“Mawazo kwa ajili ya Ukuaji katika Nyanja Zote za Maisha,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana (2019)
“Mawazo kwa ajili ya Ukuaji katika Nyanja Zote za Maisha,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Vijana
Mawazo kwa ajili ya Ukuaji katika Nyanja Zote za Maisha
Kuna njia nyingi unazoweza kukua maishani mwako! Pata mawazo kutoka katika kurasa zifuatazo, au buni yako mwenyewe. Muombe Baba yako wa Mbinguni akusaidie kujua kile unachohitaji kufanyia kazi hivi sasa.
Unaweza kupata mawazo ya ziada kwenye ChildrenandYouth.ChurchofJesusChrist.org na kwenye Gospel Living app.
Kiroho
-
Sali kwa dhati.
-
Jifunze maandiko na maneno ya manabii walio hai.
-
Tafuta nafasi za kushiriki injili.
-
Gundua na kuza karama za Kiroho.
-
Jiandae kwa ajili ya baraka zako za baba mkuu.
-
Kwa ustahiki kuwa na kibali cha Hekaluni.
-
Shughulikia historia ya familia yako na hudumu hekaluni.
-
Onyesha shukrani kila siku.
-
Tii amri kikamilifu.
-
Jifunze maisha ya Kristo.
-
Shiriki sakramenti kila wiki kwa ustahiki.
-
Shiriki seminari.
Kijamii
-
Zingatia zaidi mahitaji ya wengine.
-
Jifunze kusikiliza vizuri na kuelezea mawazo kwa uwazi.
-
Wapende na uwatumikie watu walio karibu nawe.
-
Tumia muda pamoja na familia.
-
Jiandae kuwa mwenza au mzazi.
-
Kuza uwezo wako wa kukubaliana na hali—uwezo wa kukubaliana na mazingira na kuvumilia wakati mambo yanapokuwa magumu.
-
Jihusishe katika shughuli za shuleni au za jamii.
-
Tafuta njia za kuwajali masikini.
-
Jifunze kuomba radhi. Jifunze kusamehe.
-
Zungumza na tenda kwa ukarimu, na epuka kusengenya.
Kimwili
-
Boresha afya yako ya kimwili na nguvu.
-
Jifunze au boresha ujuzi wa kimwili, kama vile michezo, dansi, au shughuli za nje.
-
Jifunze au boresha ujuzi wa kisanaa au kiufundi.
-
Tawala tamaa za kimwili katika njia bora.
-
Jifunze njia za kujilinda dhidi ya unyanyasaji, na tafuta usaidizi ikihitajika.
-
Epuka ponografia.
-
Tafuta njia bora za kutawala hisia na msongo wa mawazo.
-
Jifunze kuwajali watoto.
-
Jifunze kuwa msafi.
-
Jifunze kutumia vifaa vya kawaida vya shambani na nyumbani.
-
Jifunze huduma ya kwanza na ujuzi wa kubaki salama.
-
Tumia lugha inayofaa, na nadhifu.
Kiakili
-
Boresha ustadi wako wa kusoma na kuandika.
-
Kuza tabia nzuri ya kujifunza.
-
Fahamu unachohitaji kufanya kupata kazi nzuri, na uanze kushughhulikia lengo hilo.
-
Jifunze zaidi kuhusu kitu ambacho kinakupendeza.
-
Zungumza na watu unaowachukulia kama mfano ili uweze kujua jinsi walivyokuza sifa unazotaka kuwa nazo.
-
Jifunze kutumia fedha kwa busara.
-
Jifunze mada ya injili kwa kina.
-
Jifunze ujuzi wa msingi wa kazi ambao unaweza kuutumia sasa na baadaye.
-
Hudhuria matukio ya kitamaduni.
-
Jifunze lugha nyingine.
-
Kuwa mwenye kujitegemea zaidi.
-
Jifunze na tumia kanuni za kujiongoza.