Maandiko Matakatifu
Nakala Halisi 1


Nakala Halisi ya Mchoro kutoka Kitabu cha Ibrahimu

Na. 1

Nakala Halisi 1

Maelezo

Picha 1. Malaika wa Bwana.

Picha 2. Ibrahimu amefungwa juu ya madhabahu.

Picha 3. Kuhani wa uongo wa Elkena akijaribu kumtoa Ibrahimu kama kafara.

Picha 4. Madhabahu ya makuhani wa uongo kwa ajili ya kutolea kafara, ikiwa imesimama mbele ya miungu ya Elkena, Libna, Mamakra, Korashi, na Farao.

Picha 5. Sanamu ya mungu wa Elkena.

Picha 6. Sanamu ya mungu wa Libna.

Picha 7. Sanamu ya mungu wa Mamakra.

Picha 8. Sanamu ya mungu wa Korashi.

Picha 9. Sanamu ya mungu wa Farao.

Picha 10. Ibrahimu akiwa Misri.

Picha 11. Imechorwa ili kusimama badala ya nguzo za mbinguni, kama ilivyoeleweka kwa Wamisri.

Picha 12. Raukeeyangi, maana yake eneo pana la wazi, au anga juu ya vichwa vyetu; lakini katika jambo hili, kuhusiana na somo hili, Wamisri walitaka imaanishe Shaumau, kuwa juu, au mbingu, sawa sawa na neno la Kiebrania, Shaumahyeemu.