Nakala Halisi ya Mchoro kutoka Kitabu cha Ibrahimu Na. 3 Maelezo Picha 1. Ibrahimu akiwa amekaa juu ya kiti cha enzi cha Farao, kwa heshima ya mfalme, pamoja na taji juu ya kichwa chake, ikiwakilisha Ukuhani, kama alama ya Urais Mkuu wa Mbinguni; pamoja na fimbo ya haki na hukumu mkononi mwake. Picha 2. Mfalme Farao, ambaye jina lake limetolewa katika maandishi yaliyo juu ya kichwa chake. Picha 3. Inamwonyesha Ibrahimu akiwa Misri kama ilivyotolewa pia katika picha ya 10 ya Nakala Halisi ya Mchoro Na. 1. Picha 4. Mwana wa mfalme Farao, Mfalme wa Misri, kama ilivyoandikwa juu ya mkono. Picha 5. Shulemu, mmoja wa wahudumu wakuu wa mfalme, kama ilivyoonyeshwa kwa maandishi juu ya mkono wake. Picha 6. Olimla, mtumwa aliye mali ya mwana wa mfalme. Ibrahimu akitafakari juu ya kanuni za Elimu ya Sayari, katika baraza la mfalme.