Njoo, Unifuate 2024
Uongofu Ndiyo Lengo Letu


“Uongofu Ndiyo Lengo Letu,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Uongofu Ndiyo Lengo Letu,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani 2024

Picha
baba na watoto wakimlisha mwana kondoo

Uongofu Ndiyo Lengo Letu

Dhumuni la kujifunza na kufundisha injili ni kuongeza uongofu wetu na kutusaidia tuwe zaidi kama Yesu Kristo. Kwa sababu hii, tunapojifunza injili, hatutafuti tu taarifa mpya; tunataka kuwa “kiumbe kipya” (2 Wakorintho 5:17). Hii inamaanisha kuwategemea Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ili watusaidie kuibadili mioyo yetu, mitazamo yetu, matendo yetu na asili yetu hasa.

Lakini aina ya kujifunza injili inayoimarisha imani yetu na kutuongoza kwenye muujiza wa uongofu haitokei yote kwa wakati mmoja. Inakwenda zaidi ya darasani mpaka kwenye moyo wa mtu binafsi na nyumbani. Inahitaji uthabiti, juhudi za kila siku ili kuelewa na kuishi injili. Uongofu wa kweli unahitaji ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu hutuongoza kwenye ukweli na hushuhudia juu ya ukweli huo (ona Yohana 16:13). Yeye huangaza akili zetu, anahuisha uelewa wetu na hugusa mioyo yetu kwa ufunuo kutoka kwa Mungu, chanzo cha ukweli wote. Roho Mtakatifu huitakasa mioyo yetu. Yeye huchochea ndani yetu hamu ya kuishi katika ukweli na Yeye hutunong’onezea njia za kufanya hili. Hakika, “Roho Mtakatifu … atatufundisha [sisi] mambo yote” (Yohana 14:26).

Kwa sababu hizi, katika juhudi zetu za kuishi, kujifunza na kufundisha injili, tunapaswa kwanza na zaidi ya yote tutafute wenzi wa Roho. Lengo hili linapaswa kutawala chaguzi zetu na kuongoza mawazo na matendo yetu. Tunapaswa kutafuta chochote kinachokaribisha ushawishi wa Roho na kukataa chochote kinachofukuzia mbali ushawishi huo—kwani tunajua kwamba kama tunaweza kuwa wenye kustahili uwepo wa Roho Mtakatifu, tunaweza pia kustahili kuishi katika uwepo wa Baba wa Mbinguni na Mwanaye, Yesu Kristo.

Chapisha