Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Februari 2010
Katika Kuwa Tayari Kiroho
Ushauri kutoka kwa Nabii Wetu
Msingi wa Imani
“Kama hatuna msingi wa kina wa imani na ushuhuda thabiti wa ukweli, tunaweza kuwa na matatizo kustahimili dhoruba kali na upepo wa baridi wa shida ambazo hazina budi kutujia kila mmoja wetu.“
Maisha ya kimwili ni muda wa kujaribiwa, wakati wa kuonyesha ustahiki wetu wa kutuwezesha kurudi katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni. Ili sisi tuweze kujaribiwa, ni lazima tukabiliane na changamoto na dhiki. Haya yanaweza kutuvunja sisi, na uso wa nafsi zetu unaweza kualika na kubomoka—hivi ni, kama misingi yetu ya imani, ushuhuda wetu wa kweli haijakita mizizi sana ndani yetu.”1
Jifunze Masomo ya Awali
“Katika kutafuta ubora wetu wenyewe, maswala kadha yataelekeza kufikiria kwetu: Mimi ni kile ninachotaka kuwa? Mimi niko karibu na Mwokozi leo zaidi nilivyokuwa jana? Nitakuwa karibu kesho bado? Nina ujasiri wa kubadilika kwa ubora? …
“Miaka imekuja na miaka imeenda, lakini mahitaji ya ushuhda wa injili yanaendelea kuwa muhimu. Jinsi tunavyosonga kuelekea siku zijazo, sharti tusipuuze masomo ya awali.”2
Liahona Yako ya Kibinafsi“
Baraka za baba mkuu zako ni zako na zako peke yako. Zinaweza kuwa fupi au ndefu, halisi au za ndani sana. Urefu na lugha haiboreshi baraka za baba mkuu. Ni Roho ndiye huleta maana kamili. Baraka zako hazifai kukunjwa kimaridadi na kuwekwa kando. Haifai kuwekwa kwenye fremu au kuchapishwa. Bali, inafaa kusomwa. Inafaa kupendwa. Inafaa kufuatwa. Baraka zako za baba mkuu zitakuwezesha kupitia katika usiku wa giza. Itakuelekeza wewe kupitia hatari za maisha. … Baraka zako za baba mkuu kwako ni Liahona ya kibinafsi ya kupanga njia na kuelekeza njia yako. …“
Ustahimilifu unaweza kuhitajika wakati tunapotazama, ngojea, na fanyiza kwa baraka zilizoahidiwa kutimizwa.”3
Njoo Kwake
“Kumbuka kwamba hautembei peke yako. … Jinsi unavyotembea kupitia katika maisha, kawaida kuelekea kwenye nuru, na vivuli vya maisha vitabakia nyuma yenu. …
“Jinsi [mimi] nilivyogeukia maandiko kwa maaongozi, neno mahususi linasimama wazi muda baada ya muda tena. Neno hii [ni] ‘njoo. ’ Bwana alisema, Njoo kwangu.’ Alisema, ‘Njoo na ujifunze juu nyangu.’ Alisema pia, ‘Njoo, na unifuate mimi.’ Napendelea hilo neno, njoo. Ombi langu ni kwamba tutaweza kumwendea Bwana.”4
© 2009 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/09 Tafsiri Iliidhinishwa: 6/09. Tagsiri ya First Presidency Message, February 2010 Swahili. 09362 743