Wito Wangu kama Kiongozi wa Muziki katika Kata
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Madhumuni ya Muziki katika Kanisa
Muziki mtakatifu unaongeza imani katika Yesu Kristo. Unamwalika Roho na unafundisha mafundisho. Pia unatengeneza hisia za staha, unawaunganisha waumini, na unatoa njia ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Bwana alitangaza, “Kwani nafsi yangu hufurahia nyimbo za moyoni” (Mafundisho na Maagano 25:12). (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 19.1.)
Kiongozi wa Muziki katika Kata
Kiongozi wa muziki katika kata huwasaidia waumini wa kata waongeze imani na kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kupitia muziki mtakatifu. Wanaendesha nyimbo za mkusanyiko kwa ajili ya mkutano wa sakramenti na kwa ajili ya mikutano mingine ya kata kama ilivyoombwa (ona 19.4.3.1).
Muziki kwa ajili ya Mikutano ya Kanisa
“Muziki wenye mwongozo wa kiungu ni sehemu muhimu ya mikutano yetu ya kanisa” (Nyimbo za Dini, Utangulizi wa Urais wa Kwanza). Uchaguzi wa muziki unapaswa kufundisha injili kwa nguvu na uwazi (ona 19.3.1).
Muziki kwa ajili ya Mkutano wa Sakramenti
Muziki katika mkutano wa sakramenti unajumuisha kuimba nyimbo za dini ili kufungua na kufunga mkutano na kabla ya kutolewa kwa sakramenti. Mkutano wa sakramenti unaweza pia kujumuisha wimbo mmoja au zaidi wa dini au mawasilisho ya muziki. Nyimbo za dini au teuzi zingine za muziki mtakatifu zinaweza kutumika kwa ajili ya muziki wa utangulizi na hitimisho, muziki wa kwaya, na mawasilisho ya mtu mmoja mmoja au vikundi vidogo vidogo. (Ona 19.3:2.)
Mafunzo na Nyenzo
Kwa maelezo kuhusu mafunzo ya muziki, ona sehemu ya 19.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla. Ikiwa hakuna mpiga muziki anayepatikana kwa ajili ya mikutano ya kata, ona sehemu ya 19.4.3.2 ili kupata maandalizi ya muziki yaliyorekodiwa.
Miongozo na Sera
Kwa sera na miongozo ya ziada, kama vile kupata muziki, matumizi ya vifaa vya nyumba ya mikutano kwa ajili ya mazoezi, au kwaya za jamii, ona sehemu ya 19.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.