Msingi
Majukumu


Picha
mwanamke akiwafundisha watoto

Wito wangu kama Katibu wa Watoto

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Darasa la Watoto

Darasa la Watoto linasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kujifunza kuhusu mpango Wake wa furaha, kuishi injili ya Yesu Kristo; na kuhisi, kutambua na kutendea kazi ushawishi wa Roho Mtakatifu. Darasa la Watoto pia ni wakati wa kujitayarisha kwa ajili ya kufanya na kushika maagano matakatifu wakati watoto wakishiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 12.1.)

Katibu

Katibu wa Watoto husaidia urais kwa mahitaji ya kiutawala. Katibu hufanya urais uwafahamu watoto wapya na wageni, watoto wanaostahili kubatizwa na upandaji wa madarasa. Husaidia kupanga kazi na kutayarisha ajenda za mikutano ya Watoto ya Jumapili na kuhudhuria mikutano. Katibu pia hufanya kazi kwa karibu na walimu wa Watoto na walimu wa chekechea juu ya masuala yanayohusiana na watoto. (Ona 12.3:3.)

Madarasa na Muda wa Kuimba.

Ni heshima takatifu kufundisha watoto. Viongozi wa Watoto huwapenda na kufundisha watoto katika njia ya Mwokozi. Madarasa ya Watoto hupangwa kwa umri na kwa idadi ya walimu waliopo (ona 12.1.3). Muda wa kuimba unawasaidia watoto wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha (ona 12.1.4).

Shughuli ya Watoto

Viongozi wa shughuli za watoto hupanga shughuli za kuburudisha na jumuishi ambazo zinasaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Huduma na shughuli zinapaswa kujenga shuhuda, kuimarisha familia na kutoa fursa za kuwabariki wengine. Shughuli za Watoto kwa ujumla hufanyika mara mbili kwa mwezi kwa watoto umri wa miaka 8–11. (Ona 12.3:6.)

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusiana na watoto wenye mahitaji maalumu, mahitaji ya usalama, programu ya Watoto na Vijana na nyinginezo vinapatikana katika sehemu ya 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha