Sehemu ya 129
Mafundisho yaliyotolewa na Joseph Smith Nabii, huko Nauvoo, Illinois, 9Â Februari 1843, ambayo yanaelezea funguo kuu tatu ambazo kwa hizo twaweza kutofautisha aina sahihi za malaika na roho wahudumu.
1–3, Mbinguni kuna miili ya waliofufuka na miili ya kiroho; 4–9, Funguo zimetolewa ambazo kwa hizo wajumbe kutoka ngʼambo ya pazia wanaweza kutambulika.
1 Kuna viumbe wa aina mbili mbinguni, nao ni: Malaika, ambao ni watu waliofufuka, wenye miili ya nyama na mifupa—
2 Kwa mfano, Yesu alisema: Nishikenishikeni na mwone, kwa kuwa roho haina mwili na mifupa, kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.
3 Ya pili, ni roho za watu wenye haki waliokamilika, wale ambao hawajafufuka, lakini wanarithi utukufu huo huo
4 Wakati mjumbe akija akisema anao ujumbe kutoka kwa Mungu, mpe mkono wako na mwombe mshikane mikono.
5 Kama yeye atakuwa malaika atafanya hivyo, nawe utausikia mkono wake.
6 Kama atakuwa roho ya mtu mwenye haki aliyekamilika yeye atakuja katika utukufu wake; kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee anayoweza kuonekana—
7 Mwombe mshikane mikono, lakini yeye hatafanya lolote, kwa sababu ni kinyume cha utaratibu wa mbinguni kwa mtu mwenye haki kudanganya; lakini yeye bado atatoa ujumbe wake—
8 Lakini ikiwa ni ya ibilisi akiwa kama malaika wa nuru, ukimwomba kushikana mikono naye atakupa mkono wake, na wewe hutasikia chochote; nawe utaweza kumgundua.
9 Hizi ndizo funguo kuu tatu ambazo kwa njia hiyo ninyi mtaweza kujua iwapo huduma yoyote yatoka kwa Mungu.