Wasichana
Majukumu


wasichana wakitabasamu

Wito wangu kama Mshauri katika Urais wa Wasichana

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Kusudi la Muundo wa Kikundi cha Wasichana

Muundo wa kikundi cha Wasichana huwasaidia mabinti wapendwa wa Mungu kujiandaa kurudi kwenye uwepo Wake. Huwasaidia wasichana kuweka na kushika maagano matakatifu na kuimarisha uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Kwenye madarasa yao, wasichana huwahudumia wengine, hutimiza majukumu yao ya kimaagano, hujenga umoja na hujifunza na kuishi mafundisho. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 11.1.1.)

Washauri

Rais na washauri huwahudumia wasichana wakati wakielekea kuwa wafuasi wa Mwokozi maisha yao yote. Huwafundisha urais wa madarasa kuhusu majukumu yao na kutoa msaada (ona 11.3.2). Washauri pia humsaidia rais kwenye upande wa kumbukumbu, ripoti na masuala ya kifedha.

Uongozi wa Vijana

Urais wa Wasichana huwasaidia viongozi wa vijana. Marais wa madarasa hujumuishwa kwenye baraza la vijana. Urais wa madarasa huongoza na kuhudumu kwa wasichana wakati wakisogea karibu na Mwokozi na kushiriki kwenye kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Kwa msaada wa viongozi watu wazima, wanapanga aina za huduma, shughuli na mikutano ya Jumapili (ona 11.3.4.2).

Madarasa ya Jumapili

Uaskofu na viongozi watu wazima wa Wasichana kwa sala huamua jinsi ya kupanga madarasa kulingana na umri. Hutilia maanani fursa za uongozi kwa wasichana. Kila darasa, bila kujali ukubwa, hupaswa kuwa na rais na, pale inapowezekana, mshauri mmoja au wawili na katibu (ona 11.1.3).

Huduma na Shughuli

Urais wa madarasa, ukisaidiwa na viongozi watu wazima, hupanga huduma na shughuli ambazo hujenga shuhuda, huimarisha familia, huendeleza umoja na hutoa fursa za kuwabariki wengine (ona 11.2.1.3). Huduma na shughuli ni fursa ya kuwakusanya vijana na kushiriki shangwe ya kuishi injili na kujishughulisha kwenye kazi kuu ya Bwana.

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo ya ziada na sera kuhusiana na wasichana wenye ulemavu, nembo za vijana na zaidi hupatikana katika sehemu ya 11.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.