Kutafuta Amani kwa Ajili Yako na Wengine katika Nyakati za Matatizo
Hapa kuna njia nane za kujisaidia wewe mwenyewe na wengine kuhisi amani wakati maisha yanapokuwa magumu.
Wakati mwingine maisha hugeuka juu chini na nje ndani. Unaweza kuwa unahofia kuhusu mambo ya familia, afya, matatizo shuleni, au idadi nyingine ya matukio yanayosumbua katika ulimwengu wa leo. Tunawezaje kupata amani binafsi katika ulimwengu wenye matatizo? Haijalishi ukosefu wako wa amani huja kutokana na matukio yaliyo nje ya uwezo wako au kutokana na mambo unayoweza kushawishi na kubadilisha, hapa kuna baadhi ya mawazo kukusaidia kupata amani ya ndani kupitia Yesu Kristo.
Njia 4 za Kupata Amani kwa Ajili Yako
-
Fokasi kwenye yale ya milele
Ni vigumu kuhisi amani wakati umefokasi tu katika wasiwasi wa muda mfupi. Lakini kama ukifokasi kwenye picha kubwa, mpango wa Mungu wa furaha, unaweza kupata amani katika kujua kwamba kile kinachoumiza kwa sasa hakitadumu milele. Kwa mfano, hekalu hutusaidia kufokasi kwenye umilele. Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alisema kwamba hekaluni “mtajua amani ambayo haiwezi kupatikana sehemu nyingine yeyote.”1
-
Achana na kile kilicho nje ya uwezo wako
Pale kitu kilicho nje ya uwezo wako kinapochukua amani yako, kinaweza kushawishi kwenye kuhisi kukosa tumaini ua hasira. Lakini haisaidii kudumu katika vitu usivyoweza kubadilisha. Badala yake, sogea karibu na Mwokozi ili kupata amani ya ndani hata kama maisha hayakuendei vizuri. Yeye ameahidi kukutumia Mfariji, Roho Mtakatifu (ona Yohana 14:26–27).
-
Samehe Wengine
Mara nyingi jambo gumu la kuacha lipite ni ubaya unaohisi wakati mtu anapokukosea. Lakini Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha: “Tutapokea shangwe ya msamaha katika maisha yetu wenyewe wakati tunapokuwa tayari kutoa shangwe hiyo bila kikwazo kwa wengine. … Kama matokeo, Roho wa Bwana atajaza nafsi zetu kwa shangwe inayoambatana na amani takatifu ya ufahamu (ona Mosia 4:2–3).”2 Kumgeukia Mwokozi kunaweza kukusaidia kuwa huru kutokana na mizigo ya kihisia na kujazwa na amani.
-
Tubu na mtegemeee Kristo
Bila kujali nini kingine kinakwenda vizuri katika maisha yako, kubeba mzigo wa dhambi daima kutakunyang’anya amani. Wakati mwingine tunamhitaji askofu wetu atusaidie kutubu kikamilifu. Lakini sote tunahitaji kutubu mara kwa mara na, kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, kuwa huru kutokana na kila kitu kinachotuzuia kuwa zaidi kama Yeye.
Njia 4 za Kuwasaidia Wengine Kupata Amani
-
Shiriki Injili ya Yesu Kristo.
Kama vile tunavyoweza kupata amani kwa ajili yetu kwa kufokasi juu ya Mwokozi, tunaweza kuwaongoza wengine Kwake kama “mwanzilishi wa amani” (Mosia 15:18) Kwa mfano, kujaribu kushiriki andiko au nukuu kutoka kwenye mkutano mkuu ambayo imekusaidia wewe kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo.
-
Kuwa mpatanishi
Wasaidie rafiki zako au ndugu zako kutatua matatizo. Kama vile watu wa Anti-Nephi-Lehi katika kitabu cha Alma, tunaweza kuzika silaha zetu za vita—silaha kama umbea, kutafuta kisasi, au kuwa wabinafsi—na kuzibadilisha kwa vyombo vya amani: kuzungumza kwa ukarimu, kutii amri za Mungu, na kusamehe wengine (ona Alma 24:19).
-
Kuwa msikilizaji mzuri
Wakati mwingine watu wanaohangaika wanahitaji kuzungumza kwa uwazi kuhusu mawazo na hisia zao badala ya kunyamaza. Hatupaswi kutatua matatizo yao kwa ajili yao, bali tunaweza tu kusikiliza matatizo yao na kutoa msaada, kuonyesha upendo na uelewa kama wa Kristo.
-
Wahudumie wale walioko kwenye kata na jumuia yako.
Ungeweza kujitolea kwenye kituo cha wasio na makazi, kuhudumu kama mwalimu mwenzi, au kuleta zawadi kwa familia mpya katika ujirani wako. Wasaidie watu kupata amani katika vitu vidogo. Kuwa na sehemu ya kudumu ya kula na kulala, mshauri wa kutegemewa, au uhakika mdogo kwamba mtu fulani anajali kunaweza kuwa na matokeo ya muda mrefu.
Yesu alizungumza maneno haya ya faraja kwa wale wote wanaohangaika kutafuta amani: “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa: niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msiwe na wasiwasi moyoni mwenu, wala msifadhaike.” (Yohana 14:27). Ikiwa tutajileta sisi na kuwaleta wengine karibu na Yesu Kristo, tunaweza kupata amani hata wakati maisha yanapokuwa magumu.