Agano la Kale 2022
Nyenzo za Ziada


“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili : Agano la Kale 2022 (2021)

“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Nyenzo za Ziada

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika app ya Makataba ya Injili kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Katika kuongezea kwenye matoleo yalilochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika app za Music na Gospel Media.

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo

Vitabu vya kiada vya seminari na chuo vinatoa chimbuko la kihistoria na fasili ya mafundisho kwa kanuni zinazopatikana katika maandiko. Vinaweza pia kuchochea mawazo ya kufundisha kwa ajili ya madarasa ya Shule ya Jumapili.

Magazeti ya Kanisa

Magazeti ya Liahona na Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana yanatoa makala na tarifa zingine ambazo zinaweza kuongezea kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili.

mtoto akijifunza nyenzo za Kanisa

Mada za Injili

Kwenye Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org) unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganisho kwenye nyenzo saidizi kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko, na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa majibu ya kina ya maswali ya injili na ya kihistoria.

Hubiri Injili Yangu

Mwongozo huu wa wamisionari hutoa muhtasari wa kanuni za msingi za injili.

Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (kijitabu)

Nyenzo hii inatoa muhtasari wa viwango vya Kanisa ambavyo vinaweza kutusaidia kuishi injili na kufurahia wenza wa Roho. Unaweza kuirejelea mara kwa mara, hasa ikiwa unawafundisha vijana.

Video na Sanaa

Sanaa za mchoro, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazohusiana na maandiko. Tembelea Gospel Media katika MediaLibrary.ChurchofJesusChrist.org ili kupitia pitia mkusanyiko wa nyenzo za habari za Kanisa. Gospel Media pia inapatikana kama app ya simu ya mkononi. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kutumiwa katika mikutano ya baraza la walimu.