Wito Wangu kama Katibu wa Muungano wa Usaidizi
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumui ya wito wako.
Dhumuni la Muungano wa Usaidizi
Muungano wa Usaidizi ni kikundi kitakatifu kilichoanzishwa kwa ajili ya wanawake watu wazima wote katika Kanisa. Muugano wa Usaidizi unawasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba dhumuni la Muungano wa Usaidizi ni “kuokoa nafsi na kuondoa mateso”—kutoa faraja ya Mwokozi (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 9.1).
Katibu
Urais wa Muungano wa Usaidizi na katibu hukutana mara kwa mara (ona 9.3.2.3). Majukumu ya katibu yanaweza kujumuisha kuandaa ajenda kwa ajili ya vikao na kuandika kumbukumbu katika vikao, kufuatilia majukumu, kupanga mahojiano ya uhudumiaji, kutunza mahudhurio, kutuma ripoti, kusaidia kuandaa bajeti ya mwaka na kufuatilia matumizi (ona 9.3.3). Makatibu wasaidizi na katibu wa uhudumiaji wanaweza kuitwa ili kumsaidia katibu (ona 9.3.4).
Uongozi na Mabaraza
Viongozi wa Muungano wa Usaidizi wanapanga mikutano ya Jumapili, shughuli, utumishi, huduma, na michangamano mingine ili kuwapa wanawake uzoefu katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Washiriki wa Muungano wa Usaidizi na akidi ya wazee hufanya kazi kwa umoja (ona 9.2).
Mikutano ya Jumapili
Muungano wa Usaidizi hukutana Jumapili ya pili na ya nne kwa dhumuni la kukuza imani katika Yesu Kristo, kujenga umoja, na kuimarisha familia na nyumba. Mikutano huanza kwa sala na hujumuisha muda wa kushauriana pamoja na maelekezo ya injili na majadiliano kulingana na hotuba za mkutano mkuu wa hivi karibuni (ona 9.2.1.2).
Huduma na Shughuli
Muungano wa usaidizi unaweza kupanga shughuli ili kuimarisha imani za akina dada katika Yesu Kristo, kukuza matamanio yao ya kufanya na kushika maagano, na kuwapa fursa za kuhudumu pamoja. Rais anasimamia shughuli hizi na anaweza kumwomba mshauri au dada mwingine kuongoza katika kupanga na kutekeleza (ona 9.2.1.3).
Miongozo na Sera
Miongozo ya ziada na sera zinapatikana katika sehemu ya 9.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.