Je, Nimeshaona Mkono wa Mungu katika Maisha Yangu?
Ibada ya CES kwa Vijana • Machi 3, 2013 • Chuo Kikuu cha Texas Arlington
Ninaposafiri ulimwenguni na mume wangu, ninasikitishwa kugundua kwamba vijana wengi huhisi upweke na wana shaka kwamba Bwana anawajua kibinafsi au kwamba Yeye anawapenda. Nimeomba kuhusu kanuni ambazo ningesisitiza usiku wa leo ambazo zingewasaidia kujua kwamba Bwana anawajua ninyi na anawapenda ninyi. Naomba Roho anisaidie kutoa ujumbe huu.
Nitatumia maneno kutoka kwa wimbo wa seminari ili kuandaa hotuba yangu:
Lazima tuwe na masikio ya kusikia neno la Bwana,
Na macho ya kuuona mpango wake,
Miguu ya kufuata katika njia Yake,
Na mioyo ya kuelewa.
(Steven K. Jones, “Hearts that Understand,” Hold to the Rod Songbook [1988], 20)
Masikio ya kusikia Neno la Bwana
Kwanza, lazima tuwe na masikio ya kusikia neno la Bwana. Tunaweza kusikia sauti ya Bwana tunapojifunza maandiko (ona M&M 18:34–36). Nilipokuwa na umri wenu, Spencer W. Kimball alikuwa Rais wa Kanisa. Dondoo kutoka kwake imeniongoza katika maisha yangu. Alisema: “Nimegundua kwamba ninapozembea katika uhusiano wangu na uungu na inapoonekana kwamba hakuna sikio la kiungu linalosikiliza, na hakuna sauti ya kiungu inayozungumza, kwamba niko mbali, mbali sana. Ikiwa nitajitumbukiza katika maandiko umbali unapungua na utakatifu unarejea” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 67).
Nashuhudia kuwa ikiwa tuna masikio ya kusikia neno la Bwana, tutahisi upendo Wake, Yeye anaponena nasi kupitia kwa maandiko.
Macho ya Kuuona Mpango Wake
Pili, lazima tuwe na macho ya kuuona mpango Wake. Siku moja nilikuwa nikifikiria kuhusu mmisionari aliyerudi, niliyemjua, wakati bila kutarajia, nilipopokea barua pepe kutoka kwake. Aliniambia jinsi alivyohisi wakati Bwana alipofanya miujiza kupitia kwake katika uwanja wa misheni, lakini tangu kurejea kwake nyumbani alishangaa wakati mwingine ikiwa Bwana alimfahamu kwa kweli.
Katika jibu langu kwake, nilishiriki ushauri mwingine muhimu ambao Mzee Henry B. Eyring alitoa kwa wanafunzi wa BYU-Idaho. Alisema: “Nawabariki kwamba kila siku, kama mtauliza kwa sala ili kuonyeshwa mahali ambapo mkono wa Mungu umeingilia katika maisha yako siku hiyo, nawabariki ili muweze kuona hayo. Itadhihirishwa kwenu. Kwamba mtaona kuwa anawaelekeza na kuwaongoza na kuwainua, na kwamba Yeye anawajua” (“A Steady, Upward Course” [Brigham Young University–Idaho devotional, Sept. 18, 2001], web.byui.edu/devotionalsandspeeches).
Kisha nikaelezea jinsi niliomba kila siku kwa baraka hii na nikaona mkono wa Mungu ukifikia ili kunigusa kupitia kumbukumbu yake yenye mawazo. Nilimhakikishia Baba yake wa Mbinguni atafanya vivyo hivyo kwa ajili yake.
Nashuhudia kwamba tunapoomba kwa ajili ya macho ya kuuona mpango Wake, tutafahamu ushiriki wa Mungu katika maisha yetu na kujua kwamba Yeye anatujua.
Miguu ya Kufuata katika Njia Yake
Tatu, lazima tuwe na miguu ya kufuata katika njia Yake. Vijana wazima wengi wanahuzunika, wanakukosa imani, na kuvunjika moyo kwa sababu matukio waliyodhani yangetokea katika maisha yao na bado hayajatokea. Baadhi yao wanaamini kimakosa kuwa ikiwa Mungu hajawapa furaha au baraka walizokuwa wakizitarajia au kudhani walistahili, Yeye hajali. Kuonyesha kero yao na Mungu, baadhi yao hupoteza imani, hukiuka maagano, huweka imani yao katika anasa za kilimwengu, na hugeuka kutoka kwa Mungu kwa kujitegemea. Badala ya kuwa na miguu ya kufuata njia ya haki, wanaondoka kutoka kwa njia ya injili, kutanga mbali, na kupotea. Sote tunajua mtu ambaye ametoka “nje ya njia.” Tunaweza kuhisi upendo wa Mungu katika maisha yetu tunapoona majibu ya kuvutia ya wengi tunapofikia kutumika na kuokoa.
Njia ya Bwana imewekwa alama wazi wazi kwa mafundisho ya manabii, waonaji, na wafunuzi. Mwezi ujao ni mkutano mkuu. Nashuhudia, ikiwa tutatafuta kwa maombi ili kutambua swali la kibinafsi au tatizo la kupeleka kwa mkutano huo, Bwana atatujibu kupitia kwa ujumbe wa watumishi wake watakatifu. Tutaweza kuhisi upendo Wake na kujali Kwake na kuwa na ujasiri mwingi na miguu imara ya kufuata katika njia Yake sasa na hata milele.
Mioyo ya Kuelewa
Nne, tunahitaji mioyo ili kuelewa kipawa cha Upatanisho wa Yesu Kristo. Mzee Bednar amefundisha: “Ni jambo moja kujua kwamba Yesu Kristo alikuja duniani kufa kwa ajili yetu---hilo ni la msingi na kimsingi katika mafundisho ya Kristo. Lakini pia tunahitaji kufahamu kwamba Bwana anatamani, kupitia Upatanisho Wake na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, kuishi ndani yetu---sio tu kutuongoza, bali pia kutuwezesha” (“The Atonement and the Journey of Mortality,” Ensign, Apr. 2012, 42).
Kwangu, Upatanisho wa Yesu Kristo hutoa faraja kwa mtu binafsi na ushahidi wenye nguvu wa upendo wa Mungu kwetu. Hutuimarisha kufanya mambo magumu---mambo ambayo hatufikiria tunaweza kufanya. Hutusaidia kushikilia wakati hatuelewi mapenzi ya Mungu na wakati wake katika maisha yetu. Nashuhudia kwamba Mungu anaishi, na tutahisi upendo Wake na kujua kwamba Yeye anatujua tunapojitolea mioyo yetu kuelewa kikamilifu zaidi baraka ya Upatanisho wa Mwanawe, Yesu Kristo.
Lazima tuwe na masikio ya kusikia neno la Bwana,
Na macho ya kuuona mpango Wake
Miguu ya kufuata katika njia Yake,
Na mioyo ya Kuelewa
(Jones, “Hearts that Understand,” 20)
Katika jina la Yesu Kristo, Amina.
© 2013 by Intellectual Reserve, Inc. All rights reserved. Kiingereza kiliidhinishwa: 8/12. Tafsiri iliidhinishwa: 8/12. Tafsiri ya Have I Seen the Hand of God in My Life? Language. Swahili. PD50045417–743