Muungano wa Usaidizi
Majukumu


Picha
kundi la watu wakitabasamu

Wito wangu kama Mshauri katika Urais wa Muungano wa Usaidizi

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kutumikia katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Muungano wa Usaidizi

Muungano wa Usaidizi ni kikundi kilichonzishwa kwa utakatifu kwa ajili ya wanawake wote watu wazima katika Kanisa. Muugano wa Usaidizi unawasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba lengo la Muungano wa Usaidizi ni “kuokoa nafsi na kupunguza mateso”—kutoa faraja ya Mwokozi (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 9.1).

Washauri

Rais na washauri wake wanawasimamia akina dada wanaohudumu, mafundisho ya Jumapili, na shughuli. Wanawafundisha akina dada majukumu yao ya agano, kuwaandaa wasichana kushiriki katika Muungano wa Usaidizi, na kuratibu juhudi za kuwaimarisha akina dada vijana wakubwa (ona 9.4). Urais wa Muungano wa Usaidizi na katibu hukutana mara kwa mara (ona 9.3.2.3).

Uongozi na Mabaraza

Viongozi wa Muungano wa Usaidizi hupanga mikutano ya Jumapili, shughuli, uhudumiaji, na michangamano mingine ili kuwapa wanawake uzoefu katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Washiriki wa Muungano wa Usaidizi na Akidi ya Wazee hufanya kazi kwa umoja (ona 9.2).

Muungano wa Usaidizi na Akidi ya Wazee

Urais wa Muungano wa Usaidizi na akidi ya wazee huratibu majukumu ya uhudumiaji na kusaidia kuongoza kazi ya hekaluni na historia ya familia na juhudi za kuwaalika wote kupokea baraka za injili. Pia wana jukumu muhimu katika kuwafundisha waumini wa kata kanuni za kuwahudumia wale wenye uhitaji, kuishi sheria ya mfungo, kukuza kujitegemea, na kuongeza utayari binafsi na wa familia (ona 22.6.2).

Mikutano ya Jumapili

Muungano wa Usaidizi hukutana Jumapili ya pili na ya nne kwa lengo la kuongeza imani katika Yesu Kristo, kujenga umoja, na kuimarisha familia na nyumba. Mikutano huanza kwa sala na hujumuisha muda kwa ajili ya kushauriana pamoja na mafundisho na majadiliano kulingana na mazungumzo ya mkutano mkuu wa hivi karibuni (ona 9.2.1.2).

Huduma na Shughuli

Urais wa Muungano wa Usaidizi wanaweza kupanga shughuli za kuimarisha imani ya akina dada katika Yesu Kristo, kuongeza tamanio lao la kufanya na kushika maagano, na kuwapa fursa za kuhudumu pamoja. Rais anasimamia shughuli hizi na anaweza kumwomba mshauri au dada mwingine kuongoza katika kupanga na kuzitekeleza (ona 9.2.1.3).

Miongozo na Sera

Miongozo ya Ziada na Sera zinapatikana katika sehemu ya 9.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha