Music
Majukumu


Picha
mwanamke akiongoza kwaya

Wito Wangu kama Mpiga Ala Saidizi katika Kata

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Madhumuni ya Muziki katika Kanisa

Muziki mtakatifu unaongeza imani katika Yesu Kristo. Unamwalika Roho na unafundisha mafundisho. Pia unatengeneza hisia za staha, unawaunganisha waumini, na unatoa njia ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Bwana alitamka “Kwani nafsi yangu hufurahia nyimbo za moyoni” (Mafundisho na Maagano 25:12). (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 19.1.)

Mpiga Ala Saidizi

Mpiga ala saidizi katika kata huwasaidia waumini wa kata kuongeza imani katika Yesu Kristo kupitia muziki mtakatifu. Wanatoa muziki wa kabla ya kufungua na baada ya kufunga mkutano na kiambata kwa ajili ya nyimbo za dini wakati wa mkutano wa sakramenti na mikutano mingine ya kata kama itakavyoombwa. Inapohitajika, mpiga ala saidizi anaweza pia kuambatana na kwaya au kuhudumu kama mpiga kinanda wa darasa la Watoto. (Ona 19.4.3.2).

Muziki kwa ajili ya Mikutano ya Kanisa

“Muziki wenye mwongozo wa kiungu ni sehemu muhimu ya mikutano yetu ya kanisa” (Nyimbo za Dini, Utangulizi wa Urais wa Kwanza). Uchaguzi wa muziki unapaswa kufundisha injili kwa nguvu na uwazi (ona 19.3.1).

Muziki kwa ajili ya Mkutano wa Sakramenti

Muziki katika mkutano wa sakramenti unajumuisha kuimba nyimbo za dini ili kufungua na kufunga mkutano na kabla ya kutolewa kwa sakramenti. Mkutano wa sakramenti unaweza pia kujumuisha wimbo mmoja au zaidi wa dini au mawasilisho ya muziki. Nyimbo za dini au teuzi zingine za muziki mtakatifu zinaweza kutumika kwa ajili ya muziki wa utangulizi na hitimisho, muziki wa kwaya, na mawasilisho ya mtu mmoja mmoja au vikundi vidogo vidogo. (Ona 19.3:2.)

Mafunzo na Nyenzo

Kwa maelezo kuhusu mafunzo ya muziki, ona sehemu ya 19.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla. Ikiwa hakuna mpiga ala saidizi kwa ajili ya mikutano ya kata, ona sehemu ya 19.4.3.2 ili kupata muziki wa ala saidizi uliorekodiwa.

Miongozo na Sera

Kwa sera na miongozo ya ziada, kama vile upatikanaji wa muziki, matumizi ya vifaa vya nyumba ya mikutano kwa ajili ya mazoezi, au kwaya ya jamii, ona sehemu ya 19.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha