Wito Wangu kama Mpiga Muziki wa Kwaya katika Kata
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Madhumuni ya Muziki katika Kanisa
Muziki mtakatifu unaongeza imani katika Yesu Kristo. Unamwalika Roho na unafundisha mafundisho. Pia unatengeneza hisia za staha, unawaunganisha waumini, na unatoa njia ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Bwana alitangaza “Kwani nafsi yangu hufurahia nyimbo za moyoni” (Mafundisho na Maagano 25:12). (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 19.1.)
Mpiga muziki wa Kwaya katika Kata
Mpiga muziki wa kwaya katika kata huwasaidia waumini wa kata waongeze imani na kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kupitia muziki mtakatifu. Wanapiga kwa ajili ya mazoezi ya kwaya na wakati kwaya inapoimba katika mikutano ya Kanisa (ona 19.4.3.3).
Kwaya za Kata
Kwaya za Kanisa huleta utukufu kwa Mungu, huwaunganisha na kuwajenga waumini wa Kanisa, na huleta furaha kwa washiriki na mikusanyiko. Kwaya zinahimizwa kutumia nyimbo za dini za Kanisa, ambazo zinamwalika Roho na kuwasaidia washiriki wa kwaya na mikusanyiko kujifunza injili (ona Nyimbo za Dini, 381–83). Kwaya za Kanisa zinaweza pia kuimba chaguzi zingine za muziki mtakatifu. Chaguzi zote za muziki zinapaswa kufundisha injili kwa nguvu na uwazi. (Ona 19.3.)
Miongozo na Sera
Mazoezi ya kwaya kwa kawaida hayazidi saa moja. Kwa sera na miongozo ya ziada, kama vile kupata muziki, matumizi ya vifaa vya nyumba ya mkutano kwa ajili ya mazoezi, au kwaya za jamii, ona sehemu ya 19.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.