“Somo la 16: Chakula,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 16,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 16
Food
Shabaha: Nitajifunza kuzungumza kuhusu milo na kwa nini mtu anapenda chakula hicho.
Personal Study
Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Take Responsibility
Wajibika
I have the power to choose, and I am responsible for my own learning.
Nina uwezo wa kuchagua, na ninawajibika kwa ajili ya kujifunza kwangu mwenyewe.
Yesu Kristo alishiriki hadithi kuhusu mtu tajiri ambaye alitoa fedha fulani kwa watumishi watatu. Watumishi wawili wa kwanza walitumia fedha kwa hekima na kuzalisha. Mtumishi wa tatu alikuwa na uoga. Alizificha fedha ili kwamba yeye asije akaipoteza. Mtu yule tajiri alihuzunishwa na yule mtumishi wa tatu lakini alifurahishwa na wawili wa kwanza. Aliwaambia watumishi wawili wa kwanza.
“Vema, mtumishi mwema na mwaminifu: umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakufanya kuwa mtawala juu ya mambo mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako” (Mathayo 25:21).
Fikiria kuhusu karama ambazo Baba wa Mbinguni amekupatia. Pengine umepatiwa uwezo wa kujifunza vyema au kuwa na subira na wengine. Unaweza kuwa na imani kubwa au ujasiri wa kuzungumza. Wajibika kwa ajili ya karama hizi na uzikuze. Fikiria jinsi ya kuzitumia ili kuwasaidia wengine. Pia, unaweza kuchagua kukuza karama mpya. Unaweza kutafuta karama za kiroho kwa kutumia imani katika Mungu, ukifanyia mazoezi, na kuzitumia ili kuwasaidia wengine. Mungu atakuongoza pale unapotafuta kukuza karama zako.
Ponder
-
Je, Karama zako ni zipi?
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia karama zako ili kujifunza Kiingereza?
-
Ni kwa jinsi gani karama hizi zinaweza kuwasaidia marafiki zako katika EnglishConnect?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutengeneza kadi za kuandika ili kukusaidia kukariri maneno mapya. Unaweza kutumia karatasi au aplikesheni.
food/foods |
chakula/vyakula |
eat/eats |
kula/hula |
Nouns 1
breakfast |
kifungua kinywa |
lunch |
chakula cha mchana |
dinner |
chakula cha usiku |
Nouns 2
fruit |
tunda |
apple/apples |
tufaa/matufaa |
vegetables |
mboga |
carrot/carrots |
karoti/karoti |
meat |
nyama |
chicken |
kuku |
egg/eggs |
yai/mayai |
pork |
nyama ya nguruwe |
beans |
maharage |
bread |
mkate |
rice |
mchele |
Adjectives
bland |
sio na ladha |
delicious |
ladha ya kupendeza |
sweet |
tamu |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: What do you eat for (noun 1)?A: I eat (noun 2) for (noun 1).
Examples
Q: What do you eat for breakfast?A: I eat eggs for breakfast.
Q: What do they eat for dinner?A: They eat rice and beans for dinner.
Q: What does he eat for lunch?A: He eats chicken, bread, and an apple for lunch.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kujifunza zaidi kuhusu mipangilio katika somo hili. Fikiria kutumia vitabu vya sarufi au tovuti.
Q: What food do you like?A: I like (noun 2) because it’s (adjective).
Examples
Q: What food do you like?A: I like apples because they’re sweet.
Q: What food doesn’t she like?A: She doesn’t like rice because it’s bland.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila mtu hula nini kama kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula ya jioni. Chukueni zamu.
New Vocabulary
filling |
ya kushibisha |
gross |
kisichovutia |
salty |
enye chumvi nyingi |
spicy |
enye viungo vingi |
cheese |
jibini |
fish |
samaki |
Example: Cary
-
Breakfast: fruit and bread
-
Lunch: chicken and vegetables
-
Dinner: fish
-
A: What does Cary eat for breakfast?
-
B: She eats fruit and bread for breakfast.
Image 1: Tim
-
Breakfast: eggs and bread
-
Lunch: chicken
-
Dinner: meat, vegetables, and bread
Image 2: Pele
-
Breakfast: cheese and bread
-
Lunch: beans and rice
-
Dinner: fish, rice, and fruit
Image 3: Mari
-
Breakfast: vegetables and rice
-
Lunch: pork, vegetables, and rice
-
Dinner: eggs, vegetables, and rice
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Part 1
Uliza na ujibu maswali kuhusu wewe na familia yako mnakula nini kama kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni. Chukueni zamu.
Example
-
A: What do you eat for lunch?
-
B: I eat rice and beans for lunch.
Part 2
Uliza na ujibu maswali kuhusu ni chakula gani wewe na familia yako mnapenda au hamkipendi. Sema kwa nini. Chukueni zamu.
Example
-
A: What food do you like?
-
B: I like carrots because they’re sweet. I like bread because it’s delicious.
-
A: What food don’t you like?
-
B: I don’t like cheese because it’s gross. I don’t like fish because it’s salty.
-
A: What food does your sister like?
-
B: She likes rice because it’s filling.