2010
Kuweza Kujitegemea Mwenyewe
Januari 2010


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Januari 2010

Kuweza Kujitegemea Mwenyewe

Fundisha maandiko na madondoo haya au, ikihitajika, kanuni nyingine ambayo itabariki akina dada unaowatembelea. Toa ushuhuda wa fundisho hili. Alika wale unaowafundisha kushirikisha walichohisi na kujifundisha.

Kujitegemea Mwenyewe Ni Nini?

“Kujitegemea Mwenyewe inamaanisha kutumia baraka zetu zote kutoka kwa Baba wa Mbinguni ili kujitunza na familia zetu na kupata suluhu kwa shida zetu wenyewe.Kila mmoja wetu ana jukumu la kujaribu kuzuia matatizo kabla hayajatokea na kujifunza kushinda changamoto zinapotokea. …

“Ni kwa jinsi gani tunaweza Kujitegemea Mwenyewe? Tunaweza kujitegemea wenyewe kupitia kwa kupokea ujuzi wa kutosha, elimu, na kisomo; kwa kusimamia pesa na raslimali kwa hekima, kwa kuwa imara kiroho, kujitayarisha kwa dharura na matukio; na kwa kuwa na afya ya kimwili na ustawi mwema wa kijamii na hisia.”1

Julie B. Beck, Rais wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama.

Jukumu la Kiinjili

“Tunavyoishi kwa uwekevu na kuongeza karama na talanta zetu, tunakuwa zaidi wenye kujitegemea wenyewe. Kujitegemea mwenyewe ni kuchukua jukumu la ustawi wetu wa kiroho na kimaisha na kwa wale ambao Baba wa Mbinguni amewaweka chini ya utunzaji wetu. Ni tu tunapojitegemea wenyewe ndipo tunaweza kwa kweli kufuata Mwokozi katika kuhudumia na kubariki wengine.

“Ni muhimu kuelewa kwamba kujigemea wenyewe ni njia ya kufaulu. Lengo letu la msingi ni kuwa kama Mwokozi, na lengo hilo linaboreshwa na huduma yetu isiyo na choyo kwa wengine. Uwezo wetu wa kuhudumu unaogezwa au kudidimizwa na kiwango chetu cha kujitegemea wenyewe.”2

Mzee Robert D. Hales wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili.

“Kujitegemea Mwenyewe ni zao la kazi yetu na uhimili utekelezaji mwengine wote wa ustawi. Ni jambo muhimu katika ukuaji wetu wa kiroho vilevile wa ufanisi wa kimaisha. Kuhusu kanuni hili, Rais Marion G. Romney [1897–1988] amesema: ‘Acha tufanye kazi kwa kile tunachohitaji. Acha tuwe wenye kujitegemea wenyewe na huru. Wokovu unaweza kupatikana sio kwa kanuni nyingine. Wokovu ni jambo la kibinafsi, na ni lazima tutekeleze wokovu wetu wenyewe kwa mambo ya kimaisha na kiroho’ …

“Rais Spencer W. Kimball [1895–1985] alifunza zaidi kuhusu kujitegemea mwenyewe: ‘Jukumu kwa ustawi wa kijamii, kihisia, kiroho, au kiuchumi wa kila mtu upo juu yake, pili upo juu ya familia yake, na tatu upo juu ya Kanisa ikiwa yeye ni mshiriki mtiifu.’”3

Rais Thomas S. Monson.

Muhtasari

  1. “The Welfare Responsibilities of the Relief Society President,” Basic Principles of Welfare and Self-Reliance (2009), 4–5.

  2. “A Gospel Vision of Welfare: Faith in Action,” Basic Principles of Welfare and Self-Reliance (2009), 1–2.

  3. “Guiding Principles of Personal and Family Welfare,” Liahona, Feb. 1987, 3.

Chapisha