Music
Majukumu


Picha
mwanamke akiongoza kwaya

Wito Wangu kama Mratibu wa Muziki kwenye Kata

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Madhumuni ya Muziki katika Kanisa

Muziki mtakatifu unaongeza imani katika Yesu Kristo. Unamwalika Roho na unafundisha mafundisho. Pia unatengeneza hisia za unyenyekevu, unawaunganisha waumini, na unatoa njia ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Bwana amesema, “Nafsi yangu hufurahia nyimbo za moyoni” (Mafundisho na Maagano 25:12). (Ona Kitabu cha Maelekezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 19.1.)

Mratibu wa Muziki kwenye Kata

Waratibu wa muziki kwenye kata huwasaidia waumini wa kata kuongeza imani katika na ibada kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kupitia muziki mtakatifu. Wanahudumu chini ya maelekezo ya askofu. Waratibu wa muziki kwenye kata ni nyenzo kwa ajili ya askofu na viongozi wengine wa kata juu ya mambo ya muziki. Waratibu wa muziki wanaweza kuhudhuria mikutano ya baraza la kata kama itakavyopendekezwa na askofu. (Ona 19.4.2.)

Muziki kwa ajili ya Mikutano ya Kanisa

“Muziki wenye mwongozo wa kiungu ni sehemu muhimu ya mikutano yetu ya kanisa” (Nyimbo za Dini, Dibaji ya Urais wa Kwanza). Chaguzi za muziki zinapaswa kufundisha injili kwa nguvu na uwazi (ona 19.3.1).

Muziki kwa ajili ya Mkutano wa Sakramenti

Muziki katika mkutano wa sakramenti unajumuisha kuimba nyimbo za dini ili kufungua na kufunga mkutano na kabla ya kuhudumia sakramenti. Mkutano wa sakramenti pia unaweza kujumuisha wimbo wa ziada mmoja au zaidi toka nyimbo za dini au mawasilisho ya muziki. Nyimbo za dini au teuzi zingine za muziki mtakatifu zinaweza kutumika kwa ajili ya muziki wa utangulizi na wa baada ya tukio, muziki wa kwaya na mawasilisho ya kikundi kidogo au mtu binafsi. (Ona 19.3.2.)

Mafunzo na Nyenzo

Waratibu wa muziki kwenye kata hupendekeza na kutoa mafunzo kwa waumini kwa ajili ya kuhudumia katika miito ya muziki kwenye kata. Wanatoa msaada na maelekezo na kusimamia mafunzo ya muziki kadiri inavyohitajika. (Ona 19.6.) Kama hakuna mpiga kinanda kwa ajili ya mikutano ya kata, tazama sehemu ya 19.4.3.2 ya Kitabu cha Maelekezo ya Jumla ili kupata sauti za kinanda zilizorekodiwa.

Miongozo na Sera

Kwa sera na miongozo ya ziada, kama vile kupata muziki, matumizi ya vifaa vya nyumba ya mkutano kwa ajili ya mazoezi, au kwaya ya jamii, ona sehemu ya 19.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha