Sehemu ya 22
Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Manchester, New York, 16Â Aprili 1830. Ufunuo huu ulitolewa kwa Kanisa katika matokeo ya baadhi ya watu waliobatizwa hapo awali wakitamani kuungana na Kanisa bila ya kubatizwa tena.
1, Ubatizo ni agano jipya na lisilo na mwisho; 2–4, Ubatizo wenye mamlaka unahitajika.
1 Tazama, ninawaambia kwamba maagano yote ya zamani nimeyaondoa katika jambo hili; na hili ni agano jipya na lisilo na mwisho, hata lile lililokuweko tangu mwanzo.
2 Kwa hivyo, hata kama mwanadamu angebatizwa mara mia haitamfaa lolote, kwani hamuwezi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba kwa torati ya Musa, wala kwa kazi zenu zisizo na uhai.
3 Kwani ni kwa sababu ya kazi zenu zisizo na uhai kwamba nimefanya agano hili la mwisho na kanisa hili lijengwe kwa ajili yangu, kama ilivyokuwa katika siku za kale.
4 Kwa hivyo, ingieni ninyi katika mlango, kama nilivyoamuru, na wala msitake kumshauri Mungu wenu. Amina.