Kuishi Injili kwa Furaha
Matumaini katika uwezo wa kuokoa wa Yesu Kristo; kuweka sheria na amri Zake. Katika maneno mengine ---kuishi injili kwa furaha.
Kina dada zangu wapendwa, marafiki zangu wapendwa na wafuasi wabarikiwa wa Yesu Kristo, nina shukrani kuwa na fursa hii ya kuwa nanyi tunapofungua mkutano mwingine mkuu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Wiki ijayo Urais wa Kwanza na mitume kumi na wawili watakutana na Wakuu Wenye Mamlaka na viongozi wakuu wa makundi saidizi, vikao vilivyobaki vya mkutano wetu mkuu duniani vitafuata Jumamosi na Jumapili. Ninashukuru zaidi kwa, Rais Thomas S. Monson, nabii wa Mungu kwa siku zetu, kwa kuniuliza niwakilishe Urais wa Kwanza ninapowazungumzia kina dada wa Kanisa.
Nilipotafakari kile ningeweza kusema, fikira zangu zilirudi kwa wanawake walioshawishi maisha yangu na kunisaidia kupita changamoto za duniani. Nina shukrani kwa bibi yangu ambaye miongo mingi iliyopita aliamua kupeleka familia yake kwa mkutano wa sakramenti wa Wamormoni. Nina shukrani kwa Dada Ewig, mwanamke mkongwe wa Kijerumani asiye na bwana, ambaye jina lake linatafsiri katika Kingereza kama “ Dada wa Milele.” Alikuwa ndiye aliyetoa aliko hili la kijasiri na zuri kwa bibi yangu. Nina shukrani sana kwa mama yangu, ambaye aliongoza watoto wanne kupitia shida za Vita Vya Dunia vya II. Ninafikiria pia juu ya binti yangu, wajukuu wangu, na vizazi vijavyo vya wanawake waaminifu ambao siku moja watakuja.
Na, bila shaka, nina shukrani milele kwa mke wangu, Harriet, ambaye alinivutia kama kijana, alibeba mzigo ulio mzito zaidi wa familia yetu changa kama mama, anayesimama nami kama mke, na anawapenda na kuwathamini watoto wetu, wajukuu, na vitukuu. Amekuwa ndiye nguvu katika nyumba yetu kwa nyakati nzuri na mbaya. Analeta furaha katika maisha ya wote wanaomjua.
Mwishowe, nina shukrani sana kwa kila mmoja wenu, mamilioni ya akina dada waaminifu duniani wa umri wowote ambao hufanya mengi sana ili kujenga ufalme wa Mungu. Nina shukrani kwenu ninyi kwa ajili ya njia nyingi ambazo mnainua, mnatunza, na kubariki wale walio karibu nanyi.
Mabinti wa Mungu
Ninafurahia kuwa miongoni mwa mabinti wengi wa Mungu . Tunapoimba wimbo “I Am a Child of God,” maneno yake hugusa mioyo yetu. Kutafakari ukweli huu----kwamba sisi ni watoto wa wazazi wa mbinguni1---hutujaza na hisia ya uasili, na hatima.
Ni vyema kukumbuka kwamba wakati wote wewe ni mtoto wa Mungu. Ufahamu huu utakupa nguvu wakati wa shida katika maisha yako na utakuvutia kutimiza mambo makubwa. Hata hivyo, ni muhimu pia kukumbuka kwamba kuwa binti wa wazazi wa milele sifa unayopata ama utakayopoteza kamwe. Daima na milele utabaki kuwa binti wa Mungu. Baba yako aliye Mbinguni ana matumaini makuu kwa ajili yako, lakini uasili wako mtukufu peke yake hauwezi kukuhakikishia urithi mtukufu. Mungu alikutuma hapa ili kujiandaa kwa ajili ya siku ijayo iliyo kuu kuliko chochote unachoweza kufikiria.
Baraka zilizoahidiwa za Mungu kwa waaminifu ni tukufu na za kuinua. Miongoni mwao ni viti vya enzi, falme, mamlaka, na nguvu, utawala, urefu wote na kina.”2 Na inafaa zaidi ya cheti cha kuzaliwa cha kiroho ama “Kadi ya Ushiriki kama Mtoto wa Mungu” kustahili baraka hizi kuu.
Lakini tunazipata vipi?
Mwokozi amejibu swali hili katika siku zetu:
“Isipokuwa mmetii sheria yangu, hamwezi kuufikia utukufu huu.
“Kwa maana mlango ni mwembamba, na na njia imesonga iongozayo kwenye kuinuliwa …
“… Ipokeeni, sheria yangu.” 3
Kwa sababu hii, tunazungumzia kutembea njia ya ufuasi.
Tunazungumzia utiifu kwa amri za Mungu.
Tunazungumzia kuishi injili kwa furaha, kwa moyo wetu wote, na kwa nguvu, akili na nafsi.
Mungu Anajua Kitu Ambacho Hatujui
Na hali kwa baadhi yetu, utiifu kwa amri za Mungu huwa hauhisi kufurahisha sana. Tukubali: huenda kuwa kuna baadhi zinazoonekana kuwa ngumu ama kutofurahisha---amri ambazo tunazichukulia na shauku ya mtoto ameketi mbele ya sahani ya mboga yenye afya lakini ya kuchukiwa. Sisi hujizatiti na kujilazimisha kuzingatia ili tuweze kuendelea na shughuli tunazopenda zaidi.
Pengine wakati kama hizi tunaweza kujipata tukiuliza, “Je, tunahitaji hakika kutii amri zote za Mungu?”
Jibu langu kwa swali hili ni rahisi:
Nafikiria Mungu anajua kitu ambacho hatujui! Vitu ambavyo vimo zaidi ya kiwango chetu cha kuelewa! Baba yetu wa Mbinguni ni kiumbe cha milele ambaye uzoefu wake, hekima, na uwezo wa kufikiria ni mkuu zaidi kuliko wetu. 4 Si hayo tu, lakini Yeye anapenda milele, ana huruma, na hulenga lengo letu la heri: kuleta kupita kutokufa kwetu na uzima wa milele. 5
Kwa maneno mengine, hajui tu kile kilicho bora kwa ajili yako; Yeye pia kwa wasiwasi anakutaka uchague kile kilicho bora kwako.
Ukiamini haya moyoni mwako---ikiwa unaamini kwa kweli lengo kuu la Baba yetu wa Mbinguni ni kuinua na kutukuza watoto Wake na kwamba Yeye anajua bora zaidi jinsi ya kufanya hivyo---je, si inafaa kukubaliana na kufuata amri Zake, hata zile zinazoonekana kuwa ngumu? Je, hatupaswi kuthamini vikingi vya mwanga alivyotoa vinavyotuongoza kupita gizani na majaribio ya duniani? Vina alamisha njia ya kurudi nyumbani kwetu mbinguni! Kwa kuchagua njia ya Baba wa Mbinguni, unaweka msingi wa kiungu kwa ajili ya maendeleo yako binafsi kama binti wa Mungu ambao utakubariki katika maisha yako yote.
Sehemu ya changamoto yetu ni, nadhani, kwamba sisi hufikiria kwamba Mungu amefungia baraka Zake zote katika wingu kubwa mbinguni, akikataa kutupa isipokuwa tuwiane na mahitaji magumu ya kiuzazi ambayo ameweka. Lakini amri haziko hivyo kamwe. Kwa ukweli, Baba wa Mbinguni anamwaga baraka juu yetu kila mara, Ni hofu yetu, shaka, na dhambi ambazo, kama mwavuli, zinazuia baraka hizi kutufikia.
Amri zake ni maelekezo ya upendo na msaada wa kiungu kwetu sisi ndio tuweze kufunga mwavuli, ili tuweze kupokea wingi wa baraka za mbinguni.
Tunahitaji kukubali kwamba amri za Mungu si tu orodha ndefu ya mawazo mazuri. Si mawazo mazuri ya maisha kutoka kwa blogi ya intaneti ama nukuu ya kuinua kutoka kwa bodi ya Pinterest. Ni mashauri ya Mungu, yaliyo na msingi kwenye kweli za milele, yaliyotolewa ili kuleta “amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”6
Hivyo basi tuna chaguo. Kwa upande mmoja, kuna maoni ya dunia pamoja nadharia yake inayobadilika milele na nia za kushuku. Kwa upande mwingine, kuna neno la Mungu kwa watoto Wake---hekima Yake ya milele, ahadi zake za hakika, na maelekezo yake ya upendo kwa ajili ya kurudi kwa uwepo Wake katika utukufu, upendo, na enzi.
Chaguo ni lako!
Muumba wa bahari, mchanga, na nyota nyingi milele anakufikia siku ya leo! Anatoa risipi kuu la furaha, amani na maisha ya milele!
Ili kustahili baraka hizi tukufu, lazima ujinyenyekeze, uwe na imani, uchukue juu yako jina la Kristo, umfuate kwa maneno na vitendo, na kwa uthabiti “usimame kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika maeneo yote .”7
Sababu ya Utiifu
Mara tu unapoelewa asili ya kweli ya Mungu na amri Zake, pia utajielewa vyema zaidi na lengo tukufu la uwepo wako. Pamoja na haya, motisha yako ya kufuata amri inabadilika, na kuwa hamu ya moyo wako kuishi injili kwa furaha.
Kwa mfano, wale wanaoona kuhudhuria mikutano ya Kanisa kama njia binafsi ya kuongeza upendo wao wa Mungu, kupata amani, kuinua wengine, kutafuta Roho, na kufanya upya kujitolea kwao kumfuata Yesu Kristo watapata uzoefu wa thamani zaidi kuliko wale ambao huhudhuria mikutano bila hamu ya kuwa hapo. Kina dada, nimuhimu sana tuhudhurie mikutano yetu ya Jumapili, lakini nina uhakika kwamba Baba yetu wa Mbinguni pia anajali zaidi kuhusu imani yetu na toba kuliko takwimu za mahudhurio.
Mfano mwingine:
Mama aliyekuwa na watoto wawili hivi majuzi alishikwa na tetekuwanga. Bila shaka, haikiuchukua muda mrefu kabla watoto wake kuugua pia. Kazi ya kujihudumia na kuwahudumia watoto wake peke yake ilikuwa nyingi sana kushinda kiasi kwa mama yule mchanga. Na, kwa hivyo, nyumba ambayo kawaida ilikuwa safi ikawa chafu. Sahani chafu zilijaa kwenye beseni la kuoshea vyombo, na nguo chafu zilijaa kila mahali.
Alipokuwa anang’ang’ana na watoto waliokuwa wanalia---na akitaka kulia mwenyewe---mlango wake ukabishwa. Ilikuwa walimu wake watembezi. Wangeona dhiki ya mama kijana. Wangeona nyumba yake, jikoni kwake. Wangesikia vilio vya watoto.
Sasa, kama dada hawawangejali tu kukamilisha matembelezi ya mwezi walio pangiwa, wangempa mama sahani ya biskuti, wakeleza kwamba walikuwa wamemkosa katika Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wiki iliyopita, na kusema kitu kama, “Tujulishe kama kuna kitu tunaweza kufanya!” Kisha kwa furaha wangeenda safarini, wakishukuru kwamba wako na asilimia ya mwezi mwingine.
Kwa bahati mzuri, kina dada hawa walikuwa wafuasi wa kweli wa Kristo. Walitambua mahitaji ya dada huyu na wakatumia talanta zao nyingi na uzoefu wao. Walitengeneza nyumba, wakaleta mwangaza na uwazi nyumbani, na wakaita rafiki alete chakula kilichohitajika sana. Wakati hatimaye walimaliza kazi yao na wakasema kwaheri, walimwacha mama yule kijana akiwa analia---machozi ya shukrani na upendo.
Kutoka wakati huo, fikira ya mama yule juu ya mafundisho utembelezi ilibadilika. “Ninajua,” alisema kwamba mimi si tu jambo la kufanya kwenye orodha ya vitu vya kufanya vya mtu fulani.”
Ndio, walimu watembelezi wanafaa kuwa waaminifu katika kutembelea familia zao kila mwezi, yote hayo bila kukosa “sababu” muhimu kabisa ya amri hiyo----kumpenda Mungu na wanadamu.
Tunapochukulia amri za Mungu na sehemu yetu ya kujenga ufalme kama kitu cha kutekeleza tu kwenye orodha ya vitu vya kufanya, tunakosa moyo wa ufuasi. Tunakosa ukuaji ambao huja kutoka kwa kuishi kwa furaha amri za Baba wa Mbinguni.
Kutembea kwenye njia ya ufuasi hakuhitaji kuwa uzoefu mbaya. Ni ‘utamu kushinda yote yaliyomatamu.”8 Si mzigo unaotushinda. Ufuasi huinua roho zetu na kutuliza mioyo yetu. Hutuvutia na imani, tumanini na hisani. Hujaza roho zetu na mwangaza katika wakati za giza na utulivu wakati wa huzuni.
Hutupa nguvu tukufu na furaha ya kudumu.
Kuishi Injili kwa Furaha
Wapendwa dada zangu katika injili, iwe uko na umri wa miaka 8 ama 108, kuna kitu kimoja ninatumaini utaelewa kwa kweli na kujua:
Unapendwa.
Unapendwa na wazazi wa mbinguni.
Muumba Mkuu na wa Milele wa mwangaza na maisha anakujua! Anakujali.
Ndio, Mungu anakupenda leo hii na wakati wote.
Hangoji kukupenda hadi ushinde upungufu wako na tabia mbaya. Anakupenda leo kwa ufahamu kamili wa mapambano yako. Anajua kwamba wewe humfikia Yeye kwa maombi ya moyo na tumaini. Anajua kuhusu nyakati ambapo umeshikilia imani iliyokuwa inapunguka na kuamini---hata katika giza kubwa. Anajua kuhusu mateso yako. Anajua kuhusu majuto yako kwa ajili ya wakati umepungukiwa ama kushindwa. Na bado anakupenda.
Na Mungu Anajua kuhusu mafanikio yako; ingawa yanaweza kuonekana kuwa madogo kwako, anatambua na kuthamini kila mmoja yao. Anakupenda kwa kujitolea kwa wengine. Anakupenda kwa kujitahidi na kusaidia wengine kuhimili shida zao---hata wakati unapambana na zako mwenyewe.
Anajua kila kitu kukuhusu. Anakuona vizuri----Anakujua ulivyo kwa kweli. Na anakupenda---leo na daima!
Je, unadhani inamjalisha kwa Baba yetu wa Mbinguni kama vipodoshi vyako, nguo, nywele, na makucha yako ni kamili? Je, unafikiri thamani yako kwake inabadilika kulingana na wafuasi wangapi unao kwenye Instagramu au Pinterest? Je, unafikiri anataka wewe usumbuke ama uhuzunike kwa sababu rafiki amekuacha kwa Facebook ama tritter? Je, unafikiri urembo wa nje ama umaarufu hufanya tofauti kidogo kabisa katika thamani yako kwa Yule aliyeumba ulimwengu?
Anakupenda si tu kwa ajili ya yule uliye siku hii ya leo, lakini pia kwa kuwa mtu wa utukufu na mwangaza unao uwezo na nai ya kuwa.
Zaidi ya vile ungewahi kamwe kufikiria, Anakutaka utimize hatima yako----kurudi nyumbani kwako mbinguni kwa heshima.
Ninashuhudiakwamba njia yakukamilisha haya ni kuweka tamaa za ubinafsi na matarajio yasiostahili juu ya madhabahu ya kujitolea na huduma. Kina dada, amini ni katika nguvu za kuokoa za Yesu Kristo; shikeni amri na sheria zake. Kwa njia nyingine, ishi injili kwa furaha.
Ninashuhudia kwamba mtapata kipimo kilichofanywa upya tena na kilichozidishwa cha upendo mwema wa Mungu katika maisha yenu; kwamba mtapata imani, bidii na uamuzi kujifunza amri za Mungu, kuzihifadhi katika mioyo yenu, na kuishi injili kwa furaha.
Ninaahidi kwamba unapofanya hivyo, utagundua nafsi yako iliyo bora zaidi--- utu wako wa kweli. Utagundua kile kinachomaanisha kwa kweli kuwa binti wa Mungu wa Milele, Bwana wa wema wote. Kwa haya ninashuhudia na kuwaachia baraka zangu kama Nabii wa Bwana, katika jina la Yesu Kristo, amina.