Wito wangu kama Rais wa Wasichana
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Wasichana
Kikundi cha Wasichana kinawasaidia mabinti wapendwa wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Kinawasaidia wasichana wafanye na washike maagano matakatifu na kuzidisha uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Katika madarasa yao, wasichana wanawahudumia wengine, wanatimiza majukumu yao ya kimaagano, wanajenga umoja, na wanajifunza na kuishi mafundisho. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 11.1.1.)
Rais na Urais
Rais anahudumu kwenye baraza la kata na baraza la vijana la kata (ona 10.3.4.4). Anaitisha mikutano ya urais mara kwa mara na anakutana na askofu. Urais unawahudumia wasichana kadiri wanavyozidi kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo wa maisha yote. Wanawafundisha urais wa madarasa majukumu yao na kuwasaidia wakati wanapoongoza. (Ona 11.3:2.) Rais anasimamia kumbukumbu, ripoti na fedha. Washauri wake hutoa msaada. Rais pia anashauriana na wasichana kuhusu changamoto ambazo hazimhitaji askofu au hazihusiani na udhalilishaji.
Uongozi wa Vijana
Urais wa Wasichana unawasaidia viongozi vijana. Marais wa madarasa wanahudumu kwenye baraza la Vijana la kata. Urais wa madarasa huongoza na kuwahudumia wasichana kadiri wanavyomkaribia zaidi Mwokozi na kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Kwa kusaidiwa na viongozi watu wazima, wanapanga miradi ya huduma, shughuli na mikutano ya Jumapili. (Ona 11.3.4.2.)
Madarasa ya Jumapili
Uaskofu na viongozi watu wazima wa Wasichana kwa sala wanaamua jinsi ya kupanga madarasa kulingana na umri. Wanazingatia fursa za uongozi kwa wasichana. Kila darasa, bila kujali ukubwa, linapaswa kuwa na rais na, pale inapowezekana, mshauri mmoja au wawili na katibu (ona 11.1.3).
Huduma na Shughuli
Urais wa darasa, ukisaidiwa na viongozi watu wazima, wanapanga huduma na shughuli ambazo zinajenga shuhuda, kuimarisha familia, kuleta umoja wa darasa na kutoa fursa za kuwabariki wengine (ona 11.2.1.3). Huduma na shughuli ni fursa ya kuwakusanya vijana na kushiriki shangwe ya kuishi injili na kushiriki katika kazi kuu ya Bwana.
Miongozo na Sera
Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu wasichana wenye ulemavu, nembo ya vijana na mengine zaidi yanapatikana katika sehemu ya 11.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.