Wito Wangu kama Mshauri wa Darasa la Watoto katika Kigingi
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Madhumuni ya Darasa la Watoto
Darasa la Watoto huwasaidia watoto wahisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni; wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha; waishi injili ya Yesu Kristo; na watambue na watende, juu ya ushawishi wa Roho Mtakatifu. Darasa la Watoto pia ni wakati wa kujiandaa, kufanya na kushika maagano matakatifu pale watoto wanaposhiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 12.1.)
Mshauri wa Darasa la Watoto katika Kigingi
Washauri wa Darasa la Watoto wanahudumu katika urais wa Darasa la Watoto katika Kigingi. Washiriki wa urais wanayo majukumu mengi ambayo hujumuisha kusaidia urais wa kigingi, kuhudumu katika baraza la kigingi (rais pekee), kuwatambulisha urais mpya ulioitwa katika kata, kutoa msaada endelevu na maelekezo , na kutembelea madarasa ya kata katika kigingi. Wanapoalikwa, wanaweza kuhudhuria mikutano ya mabaraza ya uratibu na kuzungumza katika mkutano wa sakramenti na mazingira mengineyo (ona 6.7.1).
Mikutano na Mabaraza
Urais wa Darasa la Watoto wanapaswa kushauriana pamoja mara kwa mara. Wanaweza kualikwa kuhudumu kwenye mabaraza mengine ya ziada. (Ona 6.7.1.1.)
Shughuli za Watoto
Urais wa Watoto katika kigingi mara chache wanaweza kupanga shughuli za watoto ngazi ya kigingi kwa ajili ya watoto walio na umri wa miaka 8 hadi 11. Shughuli hizi zinaweza kuwa kwa ajili ya wavulana , wasichana au wote (ona 6.7.1.3).
Miongozo na Sera
Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildrekatika n.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu watoto walio na mahitaji maalumu, masharti ya usalama, programu ya Watoto na Vijana na vinginevyo vinapatikana katika sehemu ya 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.