Kupokea Ushuhuda wa Nuru na Ukweli
Ushuhuda wenu wa nuru na kweli hautawabariki tu nyinyi na vizazi vyenu hapa duniani, bali pia utawaongoza popote milele
Kama Rubani wa ndege za abiria, Niliruka masaa mengi kuvuka bara na bahari wakati wa giza la usiku. Nikiangalia anga usiku kupitia dirisha la chumba cha rubani, hususani Kilimia, mara nyingi nilishangazwa na ukuu na kina cha uumbaji wa Mungu---kile maandiko yanaelezea kama “ Dunia zisizohesabika.”1
Ilikuwa chini ya karne moja iliyopita ambapo Wanafalaki walisadiki kwamba Kilimia chetu cha kundi la nyota na sayari kilikuwa ni kundi la nyota na sayari pekee katika Ulimwengu.2 Waliamini kwamba vyote vilivyokuwa vimezagaa mbele ya kundi la nyota pamoja na sayari yetu ilikuwa ni hali kubwa ya utupu na kitu na uwazi usio kuwa na mwisho---tupu, baridi na isiyokuwa na nyota, mwanga na maisha.
Wakati darubini zilipokuwa za kisasa zaidi---zikijumuishwa na darubini ambazo ziliweza kutumwa angani---wanafalaki walianza kuelewa ukweli wa kustaajabisha, usioeleweka: Ulimwengu ni mkubwa sana, zaidi vile ilivyodhaniwa na yeyote hapo awali, kwamba mbingu zimejawa na sayari zisizohesabika, ni mbali kutokana nasi kuliko tunavyoweza kudhania, kila mojawapo ikiwa na mamia ya mabillioni ya nyota.3
Katika kipindi cha muda mfupi,uelewa wetu wa ulimwengu ukabadilika kabisa.
Hivi leo tunaweza kuona baadhi ya haya makundi ya nyota na sayari yaliyo mbali.4
Twajua kwamba yapo hapo.
Yamekuwepo kwa muda mrefu sana.
Lakini kabla binadamu hajawa na zana zenye nguvu za kutosha kukusanya mwanga wa mbinguni na kuyaleta haya makundi ya nyota na sayari katika hali ya kuonekana wazi, hatukuamini kitu kama hiki kingewezekana.
Ukubwa uliopita kiasi wa ulimwengu haukubadilika ghafla, lakini uwezo wetu wa kuona na kuelewa ukweli huu ulibadilika kwa namna ya kuvutia. Na pamoja na elimu iliyoongezeka, binadamu alijulishwa kwenye mandhari adimu
Ni vigumu kwetu Sisi Kuamini Tusichokiona
Tuseme ungeweza kusafiri nyuma kwa muda na kuwa na mazungumzo pamoja na watu walioishi miaka elfu au hata miaka mia iliyopita. Fikiria ukijaribu kuwaelezea baadhi ya teknolojia za kisasa ambazo wewe na mimi tunaziona kuwa za kawaida leo. Kwa mfano, watu hawa wanaweza kufikiria nini kutuhusu kama tungewaambia hadithi za ndege kubwa, jiko la wimbi mikro, vyombo vya kushika mkononi ambavyo vina wingi wa tarakimu katika maktaba zake, na video za wajukuu wetu ambazo tunazoshiriki mara moja na mamilioni ya watu kuzunguka ulimwengu?
Baadhi wangeweza kutuamini. Walio wengi wangetudhihaki, kutupinga, au labda hata kutunyamazisha au kutudhuru. Baadhi wangeweza kujaribu kutumia mantiki, sababu, na kweli kama wanavyozijua kuonyesha kwamba sisi tumepotoshwa, tu wajinga, au hata hatari. Wangeweza kutulaani kwa kujaribu kuwapotosha wengine.
Lakini bila shaka, watu hawa wangekuwa kabisa wamekosea. Wangeweza kuwa wanajaribu kutoa msaada na kwa kweli. Wangeweza kuhisi kabisa kwamba mawazo yao ni sahihi. Lakini kwa kawaida wasingeweza kuona kwa uwazi kwa sababu bado hawakuwa wamepokea mwanga mkamilifu zaidi, uleule wa kweli.
Ahadi ya mwanga
Inaonekana kuwa tabia ya kibinadamu kusadiki kwamba tuko sahihi hata wakati tumekosea. Na kama ni kweli, ni tumaini gani lililopo kwa yeyote kati yetu? Je, tumejaliwa kuelea tu katika bahari ya mgongano wa habari au kukwama kwenye boya tuliounda vibaya kutokana na mitazamo yetu wenyewe?.
Inawezekana kupata ukweli?
Kusudi la maoni yangu ni kutangaza ujumbe wa furaha kwamba Mungu Mwenyewe---Bwana wa Majeshi ajuae ukweli wote---amewapa watoto wake ahadi kwamba wanaweza kujua ukweli kwa ajili yao wenyewe
Tafadhali fikiria ukuu wa ahadi hii:
Mwenyezi Mungu wa Milele na, Muumbaji wa ulimwengu huu mkubwa kupita kiasi, atazungumza kwa wale ambao wanamsogelea kwa moyo wa kweli na kusudi halisi.
Atasema nao katika ndoto, maono, mawazo,na hisia.
Atasema katika njia ambayo haiwezi kukosewa na ambayo ni kubwa zaidi ya uzoefu wa binadamu.
Bila shaka, watakuwapo wale wanaodhihaki na kusema kwamba jambo kama hili haliwezekani, kwamba kama kungekuwa na Mungu, Angekuwa na masuala bora zaidi ya kufanya kuliko kusikia na kujibu sala moja tu ya mtu.
Lakini nakuambia hivi, Mungu anakujali wewe. Atasikiliza na Atajibu maswali yako binafsi. Majibu ya sala zako yatakuja katika njia Yake mwenyewe na katika muda Wake mwenyewe. Na kwa hiyo, unatakiwa kijifunza kusikiliza sauti Yake. Mungu anakutaka wewe kutafuta njia yako ya kurudi Kwake, na Mwokozi ndiye njia.5 Mungu anataka ujifunze kuhusu Mwanawe, Yesu Kristo, na upate uzoefu wa amani kubwa na furaha ambayo inakuja kutokana na kufuata njia ya ufuasi mtakatifu.
Marafiki wapendwa, kuna jaribio nyoofu maridhawa, pamoja na dhamana kutoka kwa Mungu, inayopatikana katika kitabu cha maandiko ya kale inachopatikana kwa ajili ya kila mwanaume, mwanamke,na mtoto aliyeamua kujaribu kama ni kweli.
Kwanza, lazima utafute neno la Mungu. Hiyo ina maana kusoma maandiko na kujifunza maneno ya manaabi wa kale na vilevile manabii wa kisasa kuhusu injili ya urejesho ya Yesu Kristo---bila kuwa na nia ya kuwa na shaka, au kukosoa lakini pamoja na tamanio la kweli la kugundua kweli. Tafakari juu ya mambo yale unayahisi na utayarishe nafsi yako kupokea ukweli.6 “Hata ikiwa hamwezi tena ila kutamani kuamini, acha hamu hii ifanye kazi ndani yenu …. kwa njia ambayo mtatoa nafasi kwa sehemu ya [neno la Mungu].”7
Pili, lazima ufikiri, utafakari, bila hofu hujaribu kuamini,8 na uwe na shukrani kwa jinsi Bwana amekuwa mwenye huruma kwa watoto Wake kutoka wakati wa Adamu mpaka siku yetu kwa kutupatia manabii, waonaji, na wafunuaji kuliongoza Kanisa Lake na kutusaidia sisi kuona njia ya kurudi kwake.
Tatu, lazima umwulize Baba yako wa Mbinguni katika jina la Mwanawe Yesu Kristo, kudhihirisha kwako ukweli wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho. Uliza na moyo wa kweli na dhamira halisi, ukiwa na imani katika Kristo.9
Kuna pia hatua ya nne tuliyopewa sisi na mwokozi: “Kama mtu yeyote atafanya mapenzi ya [Mungu], atajua juu ya mafundisho kama yatakuwa ya Mungu, au kama nasema juu yangu mwenyewe.”10 Kwa maneno mengine, wakati unapojaribu kuthibitisha ukweli wa kanuni za injili, haunabudi kwanza kuishi kufuatana na kanuni hizo.Weka kanuni za injili na mafundisho ya Kanisa kwenye kipimo katika maisha yako mwenyewe. Fanya hivyo kwa dhamira halisi na imani ya uvumilivu katika Mungu.
Kama utafanya vitu hivi, una ahadi kutoka kwa Mungu---ambaye anafungwa kupitia neno Lake11—kwamba ataonyesha ukweli kwako kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu. Atakuidhinishia wewe mwanga mkubwa zaidi ambao utakuruhusu wewe kuangalia kupita kwenye giza na kushuhudia mandhari adhimu yasiyofikirika. Upeo usioeleweka kwa binadamu.
Wengine wanaweza kusema kwamba hatua ni ngumu sana au kwamba hazistahili juhudi hiyo. Lakini ninapendekeza kwamba ushuhuda huu wa binafsi wa injili na Kanisa ni kitu muhimu sana unaweza kuupata katika maisha haya. Hautakubariki na kukuongoza tu wakati wa maisha haya, bali pia utakuwa na athari juu ya maisha yako yote ya milele.
Mambo ya Kiroho Yanaweza Kuelewekwa tu Kwa Njia ya Kiroho
Wanasayansi walikuwa wanasumbuka kuelewa upana wa ulimwengu, mpaka zana zilipokuwa za kisasa kutosha kukusanya ndani mwanga mkubwa sana ili waweze kuelewa ukweli kamili zaidi.
Mtume Paolo alifundisha kanuni inayofanana kuhusu elimu ya Kiroho. “Mtu wa kawaida hapokei vitu vya Roho ya Mungu,”aliandika kwa Wakorintho, “kwani ni ujinga kwake: wala hawezi kuvijua kwa sababu vinatambulika Kiroho.”12
Kwa maneno mengine, kama unataka kutambua ukweli wa kiroho, unatakiwa kutumia vifaa sahihi. Huwezi kupata uelewa wa ukweli wa kiroho na vifaa ambavyo havina uwezo wa kuvigundua.
Mwokozi ametuambia sisi katika siku yetu, “Kile ambacho ni cha Mungu ni mwanga; na yeye ambaye anapokea mwanga, na kuendelea katika Mungu, anapokea mwanga zaidi; na mwanga ule unag’aa na kung’aa mpaka siku timilifu.”13
Tunapozidi kuelekeza mioyo yetu na mawazo kuelekea kwa Mungu, tunapewa mwanga mwingi wa mbinguni. Na kila wakati tunapo na hiari na kwa dhati kutafuta mwanga ule, tunaonyesha kwa Mungu wetu utayari wetu kupokea mwanga zaidi. Polepole kile mwanzo kilionekana kuwa na ukungu, giza, na mbali kinakuwa wazi, chenye kung’aa na kilichozoeleka kwetu.
Kwa njia hiyo hiyo tunajitoa kutoka kwenye mwanga wa injili, mwanga wetu unaanza kufifia---sio katika siku moja au wiki moja lakini polepole kwa muda---mpaka tunapoangalia nyuma na tunashindwa kabisa kuelewa kwa nini daima tuliamini injili ilikuwa kweli. Elimu yetu ya mwanzo inaweza hata kuonekana ujinga kwetu kwa sababu kile ambacho hapo mwanzo kilikuwa wazi kimekuwa tena hakionekani vizuri, chenye ukungu na mbali.
Hii ndiyo kwa nini Paulo alikuwa imara katika imani yake kwamba ujumbe wa injili ni ujinga kwa wale ambao wanaangamia, “lakini kwa wale [ambao]wameokolewa ni nguvu ya Mungu.”14
Hakuna jaribio la Litimasi
Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni sehemu kwa watu wenye kila aina ya shuhuda. Kuna washiriki fulani ambao ushuhuda wao ni wa uhakika na wenye nguvu sana. Wengine bado wanajitahidi kujua kwa ajili yao wenyewe. Kanisa ni nyumbani kwa wote kuja pamoja, bila kujali uwezo wa ushuhuda wetu, hakuna alama kwenye milango ya nyumba zetu za mikutano ambayo inasema, “uhuhuda wako lazima uwe na nguvu hii ili uingie.”
Kanisa si tu kwa watu walio wakamilifu, lakini ni kwa wote “waje kwa Kristo, na wawe wakamilifu katika Yeye.”15 Kanisa imo kwa ajili ya watu kama wewe na mimi. Kanisa ni sehemu ya kukaribisha na kielimisha, si ya kutenganisha au kukosoana. Ni sehemu ambapo tunanyoosha mikono kutiana moyo, kuinuana, na kuidhinishana tunapofuatilia upekuzi wetu kwa ukweli mtakatifu.
Hatimaye, sisi wote ni wasafiri tunatafuta mwanga wa Mungu wakati tunaposafiri kwenye njia ya ufuasi. Hatuwalaumu wengine kwa kiasi cha mwanga wanaoweza kuwa au kutokuwa nao; bali tunarutubisha na kutia moyo mwanga wote mpaka unakuwa wazi,unaong’aa, na wa kweli.
Ahadi kwa Wote
Acha sisi tukubali kwamba mara nyingi kupata ushuhuda si kazi inayoisha dakika moja, saa moja, au siku moja. Si kitu fulani ambacho kinaweza kukamilika mara moja na kisha kufanyika. Njia ya kukusanya mwanga wa kiroho ni safari ambayo mwisho wake ni muda wote wa maisha.
Ushuhuda wako wa mwana wa Mungu anayeishi na Kanisa Lake la urejesho, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, linaweza lisije kwa haraka kama unavyotamani lakini naweza kukuahidi hili: kama utafanya sehemu yako, litakuja.
Na litakuwa tukufu
Ninakupa ushahidi wangu binafsi kwamba ukweli wa kiroho utajaza moyo wako na kuleta mwanga kwa roho yako. Utakuonyesha kwako akili halisi pamoja na furaha ya ajabu na amani ya kimbinguni. Nimepata uzoefu kwangu mwenyewe kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Kama vile maandiko ya kale yanavyoahidi, uwepo usioneneka wa Roho ya Mungu utakufanya wewe uimbe wimbo wa upendo na ukombozi,16 inua macho yako mbinguni, na kupaaza sauti yako katika sifa kwa Mungu aliye juu sana, kimbilio lako, tumaini lako, mlinzi wako, Baba yako. Mwokozi aliahidi kwamba kama utatafuta, utapata.17
Ninashuhudia kwamba hii ni kweli. Kama unatafuta ukweli wa Mungu, kile ambacho sasa kinaweza kuonekana kufifia, chenye mauzauza, na mbali polepole kitafunuliwa, na kubainishwa, na kuwa karibu na moyo wako kwa mwanga wa rehema ya Mungu. Mandhari matukufu ya kiroho, yasiyofikirika kwenye jicho la binadamu,yataonyeshwa kwako.
Ni ushuhuda wangu kwamba mwanga huu wa kiroho unapatikana kwa kila mtoto wa Mungu. Utaelimisha kumbukumbu zako, na kuleta uponyaji kwa moyo wako na furaha kwa siku zako. Marafiki wangu wapwendwa, tafadhali msicheleweshe muda kutafuta na kuimarisha ushuhuda wenu binafsi wa kazi takatifu ya Mungu, hata kazi ya nuru na haki.
Ushuhuda wenu wa kibinafsi wa nuru na kweli hautawabariki tu nyinyi na vizazi vyenu hapa duniani, bali utawaongoza nyinyi popote milele, miongoni mwa dunia zisizo na mwisho. Juu ya haya nashuhudia na kuwaachieni baraka zangu katika jina la Yesu Kristo, amina.