“Hitaji la Kanisa,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.
Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Hitaji la Kanisa
Dondoo
Leo, ujumbe wangu unahusu watu kama hao wema na wenye fikra ya kidini ambao wameacha kuhudhuria au kushiriki katika makanisa yao. Ninaposema “makanisa,” ninajumuisha masinagogi, misikiti au mashirika mengine ya kidini. Tuna wasiwasi kwamba mahudhurio kwenye majengo haya yote yameshuka kwa kiasi kikubwa, nchi nzima. …
Uhudhuriaji na ushiriki kikamilifu kanisani hutusaidia kuwa watu bora na ushawishi bora katika maisha ya wengine. …
Kanisani tunajumuika na watu wema ambao wanajitahidi kumtumikia Mungu. Hii inatukumbusha kwamba hatuko peke yetu katika shughuli zetu za kidini. Sote tunahitaji kujumuika na wengine na mijumuiko ya kanisa ni baadhi ya mijumuiko mizuri zaidi tunayoweza kuwa nayo. …
… Waumini ambao huacha kuhudhuria Kanisani na kutegemea mambo yao binafsi ya kiroho hujitenga kutoka kwenye mambo haya muhimu ya injili: nguvu na baraka za ukuhani, utimilifu wa mafundisho yaliyorejeshwa na motisha na fursa za kufanyia kazi mafundisho hayo. …
Katika kuongezea kwenye kuhisi amani na furaha kupitia wenza wa Roho, waumini wetu wanaohudhuria Kanisani hufurahia matunda ya kuishi injili, kama vile baraka za kuishi neno la hekima na ustawi wa kifedha na kiroho ulioahidiwa kwa kuishi sheria ya zaka. …
… Utimilifu wa mafundisho na ibada zake za kuokoa na kuinuliwa zinapatikana tu katika kanisa lililorejeshwa.