“Somo la 13: Hali ya Hewa,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 13,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 13
Weather
Shabaha: Nitajifunza kuuliza na kujibu maswali kuhusu hali ya hewa.
Personal Study
Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Love and Teach One Another
Pendaneni na Fundishaneni
I can learn from the Spirit as I love, teach, and learn with others.
Ninaweza kujifunza kutoka kwa Roho ninapowapenda, kuwafundisha na kujifunza pamoja na wengine.
Mungu anayo mambo makubwa ambayo Yeye anataka kutufundisha sisi. Yeye anaweza kuzidisha uwezo wetu wa kujifunza kupitia RohoWake. Tunamwalika Roho tunapopendana na kusikilizana. Mungu hutufundisha sisi jinsi inavyokuwa wakati tunapojifunza kwa njia ya Roho:
“Yule ambaye hulipokea neno kwa njia ya Roho wa kweli hulipokea kama vile lifundishwavyo na Roho wa kweli[.] Kwa sababu hiyo, yule ambaye huhubiri na yule apokeaye, huelewana, na wote hujengana na kufurahi kwa pamoja” (Mafundisho na Maagano 50:21–22).
Tunaweza kujua Mungu anatufundisha wakati tunapomsikia Roho na kuhisi kujengwa. Roho huleta hisia za upendo, shangwe na amani. Kila mmoja wetu anaweza kutengeneza mazingira ambayo Roho anaweza kufundisha. Tunapotafuta kujifunza kwa njia ya Roho, Mungu anaweza kutusaidia kuelewana na kujihisi shangwe pamoja. Unapojifunza pamoja na kikundi chako cha EnglishConnect, tambua wakati unapojifunza kwa Roho. Tafuta kuwa na Roho mara nyingi zaidi.
Ponder
-
Ni lini ulihisi kujengwa na uzoefu wako katika EnglishConnect?
-
Je, unaweza kufanya nini ili kutengeneza mazingira ya kujifunza kwa njia ya Roho?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno kutoka kwenye sehemu ya “Memorize Vocabulary” katika mazoezi yako ya kila siku.
Will it … ? |
ita … ? |
Will it be … ? |
itakuwa … ? |
in Mexico |
huko Mexico |
Days
today |
leo |
tomorrow |
kesho |
on Monday* |
mnamo Jumatatu* |
Verbs/Verbs + ing
hail/hailing |
mvua ya mawe/kunyesha mvua ya mawe |
rain/raining |
mvua/mvua kunyesha |
snow/snowing |
theluji/kuanguka kwa theluji |
Adjectives
nice |
nzuri |
cold |
baridi |
hot |
joto |
cloudy |
hali ya mawingu |
foggy |
hali ya ukungu |
rainy |
hali ya mvua |
snowy |
hali ya theluji |
stormy |
hali ya tufani |
sunny |
hali ya jua |
windy |
hali ya upepo |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: What’s the weather in London?A: It’s (adjective) in London.
Examples
Q: What’s the weather in London?A: It’s rainy in London.
Q: What’s the weather in Toronto?A: It’s snowing in Toronto.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kufanya shughuli ya 1 na ya 2 za kikundi cha mazungumzo kabla ya kikundi chako kukutana.
Q: Will it (verb) (day)?A: No, it won’t (verb) (day).
Examples
Q: Will it snow tomorrow?A: No, it won’t snow tomorrow.
Q: Will it be sunny tomorrow?A: No, it won’t. It will snow tomorrow.
Q: Will it be nice on Friday?A: Yes, it will.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanyia mazoezi mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama chati. Uliza na ujibu maswali kuhusu hali ya hewa kwa kila siku. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: Will it be sunny on Monday?
-
B: No, it won’t be sunny on Monday.
-
A: What’s the weather on Monday?
-
B: It will be cloudy on Monday.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Uliza na kujibu maswali kuhusu hali ya hewa katika eneo lako. Zungumza kuhusu hali ya hewa ya kila siku ya wiki. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.
Example
-
A: What’s the weather in Bogotá?
-
B: It’s cloudy in Bogotá.
-
A: Will it be cloudy tomorrow?
-
B: Yes, it will.