Msingi
Majukumu


Picha
mwanamke akiwafundisha watoto

Wito Wangu kama Mshauri katika Urais wa Darasa la Watoto

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Darasa la Watoto

Darasa la Watoto huwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni; kujifunza kuhusu mpango Wake wa furaha; kuishi injili ya Yesu Kristo; na kuhisi, kutambua na kutenda kulingana na ushawishi wa Roho Mtakatifu. Darasa la Watoto pia ni wasaa wa kujiandaa kwa ajili ya, na kuweka na kushika maagano matakatifu wakati watoto wakishiriki kwenye kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho12.1.)

Washauri

Urais wa Darasa la Watoto huwasaidia wazazi kuwaandaa watoto kuingia na kuendelea kwenye njia ya agano. Hili ni moja ya majukumu yao muhimu sana. Urais husimamia Darasa la Watoto, uhudumu kwa kila mtoto, waalimu na viongozi, na kusimamia mahitaji ya kiutendaji ya Darasa la Watoto. (Ona 12.3:2.)

Madarasa ya Watoto na Muda wa Kuimba.

Ni fursa takatifu kuwafundisha watoto. Viongozi wa Darasa la Watoto huwapenda na huwafundisha watoto katika njia ya Mwokozi. Madarasa ya Watoto hupangwa kulingana na umri na idadi ya walimu waliopo (ona 12.1.3). Muda wa kuimba huwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni na kujifunza kuhusu mpango Wake wa furaha (ona 12.1.4).

Mikutano na Mabaraza

Rais na washauri wake hukutana mara kwa mara. Pia huwa na mikutano pamoja na askofu au mshauri aliyepewa jukumu. (Ona 12.3:2.)

Walimu na Viongozi

Kuwafundisha watoto ni fursa takatifu. Urais wa Darasa la Watoto hutoa msaada kwa walimu wa Darasa la Watoto na viongozi wakati wa madarasa, darasa la watoto wadogo na muda wa kuimba (ona 12.3.5). Urais wa Darasa la Watoto hupendekeza kwa askofu wanaume na wanawake kutumikia kwenye miito kwenye Darasa la Watoto na la watoto wadogo.

Shughuli za Darasa la Watoto

Viongozi wa shughuli za Darasa la Watoto hupanga shughuli jumuishi na za kufurahisha ambazo husaidia kwenye kuikamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Huduma na shughuli zinapaswa kujenga shuhuda, kuimarisha familia na kutoa fursa za kuwabariki wengine. Shughuli za Darasa la Watoto kwa kawaida hufanyika mara mbili kwa mwezi kwa watoto wenye umri wa miaka 8–11. (Ona 12.3:6.)

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusiana na watoto wenye uhitaji maalum, usalama, programu ya Watoto na Vijana, na mengine hupatikana sehemu ya 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha