“Mambo ya Nafsi Yangu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.
Kikao cha Jumamosi Alasiri
Mambo ya Nafsi Yangu
Dondoo
Vijana mara nyingi wananiuliza ninaamini nini na ni kwa nini ninaamini. …
Je, ninaweza kushiriki nanyi baadhi ya mambo ya nafsi yangu? Mambo haya yanatumika kwa wote wanaotafuta kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo. …
Kwanza, mpende Mungu Baba na Yesu Kristo, Mwokozi wetu. …
Pili, “Mpende jirani yako.” [Mathayo 22:39]. …
Tatu, jipende mwenyewe.
Hapo ndipo wengi wanaposumbuka. Je, si ajabu kwamba kujipenda sisi wenyewe huonekana kutokuwa rahisi kuliko kuwapenda wengine? Walakini, Bwana amesema, “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” [Mathayo 22:39] Anathamini uungu ulio ndani yetu; nasi tuuthamini. Tunapolemewa na makosa, maumivu ya moyo, hisia za kutostahili, kukatishwa tamaa, hasira, au dhambi, nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi ni, kwa mpango wa kiungu, moja ya mambo ambayo huinua roho.
Nne, shika amri. …
Tano, daima kuwa mstahiki kuhudhuria hekalu. …
Sita, furahi na uchangamke. …
Saba, fuata nabii wa Mungu aliye hai.
Hii inaweza kuwa ya saba kwenye orodha yangu ya vitu, lakini ndilo la kwanza kwenye akili yangu kwa kuzingatia umuhimu wake leo.
Tunaye nabii wa Mungu duniani leo! Kamwe usipunguze maana ya hilo kwako. …
… Ninakualika uweke nane, tisa, na kumi za kwako. Fikiria njia ambazo unaweza kushiriki “mambo” yako ya moyoni na wengine na uwahimize kuomba, kutafakari, na kutafuta mwongozo wa Bwana.