Wito Wangu kama Rais wa Akidi ya Wazee
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Akidi ya Wazee
Ukuhani wa Melkidezeki unawasaidia watoto wa Mungu kujiandaa kurudi katika uwepo Wake. Washiriki wa akidi ya wazee hufanya kazi pamoja ili kusaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Wanawatumikia wengine, wanatimiza wajibu wa ukuhani, wanajenga umoja, na wanajifunza na kuishi mafundisho (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 8.1).
Rais wa Akidi ya Wazee
Rais wa akidi ya wazee huwafundisha washiriki wa akidi kazi zao za ukuhani. Majukumu yake pia yanajumuisha kuhudumu katika baraza la kata; kuunganisha juhudi pamoja na urais wa Muungano wa Usaidizi; na kusimamia uhudumiaji, shughuli, ripoti, kumbukumbu na fedha. Washauri na katibu wake wanamsaidia (ona 8.3.3.2).
Urais
Urais wa akidi ya wazee na katibu hukutana mara kwa mara. Kusaidia wazee watarajiwa kujiandaa kupokea Ukuhani wa Melkizedeki ni mojawapo ya vipaumbele vya juu zaidi vya urais huu (ona 8.4).
Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi
Urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi huratibu majukumu ya uhudumiaji na kusaidia kuongoza kazi ya hekaluni na historia ya familia na juhudi za kuwaalika wote kupokea baraka za injili. Pia wana jukumu muhimu katika kufundisha waumini wa kata kanuni za uhudumiaji, mahojiano ya uhudumiaji, kuishi sheria ya mfungo, kujenga kujitegemea na kuongeza utayari wa kibinafsi na wa familia (ona 22.6.2).
Mikutano ya Jumapili
Akidi ya wazee hukutana Jumapili ya pili na ya nne ya mwezi ili kukuza imani, kujenga umoja na kuimarisha familia na nyumba. Urais wa akidi ya wazee kwa sala huchagua jumbe kutoka kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni zaidi ili kujadili kulingana na mahitaji ya washiriki (ona 8.2.1.2).
Huduma na Shughuli
Urais wa akidi ya wazee wanaweza kupanga shughuli za kuwaimarisha washiriki wa akidi na kuwapa fursa za kutumikia pamoja (ona 8.2.1.3).
Miito ya ziada
Askofu na rais wa akidi ya wazee wanajadili hitaji la miito ya ziada inapohitajika (ona 8.3.5).