Wito wangu kama Rais wa Watoto wa Kigingi
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Madhumuni ya Darasa la Watoto
Darasa la Watoto huwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni; kujifunza kuhusu mpango Wake wa furaha; kuishi injili ya Yesu Kristo; na kuhisi, kutambua na kutenda juu ya ushawishi wa Roho Mtakatifu. Darasa la Watoto pia ni wakati wa kujiandaa, kufanya na kuweka maagano matakatifu pale watoto wanaposhiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 12.1.)
Rais wa Watoto wa Kigingi
Rais wa Watoto wa Kigingi anahudumu chini ya maelekezo ya urais wa kigingi. Anahudumu kama mshiriki wa baraza kuu la kigingi. Rais anaongoza urais wa Watoto wa kigingi. Kama urais, majukumu ni pamoja na kuelekeza urais mpya wa Watoto ulioitwa, kutoa msaada na maelekezo yanayoendelea, na kutembelea madarasa ya kata katika kigingi. Wanapoalikwa, wanaweza kuhudhuria mikutano ya baraza na kuzungumza katika mikutano ya sakramenti na maeneo mingine (ona 6.7.1).
Mikutano na Mabaraza
Urais wa Watoto wa kigingi unapaswa kushauriana pamoja mara kwa mara. Rais anahudhuria mikutano ya vigingi ya uongozi kila mwaka (ona29.3.4), anahudumu kwenye baraza la kigingi, na anahudhuria mikutano ya baraza la kuratibu wakati anapoalikwa na Sabini wa Eneo (ona 29.4).
Shughuli za Watoto
Urais wa Watoto wa kigingi mara chache unaweza kuratibu shughuli za kigingi kwa ajili ya watoto wa miaka 8 mpaka 11. Shughuli hizi zinaweza kuwa kwa ajili ya wasichana, wavulana au wote (ona 6.7.1.3).
Miongozo na Sera
Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu watoto walio na mahitaji maalumu, mahitaji ya usalama, mpango wa Watoto na Vijana na vinginevyo vinapatikana katika sehemu ya 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.