Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Februari 2010
Kusimamia Mali Vyema na Kuepukana na Deni
Fundisha maandiko na madondoo haya au, ikihitajika, kanuni nyingine ambayo itabariki akina dada unaowatembelea. Toa ushuhuda wa fundisho hili. Alika wale unaowafundisha kushirikisha walichohisi na kujifundisha.
Kusimamia Mali
”’Kuishi kwa uekevu … kunamaanisha[kutunza] kwa mali yetu, upangaji wa busara wa mambo ya kifedha, upato kamili wa afya ya kibinafsi, na ukuzaji wa kutosha wa elimu na mpangilio wa ajira, kufanyizia uangalifu ipasavyo kwa uzalishaji wa nyumbani na uhifadhi pamoja na ukuzaji wa urekebishaji wa mhemuko. … Kama tunaishi tutaishi vyema na kwa uekevu, tutakuwa salama kama kwenye chanda cha mkono Wake.”1
Rais Spencer W. Kimball (1895–1985).
”Ni ujuzi gani tunaohitaji ili kutusaidia sisi kuwa wenye kujisimamia wenyewe? … Katika siku za mapema za Kanisa, Brigham Young aliwaomba kina dada kujifunza kuzuia magonjwa katika familia, kuanzisha viwanda vya nyumbani, na kujifunza uhasibu na uwekaji hesabu na ujuzi mwengine wa mikono. Hizo kanuni bado zinasimama leo. Elimu inaendelea kuwa muhimu sana, …
”Niliwauliza maaskofu kadha ujuzi wa kujisimamia ambao kina dada katika kata zao walihitaji sana, na walisema upangaji bajeti. Wanawake wanahitaji kuelewa matokeo ya ununuzi wa kukopa na kutoishi kulingana na bajeti. Ujuzi wa pili maaskofu waliorodhesha ni upishi. Mlo uliotayarishwa na kuliwa nyumbani kwa kawaida ni bei nafuu, una afya, na unachangia katika uhusiano wa familia thabiti.”2
Julie B. Beck, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama.
Kuepukana na Deni
“Naomba nishauri hatua tano muhimu za uhuru wa kifedha. …
“Kwanza, lipa zaka yako, …
“Pili, tumia kidogo kuliko unavyopata. …
“Tatu, jifunze kuweka akiba. …
“Nne, timiza wajibu wako wa kifedha. …
“Tano, wafunze watoto wako kufuata mfano wako.”3
Mzee Joseph B. Wirthlin (1917–2008) wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili.
”Tunapoingia katika deni, tunapeana mengine ya wakala wetu wenye dhamani, usio na bei na kujiweka katika utumwa wa kujiwekelea. Tunawekea kifungo muda wetu, nguvu zetu na mali yetu kulipa kile tulichokopa—rasmali ambayo ingeweza kutumika kutusaidia wenyewe, familia zetu, na wengine. …
“Ili kulipa madeni yetu sasa na kuepukana na deni wakati ujao tunahitajika kufanya imani katika Mwokozi—sio tu kufanya vyema bali kuwa bora. Inahitaji imani kuu ili kutamka maneno haya halisi, ‛Hatuwezi kumudu.’ Inahitaji imani ili kuamini kwamba maisha yatakuwa bora jinsi tunavyoyaacha matakwa yetu ili tumudu mahitaji yetu na mahitaji ya wengine.”4
Mzee Robert D. Hales wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili.
© 2009 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/08 Tafsiri Iliidhinishwa: 6/09. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, February 2010. Swahili. 09362 743