Shule ya Jumapili
Majukumu


kundi la watu wakitabasamu

Wito wangu kama Rais wa Shule ya Jumapili

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Kusudi la Shule ya Jumapili

Shule ya Jumapili husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Inafanya hivi kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 13.1).

Urais wa Shule ya Jumapili

Rais ana wajibu wa kuhudumu katika baraza la kata, kusimamia ujifunzaji na ufundishaji wa injili nyumbani na kanisani, na kuandaa madarasa. Rais pia anaunga mkono, anahimiza, na kuwaelekeza walimu kuwa na ufanisi zaidi kwa kufuata kanuni katika maandiko na Kufundisha katika Njia ya Mwokozi (ona 13.2.2.2). Washauri wake wanamsaidia.

Madarasa ya Jumapili

Madarasa ya Shule ya Jumapili yanafanyika Jumapili ya kwanza na ya tatu ya mwezi. Ukubwa wa darasa utatofautiana kulingana na mahitaji ya kila kata (ona 13.3). Walimu wa Shule ya Jumapili hutumia maandiko, masomo yaliyopangwa ndani ya Njoo, Unifuate, na maneno ya manabii wa siku hizi kama nyenzo zao kuu za kufundishia.

Mafunzo Yanayolenga Nyumbani

Wazazi wanawajibika kuwafundisha injili watoto wao. (ona 13.5). Walimu wa Shule ya Jumapili na viongozi wanawahimiza waumini kutafuta mwongozo wa kiungu wao wenyewe kuhusu jinsi gani ya kujifunza na kufundisha injili katika nyumba zao (ona 17.2).

Mikutano ya Baraza la Walimu

Katika mikutano ya baraza la walimu, walimu wanashauriana pamoja kuhusu kanuni za kufundisha kama Kristo. Pia wanashauriana kuhusu jinsi ya kuboresha kujifunza na kufundisha injili. Kufundisha katika njia ya Mwokozi inatumika kama nyenzo (ona 17.4). Mikutano hii hufanyika kila robo ya mwaka wakati wa darasa siku ya Jumapili na kwa kawaida huongozwa na rais wa Shule ya Jumapili (ona 13.4).

Mikutano ya Baraza la Walimu kwa ajili ya Wazazi

Chini ya maelekezo ya askofu na baraza la kata, rais wa Shule ya Jumapili husaidia kuandaa mikutano ya baraza la walimu kwa ajili ya wazazi. Mikutano hii inafuata muundo na marudio sawa na mikutano ya kawaida ya baraza la walimu, lakini katika hali hii wazazi wanaalikwa kuhudhuria. Kusudi ni kuwasaidia wazazi kuwa walimu bora katika nyumba zao. Kufundisha katika Njia ya Mwokozi na nyenzo za utangulizi katika Njoo, Unifuate zinapaswa kutumika kama nyenzo (ona 17.4).

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo ya ziada ya Shule ya Jumapili inapatikana katika sehemu ya 13.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.