2010–2019
Unatazama Upande Gani?
Oktoba 2014


10:59

Unatazama Upande Gani?

Kujaribu kuwafurahisha wengine kabla ya kumfurahisha Mungu ni kuigeuza amri kuu ya kwanza na ya pili.

“Unatazama njia gani?” Rais Boyd K. Packer alinishangaza kwa swali hili la mkanganyiko tulipokuwa tukisafiri pamoja kwenye safari yangu ya kwanza kabisa kama Sabini mpya. Bila maelezo ya kuweka swali katika muktadha, nilichanganyikiwa. “Sabini” aliendelea, “hawakilishi watu kwa nabii, lakini nabii kwa watu. Kamwe usisahau njia ipi utazame! ”Lilikuwa somo lenye nguvu.

Kujaribu kuwapendeza wengine kabla ya kumpendeza Mungu ni kuzigeuza amri kuu ya kwanza na ya pili (ona Mathayo 22:37–39).Ni kusahau ni njia gani tunatazama. Na bado, wote tumefanya kosa hilo kwa sababu ya hofu ya wanadamu. Katika Isaya Bwana anatuonya, “msiogope fedheha za wanadamu”(Isaya 51:7; ona pia  2  Nefi 8:7), Katika ndoto ya Lehi, hofu hii ilitawaliwa na vidole vya dharau vilivyoelekezwa kutoka kwenye nyumba kubwa yenye nafasi, na kusababisha wengi kusahau njia gani walitazama na kuondoka kwenye mti “wameaibika”ona( 1  Nefi 8:25–28).

Shinikizo rika hili lisilo na kifani linajaribu kubadili mitizamo ya mtu, kama si tabia, kwa kumfanya mtu ajihisi ana hatia kwa kufanya kosa. Tunatafuta kuishi pamoja kwa amani na heshima pamoja na hao wanaotunyooshea vidole, lakini wakati hii hofu ya wanaadamu inapotujaribu tuipuuze dhambi, inakuwa ni “mtego”kulingana na kitabu cha Mithali(ona Mithali 29:25).Mtego unaweza kutegwa kistadi na chambo ili kuvutia upande wetu wa huruma ili tuweze kuvumilia au hata kuafikia kitu fulani ambacho kimelaaniwa na Mungu. Kwa wadhaifu wa imani, hiyo inaweza kuwa kikwazo kikubwa. Kwa mfano, baadhi ya wamisionari vijana huwa na woga huu wa wanadamu kwenye uwanja wa misioni na kushindwa kutoa taarifa ya utovu wa utiifu ulio dhahiri wa mwenza wake kwa rais wa misheni yao kwa sababu hawataki kuwakasirisha wenza wao watukutu. Maamuzi ya tabia yanafanywa kwa kukumbuka utaratibu sahihi wa amri kuu ya kwanza na ya pili(ona Mathayo 22:37).Wakati wamisionari hawa waliochanganyikiwa wanatambua kwamba wanawajibika kwa Mungu na sio kwa mwenza wake, itawapasa wao kuwa na ujasiri wa kugeuza na kurudi.

Katika umri wa ujana wa miaka 22, hata Joseph Smith alisahau upande gani wa njia alitazama wakati aliporudia rudia kumwomba Bwana kumruhusu Martin Harris kuazima kurasa 116 za miswada. Labda Joseph alitaka kuonyesha shukrani kwa Martin kwa msaada wake. Tunajua kwamba Joseph alikuwa na hamu kubwa ya kuwa na mashahidi wengine ili wasimame pamoja naye dhidi ya uongo na udanganyifu uliokuwa ukienezwa juu yake.

Licha ya sababu alizokuwa nazo Joseph, au kadiri zilivyoonekana kuhalalishwa, Bwana hakuwasamehe na kwa ukali alimkemea: “Mara ngapi wewe umevunja sheria …na umeendelea katika ushawishi wa wanadamu. Kwani, tazama, hukutakiwa umwogope binaadamu zaidi kuliko Mungu”( M&M 3:6–7; (mkazo umeongezwa). Tukio hili lenye kutia uchungu lilimsaidia Joseph kukumbuka, milele alitazama upande gani.

Wakati watu wanapojaribu kuokoa nyuso zao kwa binadamu, wanaweza bila kutegemea kupoteza nyuso zao kwa Mungu. Ukifikiria mtu anaweza kumfurahisha Mungu na wakati huo huo kupuuza kutotii kwa mwanaadamu huko sio kutopendelea upande wowote bali ni unafiki,au kuwa na sura mbili au kujaribu “kuhudumia mabwana wawili” (Mathayo 6:24;  3 Nefi 13:24).

Huku ujasiri ukihitajika bila shaka kukabiliana na hatari kubwa, ishara ya kweli ya ujasiri ni kushinda hofu ya wanadamu. Kwa mfano, Maombi ya Danieli yalimsaidia kukabiliana na simba, lakini kile ikichomfanya awe na moyo wa simba kilikuwa ni kutomtii Mfalme Dario (ona Danieli  6).Aina ile ya ujasiri ni kipawa cha Roho kwa wamwogopao Mungu ambao wamesema sala zao. Sala za Malkia Esta pia zilimpa ujasiri kama ule wa kumkabili mume wake, Mfalme Ahasuero, akijua kwamba anahatarisha maisha yake kwa kufanya hivyo (ona  Esta 4:8–16).

Ujasiri sio tu moja ya maadili ya muhimu, lakini kama vile C.S. Lewis alivyoeleza:“ujasiri ni… hali ya kila wema iwapo katika kujaribiwa---. ...Pilato alikuwa mwenye huruma mpaka hali ikawa ya hatari kwake.”1 Mfalme Herode alikuwa mwenye huzuni kwa ombi la kumkata kichwa Yohana Mbatizaji lakini alitaka kuwafurahisha “wale ambao walikaa pamoja naye kwenye chakula”(Mathayo 14:9). Mfalme Nuhu alikuwa tayari kumwachia huru Abinadi mpaka shinikizo rika kutoka kwa makuhani wake waovu lilipomsababisha kuyumba (ona Mosia 17:11–12). Mfalme Sauli hakutii neno la Bwana kwa kuweka nyara za vita kwa sababu “aliwaogopa watu na kutii sauti zao” (1  Samweli 15:24).Ili kuwaridhisha Israel iliyoasi chini ya Mlima Sinai, Haruni alitengeneza ndama wa dhahabu, akisahau njia gani alitazama(ona Kutoka  32).Wengi wa watawala wakuu wa Agano Jipya “walimwamini [Bwana];lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri, wasije wakawekwa nje ya sinagogi: Kwani walipenda sifa za wanadamu zaidi kuliko sifa za Mungu” (Yohana 12:42–43).Maadiko yamejaa mifano kama hii.

Sasa sikiliza baadhi ya mifano ya kuvutia:

  • Kwanza, Mormoni: “Tazama, naongea kwa ujasiri, nikiwa na mamlaka kutoka kwa Mungu; na siogopi kile mtu anachoweza kufanya; kwani upendo ulio kamili hutupa nje hofu.” (Moroni 8:16;mkazo umeongezwa).

  • Nefi: “Kwa hivyo, sitaandika vitu vile ambavyo vinafurahisha ulimwengu, bali nitaandika yale ambayo yanamfurahisha Mungu na wale wasio wa ulimwengu.” (1  Nefi 6;5)

  • Kapteni Moroni: “Tazama, mimi ni Moroni, kapteni wenu mkuu. Sihitaji ukubwa, lakini kuuweka chini. Sitafuti heshima ya ulimwengu, lakini utukufu wa Mungu wangu, na uhuru na ustawi wa nchi yangu. Na hivyo ninamaliza barua yangu.”(Alma 60:36).

Mormoni alikuwa na ujasiri mkubwa katika kukumbuka njia ipi alitazama na kwamba ilisemwa hivi juu yake, “ikiwa watu wote walikuwa, na wako, na ikiwa watakuweko, kama Moroni, tazama, hizo nguvu za jahanamu zingetingishwa milele; ndio, huyo ibilisi kamwe hangekuwa na uwezo juu ya mioyo ya watoto wa watu” (Alma 48:17).

Manabii wa zama zote daima wamekuwa wakishambuliwa kwa kidole cha dharau. Kwa nini? Kulingana na maandiko, ni kwa sababu “wenye hatia huchukulia ukweli kuwa mgumu, kwani unawakata hadi sehemu zao za ndani” (1  Nefi 16:2), au kama Rais Harold B. Lee alivyoeleza, “Ndege aliyepigwa hupapatika!”2 Matendo yao ya dharau, kwa ukweli, ni hatia inayojaribu kujithibitisha yenyewe, sawa na Korihori ambaye hatimaye alikiri. “Nilijua siku zote kwamba kuna Mungu”(Alma 30:52) Korihori akivutia mno katika udanganyifu wake kiasi kwamba alikuja kuamini uongo wake yeye mwenyewe (ona Alma 30:53).

Wenye kudharau mara nyingi wamelalamika kwamba manabii hawaishi katika karne hii ya 21 au ya kuwa hawa ni walokole. Wanajaribu kushawishi na hata kushinikiza Kanisa kuteremsha viwango vya Mungu hadi kufikia daraja la tabia zao zisizofaa, ambazo kwa maneno ya Mzee Neil A. Maxwell, vitawaletea kujiridhisha wao wenyewe, badala ya kutafuta kujiboresha”3 na toba.”kuteremsha viwango vya Bwana hadi kwenye madaraja ya tabia zisizofaa za jamii ni - ukengeufu. Mengi ya makanisa miongoni mwa Wanefi karne mbili baada ya ziara ya Mwokozi kwao yalianza “kunyamazia”mafundisho, nikiazima msemo wa Mzee Holland.4

Wakati unaposikiliza dondoo hii kutoka 4 Nefi, tafuta inayofanana nayo katika siku yetu ya leo: “Na ikawa kwamba wakati miaka mia mbili na kumi ilipokuwa imepita kulikuwa na makanisa mengi katika nchi; ndio, kulikuwa na makanisa mengi ambayo yalidai kumjua Kristo, na bado yalikataa sehemu kubwa ya injili yake, mpaka kwamba yalikubali aina yote ya uovu, na yalitoa kila kilicho kitakatifu kwa yule ambaye alikuwa amekataliwa kwa sababu ya kutostahili” (4 Nefi 1:27‎)‎

Déjà vu katika siku za mwisho! Baadhi ya washiriki hawaelewi wanaanguka katika mtego aina hii wakati wanashawishi ili kukubalika kwa desturi za kwao au za makabila ya ulimwengu wa mababu zao ambazo hazipatani na utamaduni wa injili(M&M 93:39). Bado wengine, wanajidanganya wenyewe na kwa kujikana wenyewe, wanakiri au wanadai kwamba maaskofu wateremshe kiwango cha sifa ya kuingia hekaluni, idhini ya shule, au maombi ya umisionari. Si rahisi kuwa askofu chini ya shinikizo kama hili. Hata kama, Mwokozi ambaye alisafisha hekalu ili kulinda utakatifu Wake(ona Yohana 2:15–16).maaskofu leo wanaombwa kwa ujasiri walinde kiwango cha kupata kibali cha kuingia hekaluni. Alikuwa ni Mwokozi ambaye alisema, “Nami nitajionyesha kwa watu wangu kwa rehema … kama watu wangu watashika amri zangu, na ikiwa hawataichafua nyumba hii takatifu” (M&M 110:7–8‎).‎

Mwokozi, Mfano wetu mkubwa, siku zote alimtazama Baba Yake. Aliwapenda na kuwahudumia wanadamu Wenzake lakini alisema, “Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu.” (Yohana 5:41).Aliwataka wale aliowafundisha wamfuate Yeye, lakini hakutaka kubembeleza fadhila zao. Wakati alipofanya kitendo cha hisani, kama vile kuwaponya wagonjwa, zawadi mara kwa mara ilikuja pamoja na ombi “usimwambie mtu” (Mathayo 8:4; Marko 7:36; Luka 5:14;8:56).Kwa kiasi fulani, hii ilikuwa kuepuka hasa umaarufu ambao ulikuwa ukimfuata licha ya jitihada zake kuukwepa (ona Mathayo 4:24).Aliwalaani Mafarisayo kwa kufanya kazi mzuri ili tu waonekane na watu (ona Mathayo 6:5).

Mwokozi, kiumbe pekee mkamilifu aliyewahi kuishi, ambaye kamwe hakuopa kabisa. Katika maisha Yake, Alikabiliwa na kundi la washitaki lakini kamwe hakushindwa kwa vidole vyao vya dharau, Yeye ni mtu pekee ambaye kamwe hata mara moja hakusahau njia gani alitazama: “Nafanya daima yale yampendezayo[Baba]”(Yohana 8:29; mkazo umeongezwa),na “Siyatafuti mapenzi yangu Mimi, bali mapenzi yake Baba aliyenipeleka” (Yohana 5:30).

Katikati ya3 Nefi sura ya 11 na 3 Nefi sura ya 28,Mwokozi ametumia cheo Baba angalau mara 150, akifanya hivyo wazi kabisa kwa Wanefi kwamba Yeye alikuwa pale kumwakilisha Baba Yake. Na kutoka Yohana sura ya 14 mpaka  17, Mwokozi anamtaja Baba angalau mara 50. Kwa kila njia inayowezekana, alikuwa mfuasi kamili wa Baba yake. Alikuwa mkamilifu sana katika kumwakilisha Baba Yake kiasi kwamba kumjua Mwokozi kulikuwa pia kumjua Baba. Kumwona Mwana kulikuwa ni kumwona Baba (ona Yohana 14:9).Kumsikia Mwana kulikuwa ni kumsikia Baba (ona Yohana 5:36) alikuwa, katika asili amegeuka asiye tofautishwa na Baba Yake. Baba yake na Yeye walikuwa wamoja (ona Yohana 17:21–22). Alijua bila dosari njia ipi alitazama

Mfano wake wakuvutia na uweze kutuimarisha sisi dhidi ya mitego ya mashimo ya kusifiwa mno kutoka kwa nje au kutoka ndani. Na itupe sisi ujasiri wa kutojikunyata kamwe au kutojikomba miguuni pa tishio. Iweze kutuvutia sisi kwenda popote tukifanya mazuri pasi kujulikana kadiri iwezekanavyo na sio “kutaka sifa za wanadamu”(M&M 121:35). Na mfano wake usio kifani utusaidie siku zote kukumbuka ni ipi “amri ya kwanza iliyo kuu” (Mathayo 22:38). Wakati wengine wanadai idhini kwa kuasi amri za Mungu,sisi na tuweze siku zote kukumbuka kuwa tu wafuasi wa nani,na njia gani tunatazama, ni ombi langu katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. C.  S. Lewis, The Screwtape Letters, rev. ed. (1982), 137–38.

  2. Harold  B. Lee, in  Boyd K. Packer, Mine Errand from the Lord: Selections from the Sermons and Writings of Boyd K. Packer  (2008), 356.

  3. Neal  A. Maxwell, “Repentance,” Ensign, Nov. 1991, 32.

  4. Jeffrey  R. Holland, “The Call to Be Christlike, ”Ensign, June 2014, 33;Liahona, June 2014, 35.