Muungano wa Usaidizi
Majukumu


Picha
kundi la watu wakitabasamu

Wito Wangu kama Rais wa Muungano wa Usaidizi

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kutumikia katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu kwa ajili ya wito wako.

Lengo la Muungano wa Usaidizi

Muungano wa Usaidizi ni taasisi iliyoanzishwa chini ya maongozi ya kiungu kwa ajili ya wanawake wote watu wazima ndani ya Kanisa. Muungano wa Usaidizi unawasaidia watoto wa Mungu kujiandaa kurudi katika uwepo Wake. Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba lengo la Muungano wa Usaidizi ni “kuokoa nafsi na kupoza mateso”—kutoa msaada wa Mwokozi (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 9.1).

Rais wa Muungano wa Usaidizi

Rais wa Muungano wa Usaidizi huongoza jitihada za kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Anatumikia kama muumini wa baraza la kata na, chini ya mwongozo wa askofu, anashauriana na waumini watu wazima wa kata. Pia anasimamia kumbukumbu, ripoti na fedha (ona 9.3.2.2).

Urais

Rais na washauri wake husimamia akina dada wahudumu, maelekezo ya Jumapili na shughuli. Huwafundisha akina dada majukumu yao ya kimaagano, kuwaandaa wasichana kushiriki katika Muungano wa Usaidizi na kuratibu juhudi za kuwaimarisha akina dada waliofikia utu uzima (ona 9.4). Urais wa Muungano wa Usaidizi na katibu hukutana mara kwa mara (ona 9.3.2.3).

Uongozi na Mabaraza

Viongozi wa Muungano wa Usaidizi hupanga mikutano ya Jumapili, shughuli, kuhudumia, huduma na mchangamano mwingine ili kuwapa wanawake uzoefu katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Washiriki wa Muungano wa Usaidizi na akidi ya wazee hufanya kazi kwa umoja (ona 9.2).

Muungano wa Usaidizi na Akidi ya Wazee

Urais wa Muungano wa Usaidizi na wa akidi ya wazee huratibu majukumu ya kuhudumia na kusaidia kuongoza katika kazi ya hekalu na historia ya familia na jitihada za kuwaalika wote kupokea baraka za injili. Pia wana jukumu muhimu la kufundisha waumini wa kata kanuni za kuhudumu kwa wale wenye mahitaji, kuishi sheria ya mfungo, kujenga kujitegemea na kuongeza utayari binafsi na wa familia (ona 22.6.2).

Mikutano ya Jumapili

Muungano wa Usaidizi hukutana kila Jumapili ya pili na ya nne kwa lengo la kuongeza imani katika Yesu Kristo, kujenga umoja na kuimarisha familia na nyumba. Mikutano huanza kwa sala na hujumuisha muda wa kushauriana kwa pamoja na maelekezo na mjadala wa kiinjili vinavyoendana na mahubiri ya mkutano mkuu ya hivi karibuni (ona 9.2.1.2).

Huduma na Shughuli

Urais wa Muungano wa Usaidizi wanaweza kupanga shughuli ili kuimarisha imani ya akina dada katika Yesu Kristo, kuongeza hamu yao ya kufanya na kutunza maagano na kuwapa fursa ya kutumikia kwa pamoja. Rais husimamia shughuli hizi na anaweza kumwomba mshauri wake au dada mwingine kuchukua jukumu la kuzipanga na kuzitekeleza (ona 9.2.1.3).

Miito ya Ziada

Askofu na rais wa Muungano wa Usaidizi wanajadili hitaji la miito ya ziada. Miito hii hujumuisha waalimu, waratibu huduma, waratibu shughuli, wasaidizi na wajumbe wa kamati, makatibu wasaidizi na makatibu wa kuhudumia. Kama itahitajika, urais unaweza kuwapangia akina dada kusaidia katika juhudi za Muungano wa Usaidizi katika njia nyinginezo (ona 9.3.4).

Miongozo na Sera

Miongozo ya ziada na sera vinapatikana katika sehemu ya 9.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha