2021
Kwa Nguvu za Mungu katika Utukufu Mkuu
Novemba 2021


“Kwa Nguvu za Mungu katika Utukufu Mkuu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumamosi Alasiri

Kwa Nguvu za Mungu katika Utukufu Mkuu (1 Nefi 14:14)

Dondoo

mkate na maji ya sakramenti

Maagano, yaliyoingizwa kupitia maagizo ya ukuhani yenye mamlaka, yanaweza kutufunga kwa Bwana Yesu Kristo na ndiyo kiini muhimu cha kazi ya wokovu na kuinuliwa katika pande zote za pazia.

Kazi ya umisionari na ya hekalu na historia ya familia ni mambo yanayokamilishana na yanayohusiana ya kazi moja kuu ambayo inalenga maagano na maagizo matakatifu ambayo hutuwezesha kupokea nguvu za utauwa katika maisha yetu na, hatimaye, kurudi kwenye uwepo wa Baba wa Mbinguni. …

Tunachukua nira ya Mwokozi juu yetu tunapojifunza kuhusu, kupokea kwa ustahiki, na kuheshimu maagano na Ibada takatifu. Tunafungamana kwa uthabiti pamoja na Mwokozi wakati tunapokumbuka kwa uaminifu na kufanya kadiri ya uwezo wetu kuishi kulingana na masharti tuliyokubali. Na muunganiko huo Kwake ni chanzo cha nguvu za kiroho katika majira yote ya maisha yetu. …

Ahadi na baraka za agano vinawezekana tu kwa sababu ya Mwokozi wetu,Yesu Kristo. Anatualika kumtazamia, kuja Kwake, kujifunza kwake, na kujifunga Kwake kupitia maagano na maagizo ya injili Yake iliyorejeshwa. Ninashuhudia na kuahidi kwamba kuheshimu maagano kutatukinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu. Na ninashuhudia kwamba Bwana Yesu Kristo aliye hai ni Mwokozi wetu.