Ukweli ni Nini?
Ndugu na kina dada zangu wapendwa, rafiki zangu vijana wapendwa, nina shukurani kwa fursa hii ya kuwa nanyi siku ya leo. Daima huinua roho yangu kuzungukwa na vijana watu wazima wa Kanisa na mmenitia moyo kutangaza.. “Acha Sayuni kwa uzuri wake iamke.” Na ninyi mnaoishi kote ulimwenguni, mnawakilisha kwa njia nzuri kudra na nguvu za Kanisa. Kwa sababu ya hamu zenu njema na sharti lenu la kumfuata Mwokozi, kudra ya Kanisa hili inaonekana kuwa angavu.
Nawaleteeni ninyi upendo na baraka za Rais Thomas S. Monson. Urais wa Kwanza huwaombea ninyi kila mara. Daima tunamwomba Bwana kuwabariki, kuwalinda, na kuwaongoza.
Wanaume Vipofu na Tembo
Naam zaidi ya miaka mia moja iliyopita, mshairi Mwamerika aliweka kina cha shairi katika methali ya kale. Ubeti wa kwanza wa shairi unaongea kuhusu:
Wanaume sita wa Kihindustani,
Waliozingatia sana kujifunza,
Ambao walienda kuona Tembo
(Ingawa wote walikuwa vipofu),
Ili kila mmoja kwa kuona,
Waweze kuridhisha akili zake.
Katika shairi kila mmoja wa hawa wasafiri sita anashika sehemu tofauti za tembo na kisha kuelezea kwa wengine kile amegundua.
Mmoja wa wanaume hawa anapata miguu ya tembo na kuelezea kwamba ilikuwa duara nay a kuparuza kama mti. Mwengine akashika pembe na kuelezea tembo kama mkuki. Wa tatu akashika mkia na kusisitiza kwamba tembo yuko kama kamba. Wa nne akagundua mkonga na kusisitiza kwamba tembo ni kama nyoka mkubwa.
Kila mmoja alielezea ukweli.
Na kwa sababu ukweli wake ulikuja kutokana na uzoefu wa kibinafsi, kila mmoja akisisitiza alijua kile alichojua.
Shairi linahitimisha:
Na kwa hivyo hawa wanaume wa Kihindutani,
Walibishana kwa sauti na kwa muda mrefu,
Kwa kila mmoja katika maoni yake mwenyewe,
Kwa ushupavu na uthabiti,
Ingawa kila mmoja alikuwa kwa sehemu fulani sahihi,
Na wote walikuwa wamekosa!1
Tunatazama hii hadithi kutoka mbali na kutabasamu. Hata hivyo, tunajua vile tembo alivyo. Tumesoma kuwahusu, na kuwatazama katika filamu, na wengi wetu hata wameona mmoja kwa macho yao wenyewe. Tunaamini tunajua kweli za kile tembo alicho. Kwamba mtu anaweza kufanya uamuzi juu ya hali moja ya ukweli na kuutumia kwa yote hili kuonekana kama upuuzi au hata isiyo ya kuaminika. Kwa upande mwingine, hatuwezi kujitambua wenyewe katika hawa watu sita vipofu? Na tumeshakuwa hata na hatia ya mfano huo huo wa mawazo?
Nadhania, sababu ya hadithi hii kubakia kuwa maarufu sana katika tamaduni nyingi sana, katika miaka mingi sana, ni kwa sababu ya matumizi yake kote. Mtume Paulo alisema kwamba katika huu ulimwengu nuru inapofifia na sisi tunaona tu sehemu kupitia “kioo, kilicho giza.”2 Na inaonekana kama sehemu ya uasili wetu kama wanadamu kufanya dhana kuhusu watu, siasa, na utiifu juu ya uzoefu wetu usio kamili na mara nyingi unaopotosha.
Ninakumbushwa juu ya hadithi kuhusu wanandoa ambao walikuwa wameoana kwa miaka 60. Walikuwa hawajabishana sana katika wakati huo, na siku zao pamoja zilipita katika furaha na kutosheleka. Walishirikiana katika kila kitu na hawakuwa na siri kati yao---isipokuwa hii. Mke alikuwa na sanduku ambalo aliweka juu ya kabati, na yeye alimwambia mumewe wakati walioana kwamba kamwe hasitazame ndani yake.
Jinsi miongo ilipita, wakati hukaja ambapo mume wake alichukua sanduku na akaomba kama anaweza sasa kujua kile kilichokuwa ndani yake. Mkewe akamruhusu, na alilifungua na kugundua vitambaa vya mapambo viwili na $25,000. Alipomuuliza mkewe maana yake, alijibu, “Wakati tulioana, mama yangu aliniambia mimi kwamba wakati wowote nikikasirika na wewe au wakati umesema au umefanya kitu ambacho mimi sitaki, ningefuma kitambaa kidogo cha mapambo na kisha kuzungumza juu ya mambo nawe.”
Mume alivutiwa na hadithi hio tamu hata kulia. Alishangaa kwamba katika miaka 60 ya ndoa yeye alikuwa amemsumbua mke wake ya kutosha kufuma vitambaa vya mapambo viwili. Akihisi vyema zaidi kujihusu, alimchukua mkewe kwa mkono wake na kusema, “Hio inaelezea hivi vitambaa viwili vya mapambo, lakini je! Hizi $25,000?”
Mkewe akatabasamu kwa furaha na kusema, “Hizo ni fedha nilizopata kutokana na mauzo ya vitambaa vya mapambo nilifuma miaka yote.”
Sio tu hii hadithi inafunza kwa njia ya kupendeza jinsi ya kukabiliana na kutoelewana katika ndoa, bali pia inaonyesha upumbavu wa kurukia maamuzi kwa kutumia habari zilizo na upungufu wa habari.
Kila mara “kweli” tunazojiambia ni vipande vya ukweli, na mara nyingi sio hasa ukweli kabisa.
Leo ningependa kuongelea juu ya ukweli. Ninapofanya hivyo, nawaalika ninyi kutafakari juu ya maswali machache muhimu.
Swali la kwanza ni “Ukweli ni nini?”
Pili, “ Je! Inawezekana kweli kujua ukweli?”
Na tatu, “Je! Tunafaa kufanya nini kwa vitu ambavyo vinavyokinzana na kweli ambazo tulijifunza mapema ?”
Ukweli ni nini?
Ukweli ni nini? Wakati wa kukunja jamvi la Maisha Yake, Mwokozi aliletwa mbele ya Pontio Pilato. Wazee wa Kiyahudi walikuwa wamemtuhumu kwa uchochezi na uhaini dhidi ya Roma na wakasisitiza kwamba Yeye ahukumiwe kifo.
Wakati Pilato alikutana ana kwa ana na Mtu wa Galilaya, aliuliza, “Wewe u mfalme basi?”
Yesu alijibu, “Kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.”3
Mimi sijui Pilato alikuwa mtu wa aina gani, wala sijui alikuwa anafikiria nini. Hata hivyo, nadhania kwamba alikuwa msomi na alikuwa ameona mengi ya ulimwengu unaofahamika.
Ninahisi ubeuzi fulani katika jibu la Pilato. Ninasikia katika maneno yake sauti ya mtu ambaye wakati fulani inawezekana kuwa ilikuwa udhanifu lakini sana---baada ya uzoefu mwingi sana wa maisha---anaonekana kuwa mgumu kidogo hata kuchoka.
Mimi siamini Pilato alikuwa anataka mazungumzo wakati alijibu kwa maneno matatu: “Ukweli ni nini?”4
Kuzidisha sana, nashangaa kama ikiwa yeye alikuwa hasa anauliza “Mtu anaweza kwa kweli kujua ukweli?”
Na hilo ndio swali la wakati wote na kwa watu wote.
Je! Mtu anaweza Kujua Ukweli?
Sasa, mtu anaweza kujua ukweli? Baadhi ya watu waelewa sana ambao waliohisi juu ya ulimwengu huu wamejaribu kujibu swali hili. Uhalisi telezi wa ukweli umekuwa mada inayopendelewa ya historia ya washairi wakuu na wasimulizi wa hadithi. Shakespeare anaonekana hasa kuvutiwa sana nayo. Wakati ujao unaposoma mojawapo wa majanga ya Shakespeare, angalia jinsi msuko ulileta suitafahamu ya ukweli muhimu.
Sasa, kamwe katika historia ya ulimwengu hatujapata kuwa na upatikanaji wa habari zaidi---baadhi yake kweli, baadhi yake uongo, na wingi wake ukweli nusu.
Kwa hiyo, kamwe katika historia ya ulimwengu haijakuwa muhimu sana kujifunza jinsi ya kutambua kikweli kati ya kweli na kosa.
Sehemu ya shida yetu katika utafutaji wa ukweli ni kuwa hekima ya mwanadamu imetuvunja moyo sana. Tuna mifano mingi sana ya mambo ambayo binadamu wakati mmoja “walijua” kuwa kweli lakini imeshabainishwa kuwa uongo.
Kwa mfano, licha wakati kuwa makubaliano sana, ulimwengu sio tambarare. Nyota hazizunguki juu ya ulimwengu. Kula nyanya hakuwezi kuleta kifo cha ghafula. Na, kwa kweli, mtu anaweza kupaa hasa---hata kuvunja kizuizi cha sauti.
Maandiko yamejaa na hadithi za wanaume na wanawake ambao walifasiri vibaya “ukweli”
Katika agano la kale Balamu hangekinza “ malipo ya haki” ”5 aliyopewa na Wamoabu. Kwa hivyo akajishawishi kuamini kweli mpya na kuwasaidia Wamoabu ili kuwafanya Waisraeli kujilaani kupitia kwa utovu wa uadilifu na ukosefu wa utiifu .6
Muasi Korihori, baada ya kuwaongoza wengi kutoka kwa ukweli, alikiri kwamba ibilisi alikuwa amemlaghai yeye hata pale yeye akaamini hasa kwamba kile alikuwa akisema ni ukweli.7
Katika Kitabu cha Mormoni, wote Wanefi pamoja na Walamani waliunda “kweli” zao wenyewe kuhusu kila kundi. “Ukweli” wa Wanefi kuhusu Walamani ulikuwa kwamba walikuwa “watu wanyama, wakatili, na wenye kupenda kumwaga damu,” 8 kamwe wasioweza kupokea injili. “Ukweli” wa Walamani kuhusu Wanefi ulikuwa kwamba Nefi aliiba urithi wa kaka yake na kwamba uzao wa Nefi walikuwa waongo ambao waliendelea kuwaibia Walamani kile kilichokuwa haki yao. .9 “Kweli” hizi zililisha chuki kundi moja na lingine mpaka mwishowe ikawamaliza wote.
Ni wazi kwamba, kuna mifano mingi katika Kitabu cha Mormoni ambayo inakinzana na haya mambo yasiyo na uasili. Hata hivyo, Wanefi na Walamani waliamini hizi “kweli” ambazo zilichonga kudra ya hawa watu ambao wakati mmoja walikuwa watu wenye nguvu.
Asili na Ukweli wa Binadamu
Kwa njia fulani sisi sote huathirika kwa urahisi kwa dhana geni kama hizi.
“Kweli” tunazoshikilia uchonga ubora wa jamii zetu pamoja na hulka zetu za kibinafsi. Mara nyingi nyingi “kweli” hizi zote zinategemea ushahidi usio kamili, na usio sawa sawa na, wakati mwingine, wanaridhisha sababu za ubinafsi.
Sehemu ya sababu za uamuzi duni huja kutokana na uelekeo wa binadamu wa kutia waa mstari kati ya imani na ukweli. Sisi mara nyingi tunachanganisha imani na ukweli, tukifikiria kwamba kwa sababu kitu kama kinaleta maana au kinafaa, lazima kiwe ni kweli. Kinyume chake, wakati mwingine hatuamini ukweli au tunaukataa kwa sababu itatuhitaji kubadilika au kukubali kuwa sisi tumekosa. Mara nyingi, ukweli hukataliwa kwa sababu hauonekani kuwa sawa na uzoefu wa hapo awali.
Wakati maoni ya “kweli” za wengine zinakinzana na zetu wenyewe, badala ya kufikiria uwezekano wa kwamba kunaweza kuwa na habari ambazo zinaweza kuwa za usaidizi na kukuza au kushamirisha kile tunachojua, sisi mara nyingi tunarukia uamuzi au kufanya dhana kwamba yule mtu mwingine ndio amepotoka, akili punguani, au hata kwa kujua tunajaribu kudanganya.
Kwa bahati mbaya, huu uelekeo unaweza kuzangaa katika maeneo yote ya maisha yetu---kutoka michezo hata uhusiano na kutoka dini hadi siasa.
Ignaz Semmelweis
Mfano wa janga la uelekeo huu ni hadithi ya Ignaz Semmelweis, daktari Mhangari ambaye aliafanya kazi ya udaktari wakati wa kati kati ya karne ya 19. Hapo mwanzoni wa kazi yake, Dkt. Semmelweis alijifunza kwamba asili mia 10 ya wanawake ambao waliokuja kwenye kiliniki yake walikufa kutokana na homa ya kulazwa hali kiasi cha vifo katika kiliniki jirani ilikuwa chini ya asili mia 4. Akaamua kuchunguza kwa nini.
Baada ya kuchunguza hizi kiliniki mbili, Dkt. Semmelweis aliamua kwamba tofauti iliyokuweko ilikuwa ni kuwa, yake ilikuwa kliniki ya mafunzo ambapo maiti zilikaguliwa. Alipata kuwa madaktari ambao walienda moja kwa moja kutoka kufanya utafiti wa maiti na kwenda kuzalisha kina mama. Akafanya uamuzi kwamba kwa jinsi fulani maiti zilikuwa zinachafua mikono yao na kusababisha homa kali sana.
Alipoanza kutoa mapendekezo kwamba madaktari wasugue mikono yao na kioevu cha chokaa iliyotiwa klorini, alikabiliwa na upinzani na kubezwa. Uamuzi wake ulikinzana na “kweli” za madaktari wengine. Hata wengine kati ya wenzi wake waliamini kwamba ilikuwa upuuzi kufikiria kwamba mikono ya daktari ingeweza kuwa najisi au kusababisha magonjwa.
Lakini Semmelweis alisisitiza, na akafanya iwe sera kwa madaktari katika kiliniki yake kuosha mikono yao kabla ya kuzalisha kina mama. Matokeo yake, kiasi cha vifo mara moja vilipunguka kwa asili mia 90. Semmelweis akahisi kuwa uthibitisho na akawa na hakika kwamba mazoea sasa yatatumika kote katika jamii ya madkatari wa afya. Lakini alikuwa amekosea. Hata baada ya matokeo ya ajabu yake hayakuwa ya kutosha kubadili akili za madaktari wengi wa siku hizo.
Je! Inawezakana Kujua Ukweli?
Jambo kuhusu ukweli ni kwamba unakuwepo hata zaidi ya imani. Ni kweli hata kama hakuna mtu anayeiamini.
Tunaweza kusema magharibi ni kaskazini na kaskazini ni magharibi mchana kutwa na hata kuamini hivyo kwa moyo wetu wote, lakini ikiwa, kwa mfano tunataka kusafiri kwa ndege kutoka Quito, Ecuador, hadi New York Mjini katika Marekani, kuna njia moja tu ambayo itatuelekeza sisi hadi huko, na hiyo ni kaskazini---magharibi haitafaa.
Hakika, huu ni ufafanuzi rahisi wa safari za ndege. Hata hivyo, kama kwa kweli kuna kitu kama ukweli kamili---ukweli usioweza kushambulika, usiobadilika.
Ukweli huu ni tofauti na imani. Ni tofauti na tumaini. Ukweli kamili hautegemei juu ya maoni ya umma au umashuhuri. Kura haziwezi kuubadilisha. Hata kwa mapendekezo ya mtu mashuhuri ya mamlaka yasiyoweza kwisha yanayoweza kuibadilisha.
Sasa tunaweza kupata kweli kwa jinsi gani?
Mimi naamini kwamba Baba yetu wa Mbinguni hupendezwa na watoto Wake wanapotumia talanta zao na akili zao kwa bidii kugundua ukweli. Katika karne nyingi wanaume na wanawake wenye hekima ---kupitia kwa mantiki, akili, utafiti wa sayansi, na, naam, maongozi---wamegundua ukweli. Huu ugunduzi umeshamirisha binadamu, umeboresha maisha yetu, na kuleta shangwe, kushangaa, na mastajabu
Hata hivyo, mambo tuliyofikiria wakati mmoja tunajua yanaendelea kuwa bora, kurekebishwa, au hata kukinzwa na wasomi hodari ambao wanajaribu kuelewa ukweli.
Kama sote tujuavyo, ni vigumu sana kuchanganua ukweli kutokana na uzoefu wetu. Kuzidisha sana, tuna adui, “Ibilisi, [ambaye] kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.”10
Shetani ni mlaghai mkubwa, “mshitaki wa ndugu,”11 baba wa uongo wote,12 ambaye daima hutafuta kuwadanganya kwamba aweze kutupendua sisi.13
Adui ana mikakati mingi ya ujanja ya kuwaweka watu mbali na ukweli. Anawapa wengine imani kwamba ukweli unategemea mambo na wakati. Akipendeza hisia zetu, upendeleo na haki, huuweka ukweli halisi kufichika kwa kudai kwamba “ukweli” wa mtu ni halali kama wa wengine wale.
Wengine huwavutia kuamini kwamba kuna ukweli kamili mahali huko, lakini kwamba ni vigumu kwa mtu yeyote kuujua.
Kwa wale ambao tayari wanapokea ukweli, mkakati wake wa msingi ni kueneza mbegu ya shaka. Kwa mfano, yeye ameshasababisha washiriki wengi wa Kanisa kujikwaa wanapogundua habari kuhusu Kanisa ambazo zinaonekana kukinzana na kile walichokuwa wanajua awali.
Kama umepata uzoefu kama huo, kumbuka kwamba katika kipindi hiki cha habari kuna wengi wanaoleta shaka kuhusu chochote na kila kitu, wakati wowote na mahali popote.
Unaweza kupata hata wale ambao bado wanadai kwamba wana ushahidi kuwa ulimwengu ni tambarare, kwamba mwenzi ni hologramu, na kwamba nyota fulani wa filamu wao kihalisi ni wageni kutaka sayari ingine. Na daima ni vyema kuelewa, kwa sababu tu kitu kimechapishwa kwenye gazeti, kinatokeza kwenye Intaneti, kinarudiwa kila mara, au kina kundi la wafuasi wenye ushiwishi mkubwa haiifanyi kuwa kweli.
Wakati mwingine madai ua habari za uongo uwasilishwa kwa njia ambayo inaonekana kuwa ni ya kuaminika sana. Hata hivyo, unapokumbana na habari ambazo zinakinzana na neno lililofunuliwa la Mungu, kumbuka kwamba wanaume vipofu katika methali ya tembo awangeweza kamwe kueleza kwa usahihi ukweli kamili.
Sisi kwa kweli hatujui mambo yote---hatuwezi kuona kila kitu. Kile kinaweza kuonekana kama kinzani sasa kinaweza kueleweka kikamilifu kama tutatafuta na kupata habari ambazo ni za kuaminika sana. Kwa sababu sisi tunaona kupitia kioo chenye ukungu, ni sharti tuamini Bwana, yeye huona mambo yote wazi.
Naam, ulimwengu wetu umejaa makanganyiko. Lakini hatimaye maswali yetu yote yatajibiwa. Mashaka yetu yote yatabadilishwa na uhakika. Na hii ni kwa sababu kuna chanzo kimoja cha ukweli ambao ni kamili, sahihi, usioharibiwa. Chanzo hicho ni hekima yetu isio na mwisho na Baba yetu wa Mbinguni anayejua yote. Yeye anajua ukweli kama ulivyokuwa, kama ulivyo, na basi kama utakavyokuwa.14 “Ajuaye vitu vyote…; na yeye yu juu ya vitu vyote, na vitu vyote viko kwake, na ni vyake yeye.”15
Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo, anatoa ukweli Wake kwetu, watoto Wake wa ulimwenguni.
Basi, huu ukweli ni nini?
Ni injili Yake. Ni injili ya Yesu Kristo. Yesu Kristo---Yeye ni njia, kweli, na uzima.”16
Kama tu tunaweza kuwa ujasiri na imani ya kutosha kutembea katika mapito Yake, itatuongoza sisi kwenye imani ya moyo na akili, maana ya kudumu katika maisha, kwa furaha katika ulimwengu huu, na kwa shangwe katika ulimwengu ujao. Mwokozi “hayupo mbali na kila mmoja wetu.”17Tuna ahadi Yake kama tutamtafuta Yeye kwa bidii, tutampata Yeye.18
Wajibu Wetu ni Kutafuta Ukweli
Je! Tunaweza kujua vipi kwamba “ukweli” huu ni tofauti na mwingine wowote? Je! Tunaweza vipi kuamini “ukweli” huu?
Mwaliko wa kumwamini Bwana hautuondolei sisi jukumu la kujijulia wenyewe. Hii ni zaidi ya fursa; huu ni wajibu, na ni mojawapo wa sababu za sisi kutumwa huku ulimwengu.
Watakatifu wa Siku za Mwisho hawaulizwi kukubali chochote wanachosikia kiolela. Tunahimizwa kufikiria na kujigundulia ukweli wenyewe. Tunatarajiwa kutafakari, kutafuta, kutathimini, na kwa hivyo kupata elimu ya kibinafsi ya ukweli.
Brigham Young alisema: “Mimi … ninahofia kwamba watu hawa wana imani nyingi sana katika viongozi wao kwamba wao hawatajiulizia wenyewe kutoka kwa Mungu kama wanaongozwa na Yeye. Ninaogopa watakaa katika hali ya upofu wa kujiamini. … Acha kila mwanaume na mwanamke ajue, kwa mnong’ono wa Roho Mtakatifu kwao wenyewe, kama viongozi wao wanatembea katika mapito ambayo Bwana ameamuru.”19
Tunatafuta ukweli popote tunapoweza kuupata. Nabii Joseph Smith alifunza kwamba “Umormoni ni ukweli. … Kanuni ya kwanza na ya msingi ya dini yetu takatifu ni, kuwa tunaamini kwamba tuna haki ya kukumbatia yote, na kila chembe ya ukweli, bila pingamizi au kuzuiwa na imani au fikra za kishirikina za binadamu.”20
Naam, sisi tuna ujalivu wa injili ya milele, lakini hii haimaanishi sisi tunajua kila kitu. Kwa kweli, kanuni moja ya injili ya urejesho ni imani yetu kwamba Mungu “bado atafunua vitu vingi vikuu na muhimu.”21
Urejesho wa injili ya Yesu Kristo ulitokea kwa sababu kijana mmoja mwenye moyo wa unyenyekevu na akili makini alikuwa anatafuta ukweli. Joseph alijifunza na kutenda, na akagundua kwamba kama anapungukiwa na hekima, anaweza kumwomba Mungu na ukweli hasa utapeanwa kwake.22
Muujiza mkubwa wa Urejesho sio tu kwamba ilirekebisha mwazo potovu na mafundisho yaliyoharibiwa---ingawa kwa kweli ilifanya hivyo---bali kwamba ilifungua wazi pazia za mbinguni na kuanzisha mtiririko thabiti wa nuru mpya na elimu ambayo imeendelea hadi leo.
Kwa hivyo tunaendelea kutafuta ukweli kutoka kwa vitabu vyote vizuri na vyanzo vizuri. “Kama kuna kitu chochote kilicho chema, chenye kupendeza, au chenye taarifa njema au chenye kustahili sifa, tunayatafuta mambo haya. .”23 Kwa njia hii tunaweza kushinda ulaghai wa mwovu. Katika njia hii tunaweza kujifunza “fundisho juu ya fundisho; mstari juu ya mstari.”24 Na tunajifunza kuwa “akili huambatana na akili; na hekima hupokea hekima; na kweli huikumbatia kweli.25
Marafiki zangu vijana, mnapokubali majukumu ya kutafuta ukweli kwa akili makini na moyo mnyenyekevu, mtakuwa mnawakubali wengine zaidi, wazi kusikiliza, tayari zaidi kuelewa, waelekevu kujenga badala ya kubomoa, na hutapendelea kuenda pale Bwana anapotaka wewe kwenda.
Roho Mtakatifu---Mwongozo Wetu kwa Ukweli Wote
Hebu fikiria kuhusu hivi. Kwa hakika una mwenzi wenye uwezo na kiongozi wa kuaminika katika huu utafutaji unaoendelea wa ukweli. Yeye ni nani? Ni Roho Mtakatifu. Baba yetu wa Mbinguni alijua jinsi itakuwa vigumu kwetu kutenganisha kwa kuchekecha kelele nyingi na kugundua ukweli katika maisha ya muda. Yeye alijua tutaona tu sehemu ya ukweli na alijua kwamba Shetani atajaribu kutulaghai. Kwa hivyo Yeye alitupatia kipawa cha mbinguni cha Roho Mtakatifu ili kuangaza akili zetu, kutufundisha, na kushuhudia kwetu kuhusu ukweli.
Roho Mtakatifu ni mfunuaji. Yeye ni mfariji, ambaye hutufunza sisi “ukweli wa mambo yote; [ambaye] anajua vitu vyote, na ana uwezo wote kulingana na hekima, huruma, ukweli, haki, na hukumu.”26
Roho Mtakatifu ni kiongozi wa hakika na salama wa kusaidia watu wote ambao hutafuta Mungu wanaposafiri maji yanayosumbua ya mkanganyiko na ukinzani.
Ushahidi wa ukweli kutoka kwa Roho Mtakatifu unapatikana kwa wote, kila mahali, kote ulimwenguni. Wale wote wanaotafuta ukweli, wale wanautafakari katika akili zao,27 na watauliza “na moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo, [watajua] ukweli … kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.”28
Na kuna kipawa ziada, kisichosemeka cha Roho Mtakatifu kinapatikana kwa wote wanaojihitimisha kupitia ubatizo na kuishi kwa ustahiki wa uenzi Wake thabiti.
Naam, Baba yenu wa Mbinguni wenye upendo hatawaacha peke yenu katika haya maisha ya muda kutangatanga gizani. Hamhitaji kulaghaiwa. Mnaweza kushinda giza la ulimwengu huu na kugundua ukweli mtakatifu.
Wengine, hata hivyo, hawatafuti ukweli sana kama vile wanajitahidi kwa ubishi. Hawatafuti kwa uaminifu kujifunza; badala, wana hamu ya kubishana, kujikweza kwa usomi wao basi kusababisha mabishano. Wanapuuza au kukataa ushauri wa Mtume Paulo kwa Timotheo: “Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa [huzaa ugomvi].”29
Kama wafuasi wa Yesu Kristo, tunajua kwamba mabishano kama hayo hayapatani kabisa na Roho ambaye sisi tunategemea katika utafutaji wetu wa ukweli. Mwokozi aliwaaonya Wanefi:“Kwani amin, amin, nawaambia, yule ambaye ana roho ya ubishi siye wangu, lakini ni wa ibilisi, ambaye ni baba wa ubishi.”30
Kama mtafuata Roho, utafutaji wenu wa ukweli wa kibinafsi hatimaye hutawaelekeza kwa Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo, kwani Yeye ndiye “njia, ukweli na uzima.”31Hii inaweza kuwa isiwe njia ifaayo sana, pengine pia inaweza kuwa ni njia isiyotumika sana, na itakuwa njia ya milima ya kukwea, mito ya mkondo mkali kuvuka, bali itakuwa ndio njia Yake---njia ya Mwokozi ya ukombozi.
Naongezea ushahidi wangu kama Mtume wa Bwana, kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Najua haya kwa moyo wangu na akili zangu zote. Najua haya kwa ushahidi na uwezo wa Roho Mtakatifu.
Nawaomba msibakishe juhudi zozote katika kutafuta kwako kujua ukweli huu mwenyewe---kwa sababu ukweli huu utakuweka huru.32
Ndugu zangu vijana wapendwa, ninyi ni tumaini la Israeli. Sisi tunawapenda. Bwana anawajua ninyi, Yeye anawapenda. Bwana ana imani kubwa katika ninyi. Yeye anajua ufanisi wenu, na Yeye anashughulikia changamoto na maswali katika maisha.
Ni maombi yangu kwamba ninyi mtatafuta ukweli kwa hamu na bila kukoma, kwamba mtatamani kunywa kutoka kwa birika ya ukweli, ambayo maji yake ni halisi na matamu, “kisima cha maji yanayochipuka katika uzima wa milele.”33
Nawabariki ninyi kwa imani katika Bwana na hamu ya kina sana ya kutambua ukweli kisahihi kutokana na kosa---sasa na maishani mwenu mwote. Haya ndio maombi yangu na baraka zangu, katika jina la Yesu Kristo, amina.
© 2013 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Kiingereza kiliidhinishwa: 8/12. Tafsiri ilihinishwa: 8/12. Tafsiri ya What Is Truth? Swahili. PD50045368 743