Sehemu ya 79
Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, 12Â Machi 1832.
1–4, Jared Carter anaitwa kuhubiri injili kwa msaada wa Mfariji.
1 Amini ninawaambia, kuwa haya ndiyo mapenzi yangu kwamba mtumishi wangu Jared Carter aende tena katika nchi za mashariki, kutoka mahali hadi mahali, na kutoka mji hadi mji, katika uwezo uliotokana na kutawazwa kwake, akitangaza habari njema za shangwe kuu, hata injili isiyo na mwisho.
2 Nami nitamletea Mfariji, atakaye mfundisha ukweli na kumwonyesha njia ya kwenda;
3 Na kadiri atakavyokuwa mwaminifu, nitamtuza tena miganda.
4 Kwa hiyo, moyo wako na ufurahi, mtumishi wangu Jared Carter, na usiogope, asema Bwana wako, hata Yesu Kristo. Amina.