2010–2019
Kitabu
Oktoba 2014


11:37

Kitabu

Kazi ya historia ya familia na hekalu inapaswa kuwa sehemu ya kawaida ya kuabudu kwetu kwa kibinafsi.

Kama kijana wa kiskauti mwenye umri wa miaka 12, nilipokea zawadi ya kifaa cha uskauti nilichokitamani sana. Kilikuwa ni shoka lenye ngozi nzito! Siku ya pili ya kambi, tuliwasili kambini baada ya giza, tukilowa maji na baridi kutoka kwa barafu nzito njiani. Yote ambayo niliweza kufikiria ilikuwa ni kutengeneza moto mkubwa wa kambi. Mara moja nikaanza kufanya kazi kwa kupasua mti ulioanguka kwa shoka langu jipya. Nilipokuwa nikipasua, nilifishwa moyo kwa sababu shoka langu halikuonekana kukata vizuri sana. Katika kufa moyo kwangu, nilifanya kazi kwa bidii sana. Kwa kusikitishwa, nilirejea kambini na vipande vichache tu vya kuni. Kwa mwanga wa moto wa mtu mwingine, niligundua tatizo. Sikuwa nimetoa ngozi ya kufunika shoka. Hata hivyo naweza kuripoti kuwa hiyo ngozi ilikatwa vipande vipande. Somo: Nilikuwa nimechanganywa ni mambo mengine.

Tunapofanya kazi ya kutuelekeza kuinuliwa, ni lazima tushughulikie mahitaji yote na tusipotoshwe kwa kuzingatia hitaji moja au mawili au mambo mengine yasiyohusika. Kutafuta ufalme wa Mungu kunaelekeza kwenye furaha na shangwe.1 Kama inahitajika, ni lazima tuwe tayari kubadilika. Marekebisho madogo ya mara kwa mara ni machungu kidogo na masumbufu kuliko marekebisho makubwa.

Si muda mrefu uliopita, Mimi na Dada Packer tulisafiri kwenye nchi kadhaa za kigeni. Tulitayarisha pasipoti zetu na hati zingine. Tulipewa chanjo zote, ukaguzi wa kimatibabu, visa, na mihuri. Kuwasili, hati zetu zilikaguliwa, na wakati mahitaji yote yalipotimizwa, tuliruhusiwa kuingia.

Kustahili kuinuliwa ni kama kujiandaa kuingia nchi nyingine. Ni lazima kila mmoja apate pasipoti yake mwenyewe ya kiroho. Hatutoi mashati, lakini, kibinafsi, ni lazima tuyatimize yote. Mpango wa wokovu una mafundisho, sheria, amri, na masharti yanayohitajika kwa wote kufuzu kuinuliwa.2 Kisha “kupitia Upatanisho wa [Yesu] Kristo, wanadamu wote waweze kuokolewa.”3 Kanisa hutusaidia lakini haliwezi kutufanyia haya. Kufuzu kuinuliwa inakuwa jitihada yetu ya maisha.

Kristo alipanga Kanisa Lake ili liweze kutusaidia. Amewaita Wanaume 15 tunaowaidhinisha kama manabii, waonaji, na wafunuaji ili kuongoza Kanisa na kutufundisha . Urais wa Kwanza4 na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili5 wana uwezo na mamlaka sawa,6 na Mtume mwandamizi aliyeteuliwa kama Rais wa Kanisa. Wale Sabini wameitwa kusaidia.7 Viongozi hawakutoa masharti ya kuinuliwa. Mungu alifanya hivyo! Viongozi hawa wameitwa kufundisha, kueleza, kushawishi, na hata kuonya ili tuweze kukaa kwenye njia sawa.8

Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha maelekezo: “Katika kutimiza madhumuni yake ya kusaidia watu binafsi na familia kuhitimu kwa ajili ya kuinuliwa, Kanisa linatilia mkazo majukumu yaliyotolewa na Mungu. Haya ni pamoja na kuwasaidia washiriki kuishi injili ya Yesu Kristo, kukusanya Israeli kupitia kwa kazi ya umisionari, kuwajali maskini na wenye shida, na kuwezesha wokovu wa wafu kwa kujenga mahekalu na kufanya ibada za niaba.”9 Malengo haya manne na sheria zingine zote, amri, na masharti yanahitajika na si kwa hiari. Kupitia kwa upatanisho wa Yesu Kristo na kwa kufanya kila moja ya haya, tunaongeza mihuri muhimu katika pasipoti zetu za kiroho.

Wakati wa mkutano huu tunafundishwa kuhusu mabadiliko ambayo yatatusaidia sote kujiandaa vilivyo.

Familia imo katikati ya mpango wa wokovu na labda ndio kwa sababu unaitwa pia mpango mkuu wa furaha.”10 Rais Boyd K. Packer amesema, “Madhumuni makubwa ya shughuli zote katika Kanisa ni kwamba mume na mke wake na watoto wao wanaweza kuwa na furaha nyumbani.”11

Rais Spencer  W. Kimball alisema, “Mafanikio yetu, kibinafsi na kama Kanisa, kwa kiasi kikubwa yataamuliwa na jinsi tunavyozingatia kwa uaminifu kuishi injili nyumbani.”12 Kazi ya Hekalu na historia ya familia ni sehemu ya kuishi injili nyumbani. Inapaswa kuwa shughuli ya familia sana zaidi na shughuli ya Kanisa.

Kumekuwa na msisitizo mpya wa kazi ya historia ya familia na hekalu na Urais wa Kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili.13 Majibu yako kwa msisitizo huu yataongeza furaha na shangwe kwako binafsi na kwa familia.

Kutoka kwa Mafundisho na Maagano tunasoma: “Siku iliyo kuu ya Bwana I karibu. ... Kwa hiyo, sisi kama kanisa na watu, na kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tumtolee Bwana dhabihu katika haki; nasi tuonyeshe katika hekalu Lake takatifu ... kitabu chenye kumbukumbu za wafu wetu, ambacho kitastahili kukubalika kote.”14

“Kitabu” hiki kitatayarishwa kutumia kumbukumbu katika hifadhidata ya Kanisa ya FamilyTree.

Naangalia na kuongeza rekodi kwa hifadhidata hii kwa sababu nataka majina ya wale wote ninaowapenda wawe kwenye kitabu. Je, wewe hutaki?

Mafundisho na Maagano sehemu ya 128 inasema, “Kwani sisi pasipo wao [mababu zetu] hatuwezi kukamilika; wala wao pasipo sisi hawawezi kukamilika.”15

Historia ya familia ni zaidi ya nasaba, sheria, majina, tarehe, na maeneo. Ni zaidi ya mkazo katika wakati uliopita. Historia ya familia pia inajumuisha wakati wa sasa tunapotengeneza historia yetu wenyewe. Inajumuisha siku za baadaye tunapobadilisha historia ya baadaye kupitia kwa ukoo wetu. Mama mchanga kwa mfano, akishiriki hadithi za familia yake na picha pamoja na watoto wake anafanya kazi ya historia ya familia.

Kama vile kushiriki sakramenti, kuhudhuria mikutano, kusoma maandiko, na maombi binafsi, historia ya familia na kazi ya hekalu inapaswa kuwa sehemu ya kawaida ya ibada yetu binafsi. Mwitikio wa vijana wetu, na wengine kwa mialiko ya kinabii imekuwa na maongozi na inathibitisha kazi hii inaweza na inapaswa kufanywa na washiriki wote wa umri wowote.

Kama vile Mzee Quentin  L. Cook alivyoelezea, sasa tuna mafundisho, mahekalu, na teknolojia.”16 Kufanya kazi hiyo sasa ni rahisi sana na hufanywa tu na idadi ya washiriki wanaoipa kipaumbele. Kazi hiyo bado inahitaji muda na kujitolea, lakini wote wanaweza kuifanya, na kwa urahisi ikilinganishwa na miaka michache tu iliyopita.

Ili kuwasaidia washiriki, Kanisa limekusanya kumbukumbu na kupeana vifaa ili sehemu kubwa ya kazi iweze kufanyika katika nyumba zetu wenyewe au katika majengo yetu ya kata na hekalu. Vingi vya vikwazo vimeondolewa. Yoyote ingine mtazamo wako wa kitambo, ni tofauti sasa!

Hata hivyo, kuna kikwazo ambacho Kanisa haliwezi kuondoa. Ni kule kusitasita kwa mtu kufanya kazi hii. Yote yanayohitajika ni uamuzi na juhudi kidogo. Haihitaji sehemu kubwa ya muda. Ni muda kidogo tu kila wakati utakaoleta furaha ya kazi. Fanya uamuzi wa kusonga mbele kidogo ili kujifunza na kuomba wengine kukusaidia. Watakusaidia! Majina unayopata na kupeleka hekaluni yatakuwa kumbukumbu kwenye “kitabu.”17

Hata pamoja na ongezeko kubwa la ushiriki wa washiriki, tunagundua kwamba washiriki wachache wa Kanisa wanahusika mara kwa mara katika kutafuta na kufanya maagizo ya hekalu kwa familia. 18Hali hii inahitaji mabadiliko katika vipaumbele vyetu. Usipinge mabadiliko, yakubali! Mabadiliko ni sehemu ya mpango mkubwa wa furaha.

Kazi hii inahitaji kufanywa, si kwa faida ya Kanisa lakini kwa wafu wetu na kwa sisi wenyewe. Sisi na mababu zetu walioaga tunahitaji mihuri katika pasipoti zetu za kiroho.

“Muunganiko wa pamoja”19 wa familia zetu katika vizazi vyote unaweza kutokea tu katika mahekalu kupitia kwa maagizo ya kufunganisha. Hatua ni rahisi: pata tu jina na uliipeleke hekaluni. Baada ya muda utaweza kuwasaidia wengine kufanya hivyo pia.

Isipokuwa kwa wachache tu—kila mtu—anaweza kufanya hivyo!

Kuna baraka halisi inayohusiana na kazi hii. Wazazi na viongozi wengi wana wasiwasi kuhusu hali ya sasa ya dunia na athari yake kwa familia na vijana.

Mzee David A. Bednar ameahidi: “Ninawaalika vijana wa Kanisa kujifunza kuhusu na kuhisi Roho wa Eliya. ... Ninaahidi [kwamba] mtalindwa dhidi ya ushawishi mwingi wa adui. Unaposhiriki katika kazi hii takatifu na kuipenda, utalindwa katika ujana wako na katika maisha yako.”20

Akina ndugu na dada, ni wakati wa kutoa juu ya shoka zetu na kwenda kazini. Hatupaswi kuachilia kuinuliwa kwetu au kule wa familia zetu kwa maslahi yasiyo ya muhimu.

Hii ni kazi ya Mungu, ya kufanywa na washiriki na wasio washiriki sawa sawa, vijana na wazee, waume na wake.

Nitahitimisha kwa kunukuu msitari wa kwanza wa wimbo 324, nilibadilisha neno moja:

Inukeni, Enyi [Watakatifu] wa Mungu!

Mmefanya mambo madogo.

Jitoleeni kwa moyo na nafsi, akili na nguvu.

Kumtumikia Mfalme wa Wafalme.21

Mimi ninashuhudia juu Yake katika jina la Yesu Kristo, amina.