia ambayo haijajulikana.” 3

Kisha kile, wamejitayarisha … kwa njia ambayo haijajulikana” kwa kweli kilivuta nadhari yangu.

Tunaweza kujitayarisha vipi kwa ajili ya baraka takatifu za hekaluni? Bwana alifunza, “Na tena, nitatoa kwenu utaratibu katika mambo yote.” 4 Acha tungalie utaratibu wa kimaandiko wa kutatusaidia kujitayarisha vyema. Matayarisho ya Moroni kwa ajili ya adui yalihitaji, bidii ya kila mara na uaminifu, na taratibu hii itahitaji sifa hii hii.

Kamwe sijapata kuonekana kuchoshwa na mithali maridadi Mwokozi alisimulia ya wanawali watano wenye busara na watano wapumbavu. Ingawa hii mithali inalenga kuwa tayari kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi wetu, sisi pia tunaweza kuilinganisha na kuwa tayari kwa baraka za hekalu, ambazo zinaweza kuwa kama karamu ya kiroho kwa wale ambao wamejitayarisha vyema.

Katika Mathayo 25 tunasoma:

“Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.

“Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. …

“[Wale ambao] wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

“Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.

“ Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

“Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.

“Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.

“Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.

“Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

“Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.

“Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.” 5

Mimi sidhanii kuna mtu yeyote, hasa miongoni mwa wale walio na mioyo ororo, ambaye hahisi huzuni kwa wale wasichana wapumbavu. Na baadhi yenu mnataka kusema kwa wasichana wengine, “Hamwezi kushiriki tu ili kila mtu aweze kuwa na furaha?” Lakini fikiria kuhusu jambo hili. Hii ni hadithi Mwokozi alisimulia, na Yeye ndiye mtu ambaye aliwaita watano wao “wenye busara” na watano wao “wapumbavu.”

Tunapofikiria mithali hii kama utaratibu wa matayarisho ya hekalu, fikiria maneno ya nabii wa siku za mwisho ambaye alisema kwamba “mafuta ya matayarisho ya kiroho hayawezi kugawa.” 6Rais Spencer  W. Kimball alisaidia kufafanua kwa nini wasichana watano “wenye busara” hawangweza kugawa mafuta katika taa zao na wale ambao walikuwa “wapumbavu” wakati alisema: “Mahudhurio ya mkutano wa sakramenti huongeza mafuta ya taa zetu, tone kwa tone katika miaka mingi. Kufunga, sala za familia, mafundisho ya nyumbani, uthibiti wa tama za kimwili, kuhubiri injili, kujifunza maandiko---kila kitendo cha kujitolea na utii ni tone linaongezwa kwenye akiba yetu. Vitendo vya ukarimu, malipo ya matoleo na zaka, mawazo na matendo mema, ,, haya, pia, yanachangia vyema kwenye mafuta ambayo kwayo tunaweza kujalizia taa zetu zinapopofifia usiku wa manane.” 7

Mnaweza kuona utaratibu wa utayari wa---tone kwa tone---ambao unaweza kutusaidia tunapofokiria jinsi tunaweza kuwa wenye bidii katika matayarisho yetu ya kupokea maagizo matakatifu kwetu wenyewe na wengine? Ni vitu gani vingine vidogo na rahisi tunaweza kufanya kuongezea matone ya mafuta yenye thamani kwenye taa zetu za matayarisho?

Tunajifunza kutoka kwa Mzee Richard G. Scott kwamba “ustahiki wa kibinafsi ni sharti muhimu ili kufurahia baraka za hekalu. … Mtu mstahiki amejengwa vyema kwa maisha ya uthabiti, chaguo sahihi ambazo kitovu chake ni mafundisho ya Bwana.” 8 Nalipenda neno uthabiti. Kuwa thabiti ni kuwa imara, mwaminifu, na wa kutegemewa. Ni maelezo bora jinsi gani ya kanuni ya ustahiki!

Tunakumbushwa katika Kamusi ya Biblia, “Nyumbani tu ndiyo panaweza kufananishwa na hekalu kwa utakatifu.” 9 Nyumba zetu au makazi yanaonyesha maelezeo haya? Msichana mpendwa katika kata yetu alikuja nyumbani kwetu majuzi. Tukijua kuwa kaka yake alikuwa amerudi kutoka misheni yake hivi majuzi, nilimuuliza vile ilivyokuwa kuwa naye nyumbani. Alisema ilikuwa vyema, lakini mara kwa mara angeomba kwamba sauti ya muziki kama ingeteremsha chini kidogo. Akasema, “Na hata haikuwa muziki mbaya!” Inaweza kustahili kwetu kujikagua wenyewe sasa na kila mara kuhakikisha nyumba zetu ni mahali tunaweza kujitayarisha kuhisi Roho. Tunapotayarisha nyumba zetu kuwa mahali ambapo Roho anakaribishwa, tutajitayarisha kuhisi zaidi “kuwa nyumbani” wakati tunapoingia katika nyumba ya Bwana.

Tunapojitayarisha wenyewe kuwa wastahiki kuingia katika hekalu na tu waaminifu kwa maagano ya hekalu, Bwana atamwaga “baraka za aina nyingi” 10 juu yetu. Rafiki yangu wa dhati Bonnie Oscarson majuzi aligeuza andiko juu chini wakati alisema, “Pale mengi yanayohitajika, mengi zaidi yatatolewa.” 11 Mimi nakubaliana naye kabisa! Kwa sababu tunakuja kwenye hekalu kupokea baraka za milele. Mzee Nelson alifunza: “Kwa sababu ni nyumba ya Bwana, viwango vya kuingia ndani vimewekwa Naye. Mtu huingia kama mgeni Wake. Kuwa na sifu ya hekalu ni fursa ya thamani kuu na ishara wazi ya utii kwa Mungu na manabii Wake.” 12

Wanariadha wa kimataifa na wanafunzi udaktari wa falsafa wa chuoni wanatumia masaa na siku nyingi, na wiki na miezi na hata miaka ya matayarisho. Matone ya kila siku ya matayarisho yanahitajika kutoka kwao ili wapate mafanikio ya juu. Vivyo hivyo, wale wanaotaka kuhitimu kuinuliwa katika ufalme wa selestia wanatarajiwa kuishi viwango vya juu vya utii ambavyo huja kutokana na kutimia sifa ya utii siku hadi siku na tone kwa tone.

Tunapoongezea mafuta kwa uthabiti na bidii, tone kwa tone, kwenye taa zetu za kiroho, tukifanya hivi vitu vidogo na rahisi, tunaweza kuwa na taa zetu “kutengenezwa na kuwaka” 13 kwa matayarisho ya kushangaza. Mume wangu, ambaye ni rais wa kigingi, majuzi alisema kwamba anaweza kwa kawaida kujua wakati mtu yu tayari na ni mstahiki kuingia katika hekalu, kwa sababu “wao wanaangaza chumba” wakati wanapoomba sifu ya hekalu.

Katika sala za kuweka wakfu za Hekalu la Kirtland, Nabii Joseph Smith alimwomba Bwana “na kwamba watu wote watakaoingia mlangoni mwa nyumba ya Bwana wapate kuhisi uwezo wako, ... na kwamba waweze kukua ndani yako, na kuupokea utimilifu wa Roho Mtakatifu, ... kujitayarisha kupokea kila jambo linalohitajika.” 14

Ni maombi yangu kwamba kwetu sisi, kuenda kwenye hekalu itakuwa zaidi ya tukio la mara moja tu. Na tuweze kujitayarisha kwa ustahiki kupokea maagizo ya kuokoa tone kwa tone na kuweka kwa moyo mkunjufu maagano husika. Tunapofanya hivyo, mimi najua tutahitimu kupokea baraka zilizoahidiwa za ujalivu wa Roho Mtakatifu na nguvu za Bwana katika nyumba zetu na katika maisha ya watu binafsi. Ni katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Barua ya kibinafsi kutoka kwa Aydia Kaylie Melo kwa Linda  K. Burton, Aug 31, 2014.

  2. Russell  M. Nelson, “Prepare for the Blessings of the Temple,” Ensign or Liahona, Oct. 2010, 41.

  3. Alma 49:8; mkazo umeongezewa, ona mistari 6–7.

  4. Mafundisho na Maagano 52:14.

  5. Mathayo 25:1–2, 4–11; Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 25:12 (katika Mathayo 25:12, tanbihi a).

  6. Marvin  J. Ashton, “A Time of Urgency,” Ensign, May 1974, 36.

  7. Spencer W. Kimball, Faith Precedes the Miracle (1972), 256.

  8. Richard G. Scott, “Receive the Temple Blessings,” Ensign, May 1999, 25; Liahona, July 1999, 29.

  9. Bible Dictionary, “Temple.”

  10. Mafundisho na Maagano 104:2.

  11. Bonnie L. Oscarson, “Greater Expectations” (Seminaries and Institutes of Religion satellite broadcast, Aug. 5, 2014); lds.org/broadcasts; ona piaLuka 12:48; Mafundisho na Maagano 82:3.

  12. Russell M. Nelson, “Personal Preparation for Temple Blessings,” Ensign, May 2001, 33; Liahona, July 2001, 38.

  13. Mafundisho na Maagano 33:17.

  14. Mafundisho na Maagano 109:13, 15.