2010–2019
Sakramenti na Upatanisho
Oktoba 2014


12:5

Sakramenti na Upatanisho

Agizo la sakramenti huhitaji kuwa takatifu na tukufu sana kwa kila mmoja wetu.

Katika mkesha wa Gethsemane na Kalivari, Yesu aliwakusanya Mitume Wake pamoja mara moja ya mwisho ili kuabudu. Mahali palikuwa chumba cha juu cha nyumba ya mfuasi katika Yerusalemu, na msimu ulikuwa wa Pasaka.1

Mbele yao ulikuwa mlo wa tamaduni ya Pasaka, ukijumuisha dhabihu ya mwanakondoo, divai, mkate usiyochachiwa, nembo za wokovu uliopita wa Israeli kutoka utumwani na kifo2 na ukombozi wa siku za usoni bado ulikuwa haujafanyika.3 Mlo ulipokuwa unaenda kumalizika, Yesu aliutwaa mkate, akaubariki na akaumega,4 na akawapatia Mitume Wake, akisema “Twaeni mle.”5 “Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”6 Vivi hivi Akatwaa kikombe cha divai, akakibariki na kukipitisha kwa wale wote waliokuwa karibu Naye, akisema: “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu,”7 “ambayo ilimwagwa … kwa ondoleo la dhambi.”8 “Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”9

Katika njia hii rahisi bali yenye umuhimu, Yesu alianzisha ibada mpya kwa watu wa agano wa Mungu. Haitakuwa tena damu ya mnyama kumwagwa au nyama ya mnyama kuliwa kwa matarajio ya dhabihu ya ukombozi ya Kristo ambaye bado angekuja.10 Badala yake, nembo za nyama iliyomegwa na damu iliyomwagwa ya Kristo ambaye tayari alikuwa amekuja zingepokelea na kuliwa katika ukumbusho wa dhabihu Yake ya ukombozi.11 Kushiriki katika ibada hii mpya kungedhihirisha kumkubali kabisa Yesu kama Kristo aliyeahidiwa kwa moyo mkunjufu kuwa tayari kumfuata na kuweka amri Zake. Kwa wale ambao wangekubali wangeonyesha na kuendesha maisha yao hivyo, kifo cha kiroho “kingewapita” wao, na uzima wa milele ungekuwa umehakikishwa.

Katika saa na siku zilizofuata, Yesu aliingia katika Gethsemane, akapelekwa Kalivari, na kwa ushindi akaondoka kutoka kwenye kaburi la Arimathaya. Baada ya kuondoka Kwake kutoka kwao, wanafunzi waaminifu wa Yesu katika na karibu na Yerusalemu walikuja pamoja katika siku ya kwanza ya wiki na “kumega mkate,”12na wakafanya “kwa uthabiti.”13 Kwa kweli, hawakufanya hivyo tu kumkumbuka Bwana wao mwendazake lakini kuonyesha shukrani kwa, na, imani katika Ukombozi Wake wa ajabu kwao.

Cha muhimu sana, Yesu alipowatembelea wanafunzi Wake katika Amerika, aliaanzisha sakramenti miongoni mwao.14 Kwa kufanya hivyo, Yeye alisema: “Na hii mtakumbuka kufanya daima”,”15na “Itakuwa ushuhuda kwa Baba kwamba daima mnanikumbuka.”16Tena, mwanzoni wa Urejesho, Bwana alianzisha ibada ya sakramenti, akitoa maelekezo kwetu sawa na yale Yeye alitoa kwa wanafunzi Wake wa mapema.17

Ibada ya sakramenti imeitwa “mojawapo wa ibada takatifu na tukufu za katika Kanisa.”18 Inapaswa kuwa takatifu na tukufu zaidi kwa kila mmoja wetu. Yesu Kristo Mwenyewe alianzisha ibada ya kutukumbusha kile Yeye alifanya ili kutukomboa na kutufundisha jinsi tunavyoweza kutumia wenyewe Ukombozi Wake na kwa hivyo kuishi tena na Mungu.

Kwa mkate uliovunjika na kumegwa, tunadhihirisha kwamba tunakumbuka mwili wa Yesu Kristo---mwili ambao uliteswa kwa maumivu, mapigo, na majaribu ya kina aina,19 mwili ambao ulibeba mzigo wa huzuni ya kutosha kuvuja damu katika kinyweleo,20mwili ambao nyama yake iliraruliwa na ambao moyo wake ulivunjwa katika kusulibiwa.21 Tunaonyesha imani yetu kwamba ingawa mwili huo huo ulilazwa katika kifo, uliinuka tena katika uzima kutoka kaburini kwa uwezo wa Ufufuko, kamwe tena hautajua ugonjwa, kuoza, au kifo.22Na kwa kula mkate kwetu wenyewe, tunakiri kwamba, kama vile mwili wa Kristo, miili yetu itafunguliwa kutoka kwa kamba za kifo, kuinuka kwa ushindi kutoka kwenye kaburi, na kurejeshwa kwa roho zetu za milele.23

Kwa kikombe kidogo cha maji, tunaonyesha kwamba tunakumbuka damu ya Yesu aliyomwagwa na kuteseka Kwake kuliompata kwa ajili ya wanadamu wote. Tunakumbuka huzuni ambayo ilisababisha matone makuu ya damu kumwagika katika Gethsemane.24 Tunakumbuka kuchubuliwa na kupigwa aliopata katika mikono ya walinzi Wake.25 Tunakumbuka damu Yake iliyomwagika kutoka kwenye mikono Yake, miguu, na ubavu katika Kalivari.26 Na tunakumbuka tafakari Yake ya kibinafsi kuhusu kuteseka Kwake: “Machungu namna gani hujui, makali namna gani hujui, ndiyo, namna gani magumu kuyavumilia hujui.”27 Kunywa maji kwetu, tunakiri kwamba damu Yake na kuteseka kulilipia dhambi zetu na kwamba Yeye ataondoa dhambi zetu tunapokumbatia na kukubali kanuni na ibada za injili Yake.

Kwa hivyo, kwa mkate na maji, tunakumbushwa Ukombozi wa Kristo kwetu kutokana na kifo na dhambi. Mfanyiko wa mkate kwanza na maji pili ni muhimu. Katika kupokea mkate, tunakumbushwa ufufuko wetu binafsi ambao lazima ufanyike, ambao unajumuisha zaidi kuliko tu urejesho wa mwili na roho. Kwa uwezo wa Ufufuko, sisi sote tutarejeshwa mbele ya Mungu.28Uhalisi huu unatuletea swali la msingi kwa maisha yetu. Swali la msingi linalotukabili si kama tutaishi, bali ni nani tunaishi baada ya sisi kufa. Ingawa kila mmoja wetu atarudi kwenye uwepo wa Mungu, sio kila mmoja wetu atabakia Naye.

Katika maisha ya duniani, kila mmoja wetu huchafuliwa na dhambi na uvunjaji amri.29 Tutakuwa tumekuwa na mawazo, maneno, na kazi ambazo hazikuwa njema.30 Kwa ufupi, tutakuwa wachafu. Na matokeo ya uchafu katika uwepo wa Mungu, Yesu alisema wazi kabisa: “Hakuna kitu kichafu kinaweza kukaa … katika uwepo wake.”31Uhalisi huo ulisemwa vyema na Alma Mdogo ambaye, wakati alikabiliwa na malaika mtakatifu, alizongwa sana, kusononeka, na kuteswa na uchafu wake kwamba alitamani “kutokuwepo kwa nafsi wala mwili, kwamba [yeye] asingeletwa kusimama kwenye uwepo wa ... Mungu.”32

Katika kupokea maji ya sakramenti, tunafunzwa jinsi tunavyosafishwa kutokana na dhambi na uvunjaji wa amri na basi kusimama katika uwepo wa Mungu. Kwa kumwaga damu yake isiyo na hatia, Yesu Kristo aliridhisha madai ya haki kwa kila dhambi na uvunjaji amri. Kisha Yeye akajitolea kututakasa kama tutakuwa na imani katika Yeye ya kutosha kutubu, kukubali maagizo na maagano yote ya wokovu, kuanzia na ubatizo na kupokea Roho Mtakatifu. Punde, tunapopokea Roho Mtakatifu, tunatakaswa na kusafishwa. Yesu Kristo alilelezea fundisho hili kwa uwazi kabisa:

“Na hakuna kitu kichafu kinachoweza kuingia kwenye ufalme wa [Mungu]. … Hakuna chochote ambacho huingia kwenye pumziko lake isipokuwa wale ambao wameosha nguo zao ndani ya damu yangu. …

“Sasa hii ndiyo amri: Tubuni nyinyi nyote katika sehemu zote za dunia, na mje kwangu na mbatizwe katika jina langu kwamba muweze kutakaswa kwa kupokea Roho Mtakatifu, ili msimame mbele yangu bila mawaa katika siku ya mwisho.”33

Hili ndilo fundisho la Kristo.34 Tunapopokea fundisho hili na kuendesha maisha yetu inavyopasa, tunatakaswa katika damu ya Kristo na kuwa wasafi.35

Kupitia sala za sakramenti, tunaonyesha kukubali kwetu hili fundisho la Kristo na sharti letu la kuishi kulingana nalo. Katika maombi yetu kwa Mungu Baba yetu wa Milele, tunatangaza kwamba “daima tutamkumbuka” Mwanawe mwenye thamani. Kwanza, tunashuhudia “utayari” wetu wa kukumbuka. Kisha tunashuhudia kwamba “tunakumbuka.” Kwa kufanya hivyo, tunafanya sharti la taadhima la kufanya imani katika Yesu Kristo na katika Ukombozi Wake kwetu kutoka kwa kifo na dhambi.

Tunatangaza zaidi kwamba “tutaweka amri Zake.” Hili sharti la taadhima la kutubu. Ikiwa mawazo yetu, maneno, au matendo yamekuwa chini ya kiwango cha kile tunapaswa kuwa katika siku zilizopita, tujiwekee sharti wenyewe la kuyaweka maisha yetu katika uwiano Naye katika siku zinazokuja.

Kisha, tunatangaza kwamba “tuko tayari kujichukulia juu yetu jina la Mwana.”36Hilo ni sharti la taadhima la kujiweka chini ya mamlaka Yake na kufanya kazi Yake, ambayo inajumuisha kupokea wenyewe kila agizo na agano la kuokoa.37

Tunapojiwekea sharti wenyewe kwa kanuni hizi, tunaahidi katika sala za sakramenti kwamba “daima tutakuwa na Roho Yake kuwa [nasi] .”38 Kupokea upya Roho ni baraka kuu, kwa sababu Roho ni wakala ambaye hututakasa na hutusafisha kutoka kwa dhambi na uvunjaji wa amri.39

Ndugu na kina dada, tukio muhimu sana katika nyakati na umilele ni Upatanisho wa Yesu Kristo. Yeye ambaye ndiye alikamilisha Upatanisho ametupa agizo la sakramenti ili kutusaidia sio tu kukumbuka bali pia kudai baraka zote za hili tendo kuu la neema. Ushiriki kwa kila mara na wa dhati katika hili agizo takatifu hutusaidia kuendelea kukumbatia na kuishi fundisho la Kristo baada ya ubatizo na kwa hivyo kufuatilia na kukamilisha mfanyiko wa utakaso. Kwa kweli, agizo la sakramenti hutusaidia kwa uaminifu kuvumilia hadi mwisho na kupokea ujalivu wa Baba katika njia ile ile Yesu alipokea, neema juu ya neema.40

Mimi natoa ushuhuda wa uwezo wa Yesu Kristo wa kutukomboa sisi sote kutoka kwa kifo na dhambi na nguvu za maagizo ya ukuhani Wake, ikijumuisha sakramenti, kututayarisha “kuuona uso wa Mungu, hata Baba wa Mbinguni, na kuishi.”41 Na tupokee sakramenti wiki ijayo, kila wiki baada ya hapo, kwa hamu ya kina na madhumuni ya dhati zaidi, mimi naomba katika jina la Bwana Yesu Kristo, amina.