Kuitafuta Amani ya Milele na Kujenga Familia za Milele
Ni injili ya Yesu Kristo ambayo inatoa msingi ambao juu yake tunaweza kupata amani ya kudumu na vitengo vya familia vya milele.
Safari yetu katika maisha ina vipindi vizuri na vibaya. Kila kipindi kina changamoto tofauti. Jinsi tunavyojifunza kuzoea mabadiliko ambayo yanakuja kunategemea msingi ambao tumeujenga. Injili ya Bwana na Mwokozi wetu inaleta msingi wa kweli na imara. Umejengwa kipande kwa kipande huku tukipata ufahamu wa mpango wa milele wa Bwana kwa watoto Wake. Mwokozi ni Mwalimu Mkuu. Sisi tunamfuata Yeye.
Maandiko yanamshuhudia Yeye na yanatoa mfano wa wema mkamilifu ili sisi tuweze kuufuata. Nimeshiriki na waumini wa Kanisa katika mkutano uliopita kwamba nina idadi ya madaftari ambayo mama yangu aliandika mambo aliyokuwa anayatumia katika kuandaa masomo yake ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Ujumbe unaeleza vile vile kama ulivyoeleza hapo kale. Moja ya ujumbe huo ilikuwa nukuu iliyoandikwa mwaka 1908 na Charles Edward Jefferson juu ya silka ya Yesu Kristo. Inasomeka:
“Kuwa Mkristo ni kumtamani Yesu kwa dhati na kwa bidii ili maisha yote yaende kwake kwa hamu ya kuwa kama Yeye.
“… Tunaweza kumjua yeye kupitia maneno aliyoongea, kupitia matendo yake, na pia kupitia ukimya wake. Tunaweza pia kumjua yeye kwa alama aliyoiweka kwanza kwa rafiki zake na pili kwa maadui wake, na tatu kwa watu ambao walikuwa wanaishi kipindi chake.
“Moja ya muhtasari wa karne ya ishirini ni kutotosheka [na shida]. ….
“… Ulimwengu unahitaji kitu fulani, lakini haujui ni kitu gani. Utajiri umekuja, … ulimwengu umejaa … uvumbuzi wa utaalamu wa mwanadamu na kipaji, lakini … [ bado] hatupumziki, hatutosheki [na] ni watatanishi. … [Kama tutafungua] Agano Jipya [tutasalimiwa, Na maneno haya], ‘Njooni kwangu nami nitawapumzisha, mimi ni mkate wa uzima, mimi ni nuru ya ulimwengu, kama mtu ana kiu acheni aje kwangu na atakunywa, amani yangu nawaachieni, mtapokea uwezo, nanyi mtafurahi” (The Character of Jesus [1908], 7, 11, 15–16).
Wanaume na wanawake wanachongwa kwa kiasi fulani na wale wanaochagua kuishi nao. Watu wanaotegemea na kujaribu kuiga pia wanaingia kwenye hayo matatizo. Yesu ni Mfano Mkuu wa kuigwa. Njia pekee ya kupata amani ya milele ni kumwangalia Yeye na kuishi.
Ni nini kinastahili cha kujifunza kuhusu Yesu?
Waandishi wa Agano Jipya hawakujali juu ya umbo la [Yesu], nguo alizovaa, au nyumba alizoishi. … Alizaliwa kwenye zizi, alifanya kazi za useremala, alifundisha kwa miaka mitatu, kasha akafa msalabani. … Agano jipya liliandikwa na watu waliojitolea … wakimlenga [Yeye] (Silka ya Yesu, 21–22) wakiwa na uhakika kwamba kwa hakika Yeye alikuwa na ni Mwana wa Mungu, Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu.
Ninaamini kwamba kuna fumbo moja la Mwokozi ambalo linahusiana hasa na siku yetu ya leo.
Linapatikana katika Mathayo sura ya 13, ambapo tunasoma:
“Wakati watu walipolala, adui yake akaja na akapanda magugu katikakti ya ngano, na akaenda zake.
“Baadaye majani ya ngano yalipomea, na kuzaa, yakaonekana na magugu pia.
“Hivyo watumishi wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika shamba lako? Limepata wapi magugu?
“Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumishi wakamwambia, Basi wataka twende tukayakusanye?
“Lakini akasema, La, msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.
“Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome, bali ngano ikusanyeni ghalani kwangu” (mistari ya 25–30).
Yule adui wa mwanadamu ametafuta nyenzo nyingi kadiri awezavyo kufikiria ili kutawanya magugu mbali. Amepata njia ya kuwafanya waingie katika hata utakatifu wa nyumba zetu wenyewe. Uovu na mambo ya kidunia umesambaa huko na kuonekana kama hakuna njia ya kuuondoa kabisa. Unakuja kwa njia ya televisheni, redio na tovuti, vyombo ambavyo vimeanzishwa kwa lengo la kuelimisha na kutuburudisha. Ngano na magugu vyote vimekua kwa pamoja. Mtu atunzaye shamba lazima, kwa nguvu zake zote, lazima akirutubishe kilicho bora na kukifanya kiwe imara na cha kupendeza ili magugu yasiwe na mvuto kwa macho au masikio. Sisi tumebarikiwa sana kama washiriki wa Kanisa la Bwana kwa kuwa na injili ya Mwokozi wetu kama msingi ambao tumejengwa.
Kutoka Kitabu cha Mormoni katika 2 Nefi tunasoma: “Kwani tazama, na tena ninakuambia kwamba kama utaingia kupitia mlango, na kupokea Roho Mtakatifu, itaonyeshwa kwako mambo yote ambayo unapaswa kutenda” (2 Nefi 32:5).
Tusiache kamwe kelele za ulimwengu zituzidi uwezo na kuishinda ile sauti tulivu na ndogo.
Bila shaka tumeonywa katika tukio ambalo tutakumbana nalo katika siku yetu. Changamoto zetu zitakuwa ni jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya tukio ambalo Bwana amesema hakika bado linakuja.
Wengi katika jamii yetu yenye wasiwasi wanaelewa kwamba kutokuwa waaminifu katika familia kunaweza kuleta huzuni na kukosa matumaini katika ulimwengu wenye shida. Kama washiriki wa Kanisa, tunajukumu la kutunza na kulinda familia ikiwa ni msingi wa muungano wa jamii na milele. Manabii wameonya na kutahadharisha juu ya madhara na majanga yasiyoepukika yatokanayo na kushuka kwa viwango vya familia.
Kadri ulimwengu unavyoendelea kutuangalia, acheni tuwe hakika kwamba mfano wetu ambao utawezesha na kusaidia mpango ambao Bwana aliutengeneza kwa ajili ya watoto Wake hapa duniani. Mafundisho yake makuu yalifanyika kwa mfano. Nyumba zetu lazima ziwe sehemu takatifu ili kustahimili misukumo ya ulimwengu. Kumbuka kwamba kikubwa zaidi ni baraka za Bwana zinazokuja na kupitia familia zenye haki.
Lazima tuendelee kwa makini kutathimini utendaji wetu kama wazazi. Mafundisho yaliyo na nguvu sana ambayo mtoto anaweza kuyapata yatatoka kwa baba na mama wenye haki. Kwanza tuangalie wajibu wa mama. Sikilizeni nukuu hii toka kwa Rais Gordon B. Hinckley:
“Wanawake wanaoifanya nyumba kuwa maskani wanatoa mchango mkubwa kwa jamii kuliko wale wanaoongoza jeshi kubwa au viongozi wa mashirika mazuri. Nani anaweza kuwa na ushawishi wa thamani kama ule wa mama kwa mtoto wake, bibi kwa vizazi vyake, au shangazi na dada katika familia zao?
“Hatuwezi kuanza kupima au kupiga hesabu za ushawishi wa wanawake, kwa njia zao wenyewe, huzijenga familia imara na huzitunza kwa ajili ya vizazi vizuri vya baadaye. Uamuzi uliofanywa na wanawake wa kizazi hiki utakuwa na matokeo ya milele. Naomba nishauri kwamba akina mama wa leo hawana nafasi muhimu na wala changamoto nyingi zaidi kuliko ile ya kuimarisha nyumba” (Standing for Something: 10 Neglected Virtues That Will Heal Our Hearts and Homes [2000], 152).
Sasa ngoja tuangalie wajibu wa baba katika maisha yetu:
Akina baba hutoa baraka na hutoa ibada takatifu kwa ajili ya watoto wao. Haya yatakuwa na alama ya kiroho katika maisha yao.
Akina baba wanajihusisha katika kuongoza sala ya familia, kusoma maandiko kila siku, na jioni ya familia ya kila wiki.
Akina baba hujenga desturi za familia kwa kujihusisha katika kusaidia kupanga safari za likizo ambazo zitawahusisha wanafamilia. Kumbukumbu za nyakati hizi muhimu haziwezi kusahaulika na watoto wao.
Akina baba huwa na mikutano ya ana kwa ana na watoto wao mmoja mmoja na kuwafundisha kanuni za injili.
Akina baba huwafundisha wana na binti zao thamani ya kufanya kazi na kuwasaidia wao kuanzisha malengo ya thamani katika maisha yao.
Akina baba huonyesha mfano wa utumishi mwema wa injili.
Tafadhali kumbukeni, ndugu, wito wenu mtakatifu kama baba katika Israeli---wito wenu mkubwa sasa na milele---wito ambao kamwe hamtapumzishwa.
Miaka mingi iliyopita katika mkutano wa kigingi, tulionyesha filamu kuelezea mada ya ujumbe tuliokuwa tunautoa. Katika miaka kadhaa, tulipokuwa tunatembelea makanisa katika majukumu yetu ya matembelezi ya mkutano wa kigingi, tuliijua vizuri ujumbe wa ile filamu. Hatuwezi kuunukuu wote kutoka moyoni. Ujumbe ulibaki katika mawazo yangu katika miaka yote hii. Filamu ilisimuliwa na Rais Harold B. Lee na ilielezea yaliyotokea katika nyumba ya binti yake. Inaelezea kama ifuatavyo:
Jioni moja mama wa nyumba alikuwa akijaribu sana kumalizia kujaza matunda kwenye chupa kwa ajili ya kuhifadhi. Mwishowe watoto wakawa tayari kulala na walikuwa sawa. Sasa ni wakati wa kutengeneza matunda. Alipojaribu kumenya na kutoa kokwa la tunda, wavulana wawili wakaja jikoni na kusema kwamba walikuwa tayari kwa ajili ya sala yao ya kwenda kulala.
Kwa kutotaka kusumbuliwa, mama alisema kwa haraka kwa wale wavulana, “Kwa nini msisali wenyewe pekee jioni ya leo na Mama aendelee kutengeneza matunda?”
Kijana mkubwa alisimama na kugoma kuondoka na akauliza, “Je, nini kilicho muhimu, maombi au matunda? (Ona Teachings of Presidents of the Church: Harold B. Lee [2000], 143–44.)
Wakati mwingine tunajikuta wenyewe katika hali ambayo tuna nafasi ya kuwafundisha watoto somo ambalo litakuwa na matokeo ya kudumu katika maisha yao ya ujana. Kwa hakika, maombi ni muhimu kuliko matunda. Mzazi mwenye mafanikio hastahili kukosa muda wa kutumia nafasi katika maisha ya mtoto wake wakati somo muhimu linaweza kufundishwa.
Ni Imani yangu thabiti kuwa hapajawahi kuwa na kipindi katika miaka yangu mingi ya maisha wakati watoto wa Baba yetu wa Mbinguni wamehitaji zaidi mkono wa mwongozo wa wazazi wema na waliojitolea. Tuna urithi wenye thamani ya wazazi wa kutoa karibu kila kitu walichonacho kutafuta sehemu ambayo tunaweza kulea familia zao kwa imani na ujasiri ili kizazi kijacho kiwe na nafasi kubwa zaidi ya zao. Lazima tuangalie kati yetu kwa roho ile ile ya ujasiri na kushinda changamoto tunazokumbana nazo kwa roho ile ile ya kujitolea. Lazima tuwekeze katika vizazi vijavyo tegemeo katika kufundisha injili ya Bwana na Mwokozi wetu.
“Na sasa, wana wangu, kumbukeni, kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu; kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, ndiyo, mishale yake kimbungani, ndiyo, wakati mvua yake ya mawe na dhoruba kali itapiga juu yenu, hautakuwa na uwezo juu yenu, hautakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye shimo la taabu na msiba usioisha, kwa sababu ya mwamba ambako kwake mmejengwa, ambao ni msingi imara, msingi ambako watu wote wakijenga hawataanguka” ” (Helamani 5:12).
Ni katika injili ya Yesu Kristo ambayo inaleta msingi huu ambao tunaweza kupata amani ya milele na kuijenga vitengo vya familia ya milele. Katika haya ninashuhudia katika jina la Bwana na Mwokozi wetu hata Yesu Kristo, amina.