2010
Baraka zako za Baba Mkuu
Februari 2010


Vijana

Baraka zako za Baba Mkuu

Rais Monson anaelezea baraka za baba mkuu kama “Liahona ya kibinafsi ya kupanga njia yako na kuelekeza njia yako.” Sasa hii baraka ni nini, na inaweza kusaidia kuelekeza maisha yetu vipi?

Baraka za baba mkuu ni nini?

Baraka zako zina makusudi mawili. Kwanza, zinataja nasaba, au kabila lipi katika nyumba ya Israeli unalotokea. Pili, zitakuwa na habari za kukusaidia kukuelekeza wewe. Babaka zako zinaweza kuwa na ahadi, wasaa, na maonyo.

Ninafaa kuwa na umri gani ili kupokea baraka zangu?

Hakuna umri uliowekwa, lakini unafaa kuwa umepevuka yakutosha kuelewa uhalisi mtakatifu wa baraka hii. Washiriki wengi huanza kufikiria juu ya kupokea baraka zao katika miaka yao ya ujana.

Nawezaje kupokea hii baraka?

Kwanza ongea na askofu au rais wa tawi lako. Kama u tayari na u mstahiki, utapokea kibali. Baada ya hivyo, unaweza kupanga miadi na baba mkuu katika eneo lako.

Nifanye nini na hii baraka yangu?

Iweke katika mahali salama, na uisome kila mara. Kumbuka, baraka yako ni takatifu na ya kibinafsi. Unaweza kuishirikisha na wanafamilia wa karibu, lakini haufai kuishirikisha kwa uma. Pia, baraka zote zilizotajwa katika baraka yako ya baba mkuu zinasimamiwa na uaminifu wako na wakati wa Bwana.

Chapisha