2010–2019
Huduma Zetu za Kibinafsi
Oktoba 2014


10:23

Huduma Zetu za Kibinafsi

Upendo wa Yesu Kristo sharti uwe mwongozo wetu ikiwa sisi tutakuwa tunafahamu mahitaji ya wale tunaweza kuwasaidia katika njia fulani.

Katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunapewa fursa na baraka za kibinafsi za kutumika. Kwa muda wote ambao nimekuwa mshiriki, nimetumika katika njia nyingi. Kama Ndugu Udine Falabella, baba yake Mzee Enrique  R. Falabella, alivyozoea kusema “Yule atumikiaye katika jambo fulani ni mzuri katika jambo fulani; Yule asiyetumikia katika jambo lolote hafai kwa chochote.” Haya ni maneno ambayo tunahitajika kuyaweka akilini na mioyoni mwetu

Jinsi nilivyotafuta mwongozo katika huduma yangu, nimepata faraja katika kukumbuka kwamba Mwokozi hutilia mkazo zaidi kwa mtu binafsi na familia. Upendo na usikivu Wake mwema kwa mtu umenifundisha mimi kwamba Yeye anatambua thamani kuu ya kila mtoto wa Baba wa Mbinguni na kwamba ni muhimu kwetu kuhakikisha kwamba kila mmoja anahudumiwa na kuimarishwa kwa injili ya Yesu Kristo

Katika maandiko tunasoma:

“Kumbukeni thamani ya nafsi ni kubwa machoni pa Mungu…

“Na ikibidi kwamba ufanye kazi siku zote za maisha yako…na kuileta, japo nafsi moja kwangu, furaha yako itakuwa kubwa kiasi gani pamoja naye katika ufalme wa Baba yangu!”1

Kila nafsi ni ya thamani kubwa kwa Mungu, kwani sisi tu watoto wake na tunao uwezekano wa kuwa kama Yeye alivyo.2

Upendo wa Yesu Kristo lazima uwe mwongozo wetu kama tunataka kutambua mahitaji ya wale tunaoweza kuwasaidia kwa njia fulani. Mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristo, yanatuonyesha njia. Na hivyo ndivyo huduma zetu za kibinafsi zinavyoanza: kugundua shida, kisha kuzishughulikia. Kama vile Dada Linda  K. Burton, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alivyosema, “Kwanza tazama, kisha tumikia.”3

Rais Thomas S. Monson ni mfano mkubwa wa kanuni hii. Katika Januari ya 2005, alikuwa akiongoza mkutano wa viongozi wa ukuhani katika Puerto Rico wakati alipoonyesha namna Mwokozi na watumishi Wake wanavyotoa huduma kwa njia ya huduma ya kibinafsi. Mwishoni mwa mkutano ule mzuri, Rais Monson alianza kuwasalimia viongozi wote wa ukuhani waliohudhuria. Ghafla aligundua kwamba mmoja wao alikuwa akiangalia kutoka mbali kidogo akiwa pekee yake.

Raisi Monson alimwendea kule pembeni, alikokuwa, na kumsemesha. Kwa hisia kubwa, Jose  R. Zayas alimwambia huo ulikuwa ni muujiza wa yeye kumsogelea na ni jibu la maombi yake yeye na mkewe, Yolanda, waliyoomba kabla ya mkutano ule. Alimwambia Rais Monson kwamba binti yao yu katika hali mbaya kiafya na kwamba yeye alikuwa na barua iliyoandikwa na mke wake ambayo alimtaka aifikishe kwa Rais Monson. Ndugu Zayas alimwambia mke wake kuwa jambo hilo halitawezekana kwa vile Rais Monson ana shughuli nyingi hatakuwa na nafasi. Raisi Monson alisikiliza habari ile na kisha akaomba hiyo barua, ambayo aliisoma kimya kimya. Kisha akaiweka katika mfuko wa suti yake na akamwambia Ndugu Zayas kwamba yeye atayashughulikia maombi yao.

Kwa njia hiyo, familia ile iliguswa na Bwana wetu Yesu Kristo, kupitia mtumishi Wake. Naamini maneno ya Mwokozi katika mfano wa Msamaria mwema yanatuhusu sisi: “Nenda, na ukafanye vivyo hivyo.”4

Mnamo Septemba 21, 1998, Kimbunga Georges kiliipiga Puerto Rico, kikisababisha uharibifu mkubwa. Dada Martinez, watoto wetu watano, nami tuliweza kusalimika dhoruba ile kubwa na upepo wa nguvu ya kimbunga kwa kukaa ndani ya nyumba yetu. Hata hivyo tulikaa kwa wiki mbili pasipo mabomba kutoa maji wala umeme.

Akiba yetu ya maji ilipoisha, kupata mengine ilikuwa vigumu sana. Siwezi kuwasahau ndugu viongozi wa Kanisa waliotuhudumia kwa kutuletea kimiminika kile muhimu, wala siwezi kusahau njia za upendo ambayo pia akina dada waliotuhudumia sisi.

German Colon alikuja nyumbani kwetu … akiwa na chombo kikubwa cha plastiki kilichojaa maji ndani ya gari lake la mizigo. Alituambia kuwa yeye anafanya hivyo kwa sababu “katika maneno yake alijua ya kuwa mna watoto wadogo ambao wanahitaji maji” Siku mbili baadaye, Ndugu Noel Munoz na Hermanio Gomez walipakia matanki matatu makubwa ya maji katika lori la wazi. Walifika nyumbani kwetu bila kutegemewa na kutujazia kila chupa iliyopatikana hapo kwa maji ya kunywa na pia kuwaalika majirani zetu nao kujaza vyombo vyao.

Maombi yetu yalijibiwa kwa huduma yao ya kibinafsi. Nyuso za wale ndugu watatu zilionyesha upendo ambao Yesu Kristo anao juu yetu sisi, na huduma zao---kwa maneno mengine, huduma zao za kibinafsi zilileta zaidi ya maji ya kunywa katika maisha yetu. Kwa kila mwana au binti wa Mungu, kujua kwamba watu wanakujali na kulinda ustawi wake ni jambo la muhimu.

Ninakushuhudieni ya kwamba Baba wa Mbinguni na Bwana wetu Yesu Kristo, wanatujua sisi kibinafsi na pia mmoja mmoja. Kwa sababu hiyo. Wao hutoa yale tunayohitaji ili tuweze kupata fursa ya kufikia uwezekano wetu mtakatifu. Katika barabara, Wao wanawaweka watu ambao watatusaidia. Kisha kadiri tunavyokuja kuwa vyombo mikononi mwao, tunakuwa na uwezo wa kuwatumikia na kuwasaidia wale watatuonyesha sisi kwa njia ya ufunuo.

Katika njia hii, Bwana Yesu Kristo atawafikia watoto wote wa Baba wa Mbinguni. Mchungaji Mwema atawakusanya kondoo wake wote. Yeye atawakusanya mmoja mmoja kadiri wafanyapo matumizi mazuri yao ya haki ya kujiamulia au baada ya ile sauti ya watumishi wake na kupokea huduma zao. Ndipo watakapoitambua sauti yake, nao watamfuata Yeye. Aina hiyo ya huduma ni muhimu katika kushika maagano yetu ya ubatizo.

Vile vile, kuwa mfano mzuri wa wanafunzi wa Yesu Kristo ni barua bora ya utambulisho wa wale tunaoweza kuwafundisha injili Yake kadiri tunavyofungua vinywa vyetu na kushiriki nao injili ya urejesho wa Yesu Kristo, tunakuwa “Wachungaji wasidizi Wake tukiwa tumeamriwa kuwalisha kondoo wake malisho yake na kondoo wa kundi Lake ”5tunakuwa “wadhaifu na wa kawaida”6“wavuvi wa watu.”7

Utumishi wetu na huduma ya kibinafsi si tu kwa maisha ya hapa duniani. Tunaweza pia kufanya kazi kwa niaba ya wafu---kwa ajili ya wale waishio katika ulimwengu wa roho na ambao wakati wa maisha yao hapa duniani, hawakupata fursa ya kupokea ibada za wokovu za injili ya Yesu Kristo. Tunaweza pia kuandika shajara na historia ya familia zetu ili kuigeuza mioyo ya walio hai kuwaelekea walio hai---vile vile mioyo ya walio hai kuwaelekea mababu zao. Haya yote ni katika kuziunganisha familia zetu kizazi kwa kizazi, katika minyororo ya milele. Tufanyapo haya, tunakuwa “waokozi … juu ya mlima sayuni.”8

Tunayo fursa maalum ya kuwa vyombo katika mikono Yake. Tunaweza kuwa hivyo katika ndoa zetu, katika familia zetu, kwa rafiki zetu na wanadamu wenzetu. Hiyo ndiyo huduma yetu ya kibinafsi kama wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

“Na mbele yake yatakusanywa mataifa yote na yeye atawatenganisha mmoja mbali na mwingine kama vile mchunga kondoo atenganishavyo kondoo na mbuzi:

“Na ataweka kondoo mkono wake wa kulia, lakini mbuzi mkono wa kushoto.

“Na kisha mfalme atasema kwa wale walio mkono wa kulia, njooni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu:

“Kwani nalikuwa na njaa, nanyi mkanipa chakula, nalikuwa na kiu, mkaninywesha, nalikuwa mgeni,mkanikaribisha:

“Nalikuwa uchi mkanivisha; nalikuwa mgonjwa mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

“Ndipo wenye haki walipomjibu, wakasema Bwana ni lini tulikuona na njaa, tukakulisha au una kiu tukakunywesha?

“Lini tulikuona u mgeni, tukakukaribisha au uko uchi na tukakuvisha?

“Au lini tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni tukakujia?

“Na Mfalme atajibu, akiwaambia, amini nawaambia, kadiri nilivyo mtendea mmoja wa ndugu zangu wadogo hawa, mmenitendea mimi.”9

Kwamba na tuyafanye hayo ndiyo maombi yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.